Katika Matajiri wetu 10 wa juu Tanzania, hakuna aliyesoma Chuo Kikuu ndani ya nchi! Uchumi wetu unategemea elimu za nje, kwanini?

Hii ndiyo negative attitude towards elimu kwa watanzania wengi. Kusoma hakuna uhusiano wowote na utajiri; usiende shule ili uwe tajiri. Utajiri unasababishwa na mambo mengine mengi tu kukiwamo vitu kama bahati, urithi, nidhamu binafsi ya mtu mwenyewe, ubunifu, na kadhalika; mambo ambayo hayana uhusiano kabisa na elimu au shule uliyosoma.
 
Habari Wadau..

Wote tumeguswa na msiba wa tajiri wetu mweusi Mr. Mengi aliyekuwa anaenda level zisizopishana sana na Watanzania weupe

Wasifu wake unaonesha hata yeye hakukanyaga chuo kikuu chetu ..

Na hapo hapo akapata akili ya kuwa tajiri na industrialist mkubwa sana...

Je, elimu yetu ipo sawa kweli?

Kwanini washika uchumi hawasomi elimu yetu
Cha msingi Fanya wewe kwanza wengne watasema kuhusu wewe
 
Hili haswa ndilo jibu sahihi, wakufunzi wetu wenyewe wana stress mpaka kwenye ukucha unategemea atoe elimu ya kumfanya mwanafunzi awe millionaire??? Mfumo wa elimu yetu ni mbovu sanaaaa, sasa kama mimi mwenyewe nimesoma kwa taabu then nikapata GPA ya kunibakisha chuoni kama tutorial then najiendeleza hadi PhD nakua senior lecturer naachaje kulamba matako ya kina Makonda ili niendelee kuishi... Hata mie Mungu akiniwezesha hiki nachokifanya now kikazidi kukua hakika watoto wangu chuo hawatasoma bongo hapa
Hahahha mtenga umenichekesha wallah
 
Maprofesa wa Tanzania ni hao kina Kabudi, Mkumbo, Mwakyembe, Dr. Bana n.k yaani hawa wanafiki na wachumia tumbo ndio wamfundishe mwanafunzi awe milionea wakati hata wao wanategemea kumsifia magufuli ili wapate kuendesha maisha yao...
Umehitimisha kila kitu , uzi ufungwe.
 
Bongo hamsomi mnakusanya vyeti tu.
Uliza mtu yeyote aliyesoma nje hasa STEM atakwambia. Tafuta walioanzia degree bongo alafu wakapiga masters au phd nje wanajua utofauti uliopo, ni mkubwa balaa.
 
Maprofesa wa Tanzania ni hao kina Kabudi, Mkumbo, Mwakyembe, Dr. Bana n.k yaani hawa wanafiki na wachumia tumbo ndio wamfundishe mwanafunzi awe milionea wakati hata wao wanategemea kumsifia magufuli ili wapate kuendesha maisha yao...

Hawa maprofesa ni watoto wa maskini kama Mengi na wamesoma Ulaya na Marekani tena kwa muda mrefu kuliko Mengi lakini si matajiri. Kwa nini? Na kwa nini raia wa huko Ulaya na Marekani waliosoma vyuo vikuu huko kwao si matajiri na kuna mabilionea wa dunia ambao hawakwenda vyuo vikuu kabisa?
 
Nina mengi ya kuchangia ila muda si rafiki mno kwangu leo hii. Nina mzazi alisoma udsm na akaenda nje kwa ajili ya masters, hio ilikua kama miaka 40 iliyopita. Alivyorudi kutoka masters, alikaa miaka 2 ndani ya shirika lililomsomesha nje, akabadilisha vitu vingi ndani ya shirika hilo na baadae akaacha Kazi. Sababu kubwa ya kuacha kazi ni aliona kua asingeweza kufika kule ambako alitaka kufika. Alianzisha kampuni yake nchini, na taratibu kampuni ikawa inafanya vizuri mno. Aliapa kuwasomesha wanae wote nje na aliweza kutimiza ndoto yake hio.

Kitu nilichojifunza nikiwa nasoma nje ni kua ile exposure tu ya nje ni zaidi ya vitu vingi sana. Ile combination ya kusoma, kufanya zile part time student jobs na mikiki mikiki ya nje inakufungua sana akili. Huko chuo nako, kama unasoma biashara, ndani ya mwaka 1, mnakua mmeshatembelewa na wafanyabishara matajiri wengi tu, Ceo's wanaolipwa milioni mia za Tanzania kwa mwezi, Real estate Moguls, owners wa biashara kubwa kubwa za kufa mtu. Hao wote wanakua invited vyuoni ili kuwapa somo na jinsi walivyotengeneza utajiri wao na kuwapa moyo kua inawezekana.
Sasa hapo mwanafunzi unaanza nawe kua na confidence ya kua kama hawa wameweza, mie kwanini Nishindwe?

