Katika msimu huu wa mvua naombeni tujuzane mbinu za kukausha nguo

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Sehemu nyingi sahizi kuna mvua hapa nchini.

Ni neema na baraka kwavile tutapata vyakula.

Ila sasa kuna hii ishu ya nguo wakuu,

Wewe unadili nayo vipi?
 
Usifue ovyo ovyo na ukifua fua chache

Fua kwa ratiba siku ukiona hamna wingu

Fulia mashine na kukausha ili uanike muda mfupi
 
Au afue hivi

Kama ni suruali fua chini kule kwenye ile round, magotini, makalioni na sehem za mifuko

Tshirt fua makwapani na sehemu ya shingo halafu ianike kuining'iniza

Mashat ya mikono mirefu fua kwenye kola, makwapani na sehemu za viganja utakua umemaliza ukiona zimenyauka bado zinazizima piga pasi
 
Kamua sana

Unaweza kupunguza unyevu kwa pasi, ila usipige pasi nguo mbichi direct, tanguliza taulo au shuka,
Shuka litafyonza unyevu na unyevu utakaushwa na pasi baada ya hapo unaweza kuanika itakaa muda mfupi na kukauka.

Njia nyingine tumia feni kama ni lazima uvae hiyo nguo na una uhitaji nayo sana, fua kamua vizuri iweke mbele ya fan kama ni fan ya stand, kama ni zile za juu basi itandaze nguo sehemu ambapo upepo unafika vizuri itawahi kukauka.
 
bila kusahau kutumia sabuni ya kipande,maana ya unga halafu nguo ukaianikia ndani ikikauka inatoa harufu kama dagaahuwezi ivaa,na hakuna perfume inawezakata hiyo uvundo.
 
Inaonekana we jamaa nguo zako ni "Kauka nikuvae"

Eniwei ukitaka kukausha fasta chukua nguo ikunje fresh halaf mtandikie kuku anaetamia mayai, mf ukimuwekea usiku had asubuh kwa kale kajoto nguo yako(Kauka nikuvae) itakuw tayar
 
Kamua maji, kung'uta, halafu zipange kwenye godoro uzilalie hadi asubuhi utakuta zishakauka, hii mbinu tuliitumia sana tukiwa tunakojoa kitandani.
 
Hakika humu ndani ni kuzuri sana, kila swali lazima lipate jibu, unaweza ukaona swali la kipuuzi ila majibu yatakuwepo tu, na ukafahamu zaidi.
 
bila kusahau kutumia sabuni ya kipande,maana ya unga halafu nguo ukaianikia ndani ikikauka inatoa harufu kama dagaahuwezi ivaa,na hakuna perfume inawezakata hiyo uvundo.
Muhanga sio kwa hadithi hiyo😅😅😅
 
Back
Top Bottom