Katika maslahi mapana ya taifa ni bora Serikali ikawekeza kwenye rasilimali watu au kwenye mali (miradi) za/ya Serikali?

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
Swali langu limetokana na awamu zote za serikali za Tanzania kwanzia Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya sasa.

Serikali zetu zimeshindwa kuwekeza kwenye wananchi wake, hususa kwenye tasnia ya elimu (Aina ya elimu, mitahara ya elimu, mifumo ya elimu, miundo mbinu ya elimu).

Hali hii kupelekea kuzalisha nguvu kazi kubwa yenye kujua kusoma na kuandika, kuzalisha wasomi wasio weza katika ushindani wa ajira hata tu ule wa kikanda kama ule Afrika Mashariki.

Graduate wa Kitanzania huwezi mfananisha na graduate wa Kikenya, hata kwenye ushindani wa kiajiri wa Kitanzania wanaoweza kushindana na Wakenya ni asilimia ndogo sana.

Serikali ya awamu ya tano imelenga na kuelekeza nguvu kubwa kwenye miundo mbinu, huku ikiifanya elimu kuwa bure. Jambo hili lina faida na hasara pia.

Hasara ni kuwa tunazidi ididmiza elimu yetu, maana serikali yetu haina uchumi wa kutoa elimu bora bure. Sana sana itaweza kutoa bora elimu, sasa bora elimu katika Karne hi ya 21 haitakiwi. Pili, hasara nyingine ni serikali inazidi kujiingiza kwenye matumizi makubwa ya fedha za ki-serikali.

Faida ni kuwa serikali inajipatia Watanzania wa shule ya msingi na sekondari wanaojua kusoma na kuandika.

Sasa ni bora serikali ikazalisha Watanzania 1,000,000 ambao wapo competent na wamepata elimu bora kwenye tasnia mbali mbali kuliko kuzalisha Watanzania 40,000,000 wanaojua kusoma na kuandika?

Sera ya elimu haikufikiriwa kwa upana sana, ilikuwa ni sera ya kisiasa tokana na ugumu wa uchaguzi wa mwaka 2015.

Maendeleo ya taifa lolote duniani, ni Aina ya wananchi walio nchini. Yani kiufupi serikali ikishindwa kuandaa wananchi wake kwenye fikra na kielimu basi hilo taifa litapata matokeo ya kiuchumi tokana na aina ya wananchi ilio waandaa.

Serikali za Tanzania zinapaswa kuwekeza nguvu nyingi na fedha nyingi kwenye tasnia ya elimu, afya na ndio vingine vifuate.

Faida za standard gauge au Stigler's Gorge si pana Kama ambavyo zile zingepatikana baada ya uboreshaji wa elimu (Aina ya elimu, mitahara ya elimu, mifumo ya elimu, miundo mbinu ya elimu).

Taifa letu ujinga, ufukara, umaskini na afya ndio changamoto sana na ni kikwazo kwa taifa hili kushindwa fikia malengo ya uchumi wa kati.

Watanzania wakielimika, wanaweza jenga standard gauge, Stigler's Gorge, fly overs, air port na kuanzisha viwanda.

Watanzania wakielimika wanaweza kuunda mifumo Bora ya kiutawala ya ki-serikali, pia hata wakielimika wanaweza unda katiba Bora.

Ni kheri umpatie mtu fikra na akili za kutafuta mali au umpatie Mali?
 
wilson kaiser senior,

Umesema kweli kabisa, leo tunashangilia maendeleo ya ujenzi wa vitu mfano standard gauge, MHEP na barabara ambavyo kiuhalisia hatuna wataalamu wa kujenga au uwezo wa kujenga sisi wenyewe hatuna hivyo tunalazimika kuwapa kazi makampuni kutoka nje. Ni sawa lakini je tumejitathmini kama nchi ni lini tutaweza kufanya haya sisi wenyewe ili hiyo dhana ya maendeleo iwe imetimilika maana maendeleo twapaswa kujiletea wenyewe.

Utakuta watu wetu sisi kwenye miradi hiyo ni daraja la kati kabisa maexpert wanatoka nje hapo utaalamu sio wetu. Je tangu nchi kupata uhuru na sasa miaka zaidi ya sitini(60) mfumo huu wa elimu umetusaidia kupata wataalamu tunaowahitaji? Kwa kiwango gani? Kama taifa kuna haja sasa ya kuwa na maono ya kimabadiliko.

Nimewahi sikia mara kadhaa, tukijisemea na viongozi wetu kuwa mataifa kadhaa ambayo sasa yako kwenye hatua nzuri ya maendeleo kama China, India, Singapore, Taiwan, n.k miaka 50 nyuma tulikuwa nao kwenye level moja ya uchumi na maendeleo lakini leo wenzetu wametuacha hatua nyingi sana mbele yetu.

Siri kubwa ni kuwa waliwekeza sana katika kupata maarifa(elimu); walibadili mifumo yao ya elimu ili iweze kuwakomboa na kweli leo nchi hizo zina wataalamu wao katika tasnia karibu zote na wamekuwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa ambazo hata kwetu ni watumiaji wakubwa. Sasa tujiulize sisi tunazalisha nini ambacho soko la dunia au hata Afrika tu humu wanatumia? Achana na raw goods. Kiukweli bado tuna safari ndefu kama taifa na hii inahitaji mapinduzi makubwa ya kifikra kwanza.

Tuache kuchagua viongozi wasio na dira ya kuleta mabadiliko chanya tena kuanzia katika mifumo ya uendeshaji nchi. Tusichague viongozi kwa mazoea na kujuana au itikadi bali tuchague wenye uthubutu na malengo thabiti. Sio wenye hadaa za kisiasa bali watendaji kwelikweli wasiohitaji kutangaza wamefanya nini bali waliyoyafanya ndio yaonekane bayana.

Hakuna haja ya kuwekeza pesa za walipa kodi et kuandaa vipindi kuonesha tumetekeleza, hapana hayo ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi yaache maendeleo yenyewe yajioneshe maana maendeleo hayajifichi ndugu zangu.
 
Wapo wananchi wana uwezo wa kusaka elimu bora ndani na nje lakini wanasubiri miujiza ya serikali zetu hizi. Hata hiyo Kenya haina Elimu bora kivile, lakini kwa kulitambua hilo wanasaka elimu bora duniani kote kwa mtindo wao maarufu wa harambee.

Baba ana Prado, Mama Cruiser, watoto wao kila mmoja ana Harrier, Send off ya binti yake katoa milioni 150, unafikiri watu hao wakiamua kusaka elimu bora iliyo nafuu world wide kwa watoto wao wanashindwa?
 
Back
Top Bottom