Pia unajifunza kua fursa ni popote, sio lazima iwe kwenye nchi uliyozaliwa. Unaanza kufikiria in $ millionaire sio Tsh. Millionaire. Ukimaliza chuo, ile elimu, exposure, life experience, uthubutu nk inakufanya uwe unafanya mambo yako kwa speed ya 5G, kwa hio inakua ngumu sana kufeli maisha. Ndani ya miaka 10 kutoka kumaliza chuo, unakua mbali sana ( though sio wote)
 
Habari Wadau..

Wote tumeguswa na msiba wa tajiri wetu mweusi Mr. Mengi aliyekuwa anaenda level zisizopishana sana na Watanzania weupe

Wasifu wake unaonesha hata yeye hakukanyaga chuo kikuu chetu ..

Na hapo hapo akapata akili ya kuwa tajiri na industrialist mkubwa sana...

Je, elimu yetu ipo sawa kweli?

Kwanini washika uchumi hawasomi elimu yetu
Tatizo sio kukanyaga chuo kikuu cha Tanzania ama la, Suala la mtu kuwa millionaire sio la kujadiliwa kwa point ya chuo. tunao watanzania wengi tu ambao hawajakanyaga vyuo vya Tanzania na sio mamilionaire, ingekuwa kusoma huko walikosoma kina Mengi na wengine ndio sababu pekee iliyowafanya wawe matajiri basi tungekuwa na matajiri weeengi sana maana hata kwenye vyuo vyetu mfano udsm wapo watu waliosoma vyuo nje tu, tunao wanasiasa kama January wamesoma nje tu lakini si mamilionaite
 
Wapo pia waliosoma nje ya nchi mpaka ngazi ya PhD lakini wamezidiwa utajiri na watu ambao hawakusoma nje ya nchi.

Utajiri wa level ya marehemu Mengi ni suala kubwa ambalo linahitaji exposure kubwa kuhusu investment.
Na exposure ya aina hiyo sidhani kama ilikuwa rahisi kuipata hapa Tanzania katika miaka ambayo Mengi alikuwa anaji-establish.
Msingi wa elimu ya Tanzania ulikuwa ni wa kijamaa(basically kwaajili ya maslahi ya jamii na sio mtu binafsi) kwahiyo haiuwa rahisi kuimpart fikra za kijasiriamali na uwekezaji kwa waliohitimu elements za msingi kabisa katika utajiri.
Mimi naweza kuhitimisha kwamba watu waliopata fursa ya kusoma nje ya nchi kipindi hicho walikuwa na advantage ya kupata exposure namna watu wanavyobuni mawazo ya kibiashara,namna watu wanavyo endesha corporates,mfumo wa soko na hisa unaendaje,na mambo mengine kama hayo.
Lakini ni lazima tukubaliane kwamba haya mambo sio lazima yawe walifundishwa darasani,hususani wale ambao hawakusoma fani za biashara na uhasibu ila waliyaona yanaendelea katika hizo jamii walizoenda kusoma na wao wakayaleta huku.
 
Nje walifundishwa ubepari ujasiliamali ( maendeleo binafsi) elimu ya ndani wanafundisha ujamaa ( umasikini) .Mjamaa hawezi akawa tajiri,wajamaa wanawachukia matajiri.
 
Maprofesa wa Tanzania ni hao kina Kabudi, Mkumbo, Mwakyembe, Dr. Bana n.k yaani hawa wanafiki na wachumia tumbo ndio wamfundishe mwanafunzi awe milionea wakati hata wao wanategemea kumsifia magufuli ili wapate kuendesha maisha yao...
Wamsifia TLissu ambaye kafundishwa na Kabudi !?
 
Maprofesa wa Tanzania ni hao kina Kabudi, Mkumbo, Mwakyembe, Dr. Bana n.k yaani hawa wanafiki na wachumia tumbo ndio wamfundishe mwanafunzi awe milionea wakati hata wao wanategemea kumsifia magufuli ili wapate kuendesha maisha yao...
Akina Lema, Mdee, Mnyika, na Sugu wao wanachumia mattako !?
 
Back
Top Bottom