Katika Mazingira ya Kugawa Rasilimali Kisiasa na "Kupika Data" Kuna Haja ya Sensa?

Kingcobra

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,000
309
Wakuu,

Zipo nchi ambazo kweli zikifanya zoezi la sensa linakuwa na maana. Lakini nina mashaka na hapa kwetu. Nahisi ni kama viongozi wetu wanafanya kwa kuiga tu nchi zingine. Nasema hivi kwa sababu hata mgawanyo wa rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi hauzingatii kabisa mtawanyiko wa watu wala idadi yao katika eneo fulani. Mgawanyo wa rasilimali au faida za kiuchuni unazingatia zaidi matakwa ya kisiasa. Hali kadhalika, zikitolewa data za ukuaji wa kiuchumi wengi wetu tumekuwa na mashaka kama data hizo ni za kweli kwani mara nyingi hazioani kabisa na hali halisi mitaani kwetu na hasa vijijini. Inaonekana akina Prof. Benno Ndulu nao ni kama wanasukumwa na matakwa ya kisisa kutoa takwimu za mwenendo wa ukuaji wa uchumi ingawa nafai zao lazima zitakuwa zinawasuta. Katika hali kama hiyo, maana ya sensa kwa nchi yetu na chini ya uongozi wa magam.....a ni kama haipo ingawa matumizi ya sensa hayaishii katika maeneo hayo mawili niliyogusia.

Ni maoni yangu tu.
 
Back
Top Bottom