Katika mtazamo wa kitanzania: mwanasiasa ni nani?

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
Ndugu wanaJF,
Kitu kikiwa kibaya huchukiwa bali kizuri hupendwa.Vipo vizuri vinavyovalishwa sura ya ubaya na vipo vibaya vinavyovikwa joho la uzuri.
Katika mantiki hii, na mtazamo wa watanzania, siasa inaangukia wapi na kwahiyo mwanasiasa ni nani
 
Kwanza kabisa niseme asante sana kwa kuleta mada hii hapa JF.
Kwangu mimi wanasiasa ni mtu ambaye ninaweza kumfananisha kama nyoka CHATU. Kwa wale ambao wamewahi kuchunga porini mifugo kama ng'ombe, mbuzi, kondoo na kadhalika, bila shaka chatu wanamfahamu sana. Chatu ni mpole sana akiwa na shibe, lakini ni katili sana akiwa na njaa. Ukatili wake hauonyeshi kabla hajanasa windo bali baada ya kunasa windo. Ukiwa na mbwa mbele ya chatu mwenye njaa utaungana nami katika mantiki hii. Wakati wa njaa chatu ni mpole na mwenye macho ya kuvutia kiasi kwamba mbwa hujisogeza mwenyewe tena hata humng'ata mwenye mbwa yule wakati akijaribu kumnasua asimsogelee yule chatu. Chatu hujisogeza mwenyewe akiwa amefyata mkia hadi mdomoni mwa chatu na chatu bila hiana humviringisha yule mbwa na kumvunja vunja mbavu na kumuua mbwa na kisha hummeza.

Mwanasiasa vivyo hivyo, wakati wa kampeni huwa mpole ambaye kila lililo jema hutolea AHADI ZA KUTIMIZA MARA TU AKICHAGULIWA. Na wananchi bila kujidadisi humchagua kama vile mbwa ajisogezapo kwa chatu. Lakini cha ajabu baada ya kuchaguliwa Mwanasiasa huyu huwageuka wapiga kura wake na kuanza kutafuna hata nguvu zao (kufanya ufisadi). Tukiwa hoi bin taabani mwanasiasa huyu anatumia kejeli;
Mfano Malecela "Go to hell those who blem our good infrastructure"
Basil Mramba "Ikiwezekana hata wananchi wale majani lakini ndege ya Rais ipatikane.
Mkapa "Watanzania wavivu wa kufikiri" wakati huo akiwa anatutafuna nyuma la pazia la "UWAZI NA UKWELI"
Andrew Chenge "Pesa zenyewe ni vijisenti tu" Wakati wananchi wake wanakufa kwa kukosa madawa katika zahanati zao yeye anamiliki mabilioni huko ulaya halafu anadai hayo mabilioni ni "Vijisenti tu"
Na wengine wengi ambao wameweza kutoa kauli za namna hiyo.
Hapo ndipo mimi nawaona hawa wanasiasa ni "CHATU"
 
LO! KWA HIYO SIASA NI MAWINDO YA CHATU DHIDI YA MBWA!
IPO HAJA BASI YA KUIPATIA SIASA MAANA NYINGINE, VINGINEVYO OLE WAO MBWA!
 
siasa ni mtego wa kujipatia mali bila jasho na siasa ni blah blah!
Siasa hazikupaswa kuwa hivi, ndio maana natoa wito kwa watu wema kuuvamia uwanja wa siasa ili tuwang'oe walioifanya siasa ikadhanika kuwa mchezo mwovu.
siasa ni kwa ajili ya maendeleo na ustaarabu wa jamii
siasa ni kwa ajili ya mafanikio ya taifa
umefika wakati tumnyan'ganye ibilisi na watumishi wake taasisi na taaluma hii ya thamani
endapo hatutawanyang'anya basi nasi tutakuwa waovu kama wao
sharti tuinyakue taasisi hii mara moja
tusiendelee kuruhusu uchawi unahamia hadi BUNGENI!!!!!
 
Sasa dada waridi, naomba ushauri tufanyeje tuwangoe hawa waliovamia? (mimi na wewe) si yule wala wao.
 
Aika,
Mimi nimeamua kujiunga na chama cha siasa, chenye wanasiasa wanaoonesha wana siasa safi kuanzia dhamira zao na matendo yao, karibu chamani kama nawe una dhamira ya namna hiyo. Ni kupitia huko tutagombea uongozi katika chaguzi zijazo na hatimaye Mungu si Athuman, tutawang'oa vitini wachafuzi wa siasa. Join me Aika
 
Waridi,

ulipotea jamani. Umejiunga na chama gani? sera zao vipi huko. Hebu mwaga sera hapa maana na mimi nipo kwenye hizo harakati za kutafuta chama chenye sera nzuri zitakazowezesha kumkomboa mtanzania.
 
karibu sana,
kwa maelezo zaidi wasiliana na mmoja wa viongozi wa juu wa chama changu, e-mail yake ni kahangwagl@udsm.ac.tz, au nikupe simu yake kabisa?
 
Hadi niwasiliane na uongozi wa juu, hao wakubwa sana na wako busy. Naomba website ya chama chenu itakuwa rahisi zaidi, waweza tumia PM.

Asante.
 
siasa yetu tunaiharibu wenyewe kuruhusu viongozi muflisi kututawala kimawazo hadi maamuzi. Tuamke siasa ndo kila kitu kwa maisha ya mwanadamu duniani.Mwlm hakukosea ili nchi iendelee yahitaji SIASA SAFI, ARDHI, VIONGOZI BORA. WAPI TUMEKOSEA?????
HATUKO MAKINIIII...
 
nakwambia hayuko busy kama unavyofikiri, tena sasa hivi wana/tuna program ya kuhimiza akina mama wajuinge na mageuzi, mjaribishe uone atakavyokujibu haraka. Hata hivyo web nitakutumia, karibu sana tujenge chetu tuiokoe nchi
 
siasa yetu tunaiharibu wenyewe kuruhusu viongozi muflisi kututawala kimawazo hadi maamuzi. Tuamke siasa ndo kila kitu kwa maisha ya mwanadamu duniani.Mwlm hakukosea ili nchi iendelee yahitaji SIASA SAFI, ARDHI, VIONGOZI BORA. WAPI TUMEKOSEA?????
HATUKO MAKINIIII...
Nyauba,
well said.Nakuomba jiunge nasi tuitafute huo umakini na kuijenga siasa safi. Karibu
 
NCCR wale wa kwenye LUNINGA? Bado kuna SIASA huko?

Ndio kwanza chama kinazidi kupata nguvu, na sasa hivi kiko katika mchakato wa chaguzi kuanzia mashinani hadi ngazi ya taifa, hivyo ni zaidi ya kuonekana kwenye luninga unakokusema wewe
 
Labda naomba wan JF mnisaidie, nini maana ya SIASA? na ili uwe mwanasiasa ni lazima uwe kiongozi?
 
kwa mtazamo wangu, siasa ni njia azitumiazo mtu kutafuta kupata,au kutafuta kubakia kwenye mamlaka ya kiuongozi ili awatumikie waongozwa.

siasa safi ni pale njia hizo si za hila, bali za haki.Siasa chafu ni udanganyifu, hila na matumizi mabaya ya mamlaka inayotafutwa
 
Sasa tunaposema siasa safi lakini uongozi si bora, inaleta picha gani hapa? inawezekana kweli kuwa na uongozi bora halafu siasa chafu au kinyume chake? au hivi viwili vinakwenda pamoja?
 
Back
Top Bottom