Katika muda mchache niliojiingiza kwenye soko la ajira, nimegundua mambo haya

kyanyangwe

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
1,147
2,746
1. connection hasa private sector ni muhimu,mfano mimi sehemu niliyojishkiza, hata hawakutangaza nafasi za kazi,isipokua HR anafahamiana na jamaa yangu hivyo nikapigiwa pande.

2. Experience ya kuanzia 3 years kwenye reputable companies ni muhimu sana.ninaposema reputable companies namaanisha makampuni makubwa kama Vodacom, Twiga Cement, TBl,NGO za kimataifa na mengine ya dezaini hiyo au Government entities.aisee hii kitu ni muhimu sana,mfano jamaa yangu juzi kati aliomba nafasi za sales kwenye kampuni moja hivi ya wazungu wana kiwanda cha Bia hapa Tanzania, jamaa ana experience ya sales ya like 5 years kwenye hizi kampuni za wachina wale wazungu wakamkataa live kwenye interview kuwa hawawezi kumchukua coz hana experience kutoka kwenye kampuni inayoeleweka.

3. Chuo ulichosoma kina matter aisee,nimegundua waajiri wengi wanapenda wahitimu wa kutoka vyuo flani flani.mfano private sectors wanapenda wahasibu kutoka udsm na mzumbe, serikalini wanapenda wahasibu kutoka Ifm, TIA na IAA.etc

4. Ukabila,aisee kuna taasisi zina ukabila.mfano kuna bank flani bika kuwa mtu wa kutoka kabila mojawapo hapa Tanzania liko huko kaskazini mwa nchi yetu hupati kazi kurahisi,pia kuna microfinance moja nayo bila kuwa wa kutoka kabila moja huko kanda ya ziwa lenye sifa ya kuwa na watu wababe ni ngumu kupata kazi.

5. ufaulu mzuri,japo sio saana ila ukiwa na GPA nzuri inasaidia walau hata kuitwa kwenye interview.

6. Uandishi mzuri wa CV, aisee ukiwa na cv iliyoandaliwa hovyo hovyo ni ngumu sana kuwavutia waajiri.

7. Udini nao una nafasi, kuna taasisi kama uchumi commercial bank, hawaajiri mtu asiyekua mlutherani.

8. Ndumba,ebana kuna watu wanaroga aisee kwa ajili ya kupata kazi.
 
Dunia ndio iko hivyo..usisahau kadi ya chama cha kijani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ndumba umepuyanga hayo sijui ukabila na udini sana tu tunaona hata makazini sehemu zinazokuwa na watu mchanganyiko ukabila upo ila udini sio sana sijaona

Pako ivi mfano wakati wa kuchangia labda harusi au msiba unaona mtu fulani kisa wa kanda fulani wenzie wanamchangia sana kingine hata ile kuzoeana pia watu kujitenga ni ivyo ivyo ,kuwa pamoja kupostiana japo hawajasoma pamoja ila wakutana kazini na wanatoka kanda moja inakuwa ivyo basi

Ila yote hayo hayana umuhimu kikubwa kazini jua kilichokupeleka ni taaluma yako fanya kazi usepe usiangaike kuforce mahusiano
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom