Katika mapenzi usikubali ‘kuuziwa mbuzi kwenye gunia’


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
Tatizo ambalo limekuwa likiwakuta wapenzi wengi wanaoanzisha uhusiano wa kimapenzi wenye mwelekeo wa maisha ya ndoa ni kuingizwa ‘mkenge’ kwa kufichwa baadhi ya tabia mbaya na wapenzi wao... Wapenzi wanaoficha tabia wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuteka mapenzi ya watu, lakini baadaye wakishafanisha azma yao hujiachia na kuanza kuwatesa wenzao.

“Sikujua kabisa kama ana tabia hizi, ningetambua mapema kama ni mhuni nisingekubali kuoana naye.”
Uchunguzi unaonyesha kuwa wanandoa wengi mpaka sasa wanajuta kufunga ndoa na wapenzi wao na kwamba kama wangetambua tabia za wenza wao mapema wasingekubali kufunga ndoa.

Inawezekana hata wewe unayesoma makala haya unajuta kiasi cha kulalamika mwenzako alivyobadilika tabia tofauti na mwanzo ulivyoanza kupendana naye. Hebu fuatilia dondoo hizi zikifuatwa zinaweza kuwasaidia watu wasijiingeze kwenye uhusiano usiyo sahihi.

MPE UHURU WA KUTOSHA
Watu wengi wanapoanzisha uhusiano huwabana sana wapenzi wao kwa kuwapekulia simu, kuwachunga watokapo na waingiapo, jambo ambalo huwafanya wahusika kujilinda sana wakiamini wanafuatiliwa.

Ndugu yangu usimbane mpenzi wako, mwache huru, atembee atakavyo na awasiliane na amtakaye, wewe kaa nyuma yake ukimchunguza bila mwenyewe kujua. “Mke/mume wangu hajali mambo haya” Hujali kumbe unamteka mwisho wa yote utamnasa.

MPE MAJUKUMU
Ukisha mchagua umpendaye, huwezi kutambua uwezo wake mpaka umpe majukumu ya kufanya. Kwa mfano mtume akalipie maji, umeme au mwagize asimamie jambo fulani la maendeleo.
Ukishafanya hivyo kaa kando mwangalie, anavyoiba chenji, anavyopunguza gharama bila kukushirikisha, lakini baadaye muulize, utashangaa alivyotibua mambo akidhani wewe si mtu wa kujali sana, kumbe ulikuwa umemtega na hatimaye umemnasa.

MUWEKE KWENYE WAKATI MGUMU
Njia nyingine ya kumnasa anayekufichia makucha ni kumuweka katika wakati mgumu. Wanasema rafiki wa kweli hujulikana kwa dhiki. Tengeneza dhiki kwa makusudi na kuzitekeleza.

Akikuambia naomba unitumie vocha au ninunulie nguo, mwambie sina pesa, halafu uone kama atakuwa na kiwango kile kile cha mapenzi. Siku hizi kuna wapenzi wengi wa pesa na mishahara, wakiona hakuna vitu hivyo wanaachia ngazi, dawa yao ni kuwatega kwa kuwanyima hata kama mifuko imejaa noti.

TUMIA WATU
Katika hali ya kawaida, majirani na marafiki wanawatambua zaidi wapenzi wetu kuliko jinsi tunavyowatamba sisi. Inawezekana kabisa mpenzi wako akawa mtakatifu unapokuwepo lakini ukiondoka anajiachia ile mbaya, hivyo ili kujua tabia zake waulize rafiki na jirani zako watakusaidia kumtambua mpenzi wako.

ANGALIA ANAVYOWATENDEA WENGINE
Wapenzi wengi wanapokuwa wamepata wapenzi hutazama wanavyotendewa wao na kudhani inatosha. Mtu muungwana huwatendea pia wengine mema. “Aa, mama naye kanichosha kila siku anataka pesa.”
Hebu sikia kauli hii, kama mtu analalamika kuchoshwa na mama mzazi, ndugu zake, rafiki yake itakuwaje kwako? Amka na kutambua kuwa anakufichia makucha na ipo siku atakubadilikia hata wewe na kukutesa. Kwa waliodanganywa tayari wiki ijayo tutaangali somo la UFANYE NINI UNAPOGUNDUA ULIYEMPA PENZI HAKUFAI?
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
Ni mara nyingi sana tumekuwa tukisikia mwanamke anaolewa leo lakini baada ya siku chache tu anaanza kulia na kudai kuwa, eti mwanaume aliyemuoa hafai. Sababu zaweza kuwa ni mbabe, hajali na tabia nyingine zisizovumilika.

Ukijaribu kufuatilia utabaini kuwa, mwanamke huyo hakuwa makini katika kuchunguza kama mwanaume huyo anastahili kuwa mumewe wa maisha au laa. Matokeo yake sasa akawa umejijengea mazingira ya kuuziwa mbuzi kwenye gunia kwa kukubali kuolewa na mwanaume asiye na vigezo.

Hali hiyo hutokea pia kwa wanaume. Wapo wanaoanzisha uhusiano wa kimapenzi wenye mwelekeo wa maisha ya milele lakini wanashindwa kuwa makini na hatimaye kujikuta wanafichwa baadhi ya tabia na wapenzi, mwisho wa siku baada ya utambulisho au ndoa, ndiyo wanakuja kubaini mwanamke aliyemchagua hakuwa sahihi.

Wiki hii nianze na wanaume. Ili mwanaume aepukane na tatizo la kuuziwa mbuzi kwenye gunia ni vyema siku za kwanza za uhusiano kabla hajamtambulisha kwa ndugu au kumuoa kabisa akatumia mbinu zifuatazo ili kuibua tabia mbaya ambazo mpenzi wake anaweza kumficha kwa lengo la kummiliki.

Wanawake wanaoficha makucha huwa na nidhamu ya woga, mara zote husoma tabia za wapenzi wao ili kuhakikisha maovu yao hayatokezi kwenye uso wa mwanaume anayemuwinda. Hivyo ni jukumu la mwanaume mchunguzi kutoa uhuru wa kutosha kwa mpenzi wake wa kwenda na kufanya atakavyo. Hii itamfanya mwanamke akose umakini na kudhani mwanaume aliyempata si mtu wa kujali mambo. Atajiachia na uwezekano wa kumnasa utakuwa mkubwa.

Pamoja na hilo jambo lingine ni kumpa majukumu muhimu ya kifamilia, kwa mfano ahudumie wagonjwa, asimamie watoto, atunze pesa za matumizi ya kutwa na zile za wiki na atembelee ndugu wa familia ya mume.

Mambo haya yote asiulizwe matokeo kwani anaweza kudanganya au kujenga mianya ya kujitetea pale alipokosa alama za kukubalika, badala yake watu anaowahudumia wamzungumzie na matokeo yajioneshe yenyewe.

Mbinu nyingine ni kumuweka katika wakati mgumu wa kimaisha. Kama wengi wetu tujuavyo shida ndiyo kitu cha kwanza cha kupima uaminifu na ustamilivu wa mtu. Hivyo kabla ya kumpisha umpendaye lazima umtumikishe katika hili ili kujua utayari wake wa kukabili mabadiliko ya maisha ambayo kwa dunia ya leo si ya kuepuka kwa kiwango cha juu.

Pamoja na uhuru niliousema hapo juu, ni wajibu wa mwanaume anayetaka kuibua makucha ya mpenzi wake kufanya uvamizi wa kuhoji kile kilichoendeshwa na mpenzi wake.

Kwa mfano kama alimpatia pesa za matumizi aziweke amshtukize kwa kumwambia akupatie kiasi cha matumizi ya siku moja, kama si mwaminifu atakuwa alishazitumia. Ni vema pia kuepuka huduma na vyakula unavyowekewa wewe peke yako, mara nyingine shiriki na wengine ili kujua kama mpenzi wako anajali usawa au ni mbaguzi.

Kimsingi haya ni kwa uchache, lakini kuna mbinu nyingi zaidi za kumbaini mpenzi anayetaka kukuingiza mkenge. Hivyo basi ni muhimu kwa mwanaume ambaye ana mpenzi na angependa amtambulishe kwao azingatie haya.

Vinginevyo anaweza kumpeleka kwa wazazi mwanamke ambaye hana tabia njema na baadaye akalazimika kurudi kuiambia familia na marafiki zake kwamba amemwacha kwa sababu hakuwa mtu makini. Ni jambo baya sana kuwatambulisha wazazi mchumba kisha kumtema.

Ni hayo tu kwa leo, tuonane tena wiki ijayo. Kwa ushauri maoni kama kawaida wasiliana nami kwa simu namba 0716007373 au baruapepe:zekaima@yahoo.com
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
ANABADILIKA
Mwanaume ambaye ana malengo ya kuoa hubadilika kitabia. Muda mwingi hutaka kuonekana mtu mzima mwenye sifa nzuri. Hatakuwa mtu wa kulewa kupita kiasi na kutapanya mali na wanawake wengine. Tabia zake mbaya za zamani ataziacha

Kisa cha mabadiliko hayo kinatajwa na wataalamu wa masuala ya ndoa kuwa ni pamoja na kumshawishi mwanamke aliyemchagua aitikie mwito wa kuwa pamoja katika maisha. Lakini pia ni kuwapa kielelezo chema ndungu au wazazi wake wamuunge mkono katika harakati zake za kuoa.

ATAONGEZA JITIHADA ZA KUJITEGEMEA
Mara nyingi wanaume walio makini na tayari kufunga ndoa, wanahitaji kuwa na kipato cha kutosha kuweza kuwahudumia wake zao na familia ambazo watakuwa nazo hapo baadaye hivyo wanajitahidi kutafuta njia za kupandisha hali yao kiuchumi.

Kama ni muajriwa anaweza akaanza kutafuta miradi mingine nje ya kazi yake ili imsaidie kuongeza kipato cha kujikimu na hali ya maisha. Kama alikuwa anaishi na wazazi atapanga chumba na ataanza kujitemea.

ANAGUNDUA KWAMBA ANAHITAJI KUITWA BABA
Njia nyingine ya kugundua mwanaume aliye tayari kwa ndoa ni pale unapotembea naye barabarani, anawafurahia watoto mnaokutana nao njiani na mara kwa mara ataonekana kukueleza jinsi atakavyowafanyia watoto wake mara baada ya kuwapata hapo baadaye.

Mwanaume huyo pia huwa na tabia ya kufurahia maisha ya ndoa ya watu wengine yaani anapomuona mke na mume wakiwa na mtoto wao basi hutamani sana mngekuwa nyinyi. Mnapotoka hukuita mke wake!

NI RAFIKI LAKINI NI MUME KAMILI
Mwanaume anayetaka kuoa anakuwa ni rafiki yako tu kwa sababu hamjafunga ndoa, lakini matendo anayokufanyia hayana tofauti na yale ya mtu kwa mkewe. Kwa mfano kupanga mipango ya baadaye ya maisha yenu, kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake. Huwa na hamu ya kutaka kujua matatizo yako na kukusaidia na wakati mwingine kukushirikisha katika matatizo yanayomkabili.

Mara nyingi huwa makini sana kutambua mabadiliko ya mapenzi na hutoa uhuru na kukumilikisha vitu vyake kwa mfano kukupa funguo za chumba au nyumba yake. Hupenda kutoa misaada ya kumwendeleza mpenzi wake kimaisha, kama kumsomesha au kumtafutia kazi.

HUFURAHIA UKARIBU
Mwanaume aliyetayari kuoa hupenda kuwa karibu na mpenzi wake na asilimia kubwa ya mazungumzo yake atayaelekeza katika maisha si ngono. Atajitoa kusaidia ndugu wa mke kila linapokuja tatizo. Na atalalamika anapotengwa na familia ya mchumba wake.

Sifa za mwanaume anayekuchezea
ANAKWEPA MAZUNGUMZO YA NDOA
Haonyeshi kufurahi unapoanzisha mazungumzo kuhusu suala la kufunga ndoa na wala hapendi kuzungumzia hilo. Wakati mwingine hata kukutambulisha kwa ndugu zake au rafiki inakuwa shida.

ANAGHARAMIA ANASA KULIKO MAMBO MUHIMU
Anakuwa ni mtu wa kukununulia mapambo ya gharama na vitu vyote vya anasa, lakini hana mawazo ya kuzungumzia maisha yenu ya baadaye wala kukununulia vitu ambavyo vitakuwa na manufaa katika maisha ya mbeleni. Haangalii masuala ya elimu wala kukutafutia mtaji au kazi.

HAJALI MACHOZI YAKO
Unaweza kugundua ni jinsi gani hana mpango mzuri na maisha yako, kwani hata anapokuudhi anakuwa hajali wala haumizwi na machozi yako, ni busara kuwa makini kwa sababu huyo atakuwa ni mtu wa kukupa maumivu wakati wote.

HAJITOKEZI HADHARANI
Mwanaume ambaye malengo yake ni kukuchezea huwa hataki mapenzi yenu yajulikane hadharani atakuwa mtu wa kutaka mambo yaende kwa siri. Hajitambulishi kwa rafiki wala kwa ndugu zako. Hatoi nafasi ya wewe kumtembelea nyumbani kwake.

Tukutane wiki ijayo leo tunatia nanga hapa!
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
Jamani, mapenzi yana nafasi kubwa sana katika maisha ya binadamu. Ndio maana hakuna anayeweza kuishi bila kuwa na mpenzi na kama yupo basi atakuwa na matatizo. Na ili kujua kwamba kweli mapenzi yana umuhimu sana, yanapokosekana wapo ambao huchanganyikiwa kabisa na kushindwa kutimiza majukumu yao ya kila siku.

Niseme tu kwamba, maisha bila mapenzi lazima yatakuwa na mapungufu hivyo basi kwa wale waliobahatika kupendwa, wajitahidi kulilinda penzi lao kwa hali mali ili mwisho wa siku waweze kuishi maisha yenye furaha.

Mpenzi msomaji, wiki hii nataka kuzungumzia mada ambayo itawagusa moja kwa moja wanawake wenye makuzi ambao hulazimisha kufanyiwa mambo makubwa bila kujali kama wapenzi wao wana uwezo ama laa.

Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba, yaweza kuwa kero kwa wanaume kutokanana na tamaa zao. Kwa mfano, kila wikiendi utamsikia akimwambia mpenzi wake” Leo tunakwenda wapi dear” Yaani yeye bila kutolewa ‘out’ siku siku za wikiendi hajisikii raha.

Akimuona rafiki yake kanunua simu ya bei mbaya na yeye utamsikia akisema “Na mimi ninunulie simu kama ya fulani”. Hata kama simu anayo lakini kwasababu tu kaona kazidiwa kete na mashoga zake, na yeye anataka anunuliwe.

Ukienda naye hotelini anaagiza chakula cha bei mbaya. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na asipotekelezewa hayo anayoyataka, utamkuta anachukia na anaweza kufikia hatua ya kupunguza mapenzi.

Kwa mwanamke mwenye tabia hizi kama hajaolewa ni vigumu sana kuolewa na mwanaume aliye naye na kama yuko ndani ya ndoa, ndoa yake haiwezi kudumu.
Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.

Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema “ Unataka nikununulie simu ya aina gani mke wangu/mpenzi wangu? Wiki hii nataka nikutoe ‘out’, utafurahi kama nitakupeleka wapi? Hapo ndipo mwanamke atakuwa na nafasi ya kusema “mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.

Kama ulikuwa hujui, wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa au wale walio nao katika ndoa chochote watakachohitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanaume.

Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho ukiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.

Ninaposema hayo simaanishi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! Kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo, mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.

Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana uwezekano haupo. Na nikudokeze tu kwamba, ukimweleza mpenzi wako shida yako inayohitaji pesa nyingi na akawa hana uwezo wa kukusaidia, huwa anaumia sana na anaweza kujenga akilini mwake kwamba unaweza kumsaliti endapo utampata mwanaume mwenye uwezo.

Ili kuliepusha hilo, msome mpenzi/ mume wako kabla ya kumwambia shida yako, ukiona shida uliyonayo iko nje ya uwezo wake, tumia njia nyingine ya kumshirikisha na si kwa kumuomba moja kwa moja akusaidie. Naamini kwa kufanya hivyo angalau mnaweza kusonga.

Ni hayo tu kwa leo, kwa mada nyingine kali ungana nami tena wiki ijayo. Kwa ushauri au maoni, wasiliana nami kwa simu namba 0716007373 au baruapepe:zekaima@yahoo.com
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
Wiki hii msomaji wangu nataka kuzungumzia mada ambayo inaelezea uhalisia wa maisha ya kimapenzi ya huko mtaani. Imekuwa ni kitu cha kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wenzake kwa kusema; “Mimi nina kibuzi changu bwana kila nikihitaji pesa ananipatia, yaani namchuna kama sina akili nzuri”

Si hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kuwaombaomba pesa hata kama wanao uwezo wa kuzipata kama wakijishughulisha.

Unaweza kumsikia mwanaume akisema, “Aah! Yule demu kazimika ile mbaya na mapigo yangu, kila ninachotaka ananipa kwani anajua akininyima namtosa”.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano wowote na pesa, ukiona mpenzi wako anaweka pesa mbele na ukishindwa kumpatiliza anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini. Hakupendi bali anakutumia kama kitega uchumi chake.

Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo fanya hivyo na kama huna mueleze kwa njia ya unyenyekevu kwamba huna kisha muangalie jinsia mnavyoweza kusaidiana katika kutatua tatizo linalomkabili.

Itakuwa sio busara kama utakuwa na tatizo linalohitaji pesa ili kulitatua lakini ukaona ukimweleza mpenzi wako ataona kwamba unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana. Hili ni kwa pande zote mbili.
Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe.

Yaani sasa hivi umemuomba mpenzi wako pesa ya kununulia vocha, hajakaa vizuri umemtaka akupe pesa ukanunue kitu fulani, bila kujali kama wakati huo mpenzi wako ana fedha au hana. Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchukulia kwamba umekaa kibiashara kweli?

Ifike wakati tuone wazi kwamba, mapenzi na pesa ni vitu viwili tofauti kabisa na ndio maana mapenzi yanaweza kuendelea kuwepo hata kama pesa haipo. Wapenzi wangapi leo hii uwezo wao kipesa ni mdogo sana lakini bado wanaoneshana mapenzi ya dhati?

Lakini pia ni wanawake wangapi wako katika uhusiano wa kimapenzi na wanaume wenye uwezo kipesa lakini bado wanaishi maisha yasio na furaha wala amani kiasi cha kujuta kuingia katika uhusiano na watu hao?

Mimi niseme kitu kimoja kwamba, kwa maisha ya sasa wapo watu wanaoingia katika uhusiano wa kimapenzi kwa gia ya biashara. Msichana anajifanya kumpenda sana mwanaume fulani kwasababu tu ameona anao uwezo kifedha na mwanaume asiposhitukia, anaweza kuhisi amepata bahati ya kupendwa kwa dhati kumbe kilichopendwa kwake ni pochi yake iliyonona.

Katika hili nishauri kwamba, unapoingia katika uhusiano wa kimapenzi na mtu, unalo jukumu la kufanya uchunguzi ili kubaini kama umeingia katika penzi la kweli ama laa! Miongoni mwa dalili za mpenzi asiye na penzi la dhati kwako ni kuweka pesa mbele kisha mapenzi yanafuata.

Ni hayo tu kwa leo, tuonane tena wiki ijayo kwa mada nyingine. Kwa ushauri au maoni nicheki kwenye simu namba 0716-007373 au email:zekaima@yahoo.com
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita utakumbuka niliandika mada iliyokuwa inazungumzia dalili tano za mpenzi anayekutafutia sababu ili muachane. Ni mada iliyoonekana kuwagusa wengi kwani nimepokea simu nyingi pamoja na ujumbe mfupi wa maneno wa kumwaga kutoka kwa watu mbalimbali wakiniunga mkono katika kile nilichokiandika.

Mmoja wapo ni dada Joyce wa Chuo Kikuu Dodoma ambaye baada ya kusoma makala hiyo alilazimika kunipigia na tukaongea kwa takribani saa mbili akinipa baadhi ya changamoto ambazo naamini zitanisaidia katika kuandika makala zenye mguso zaidi katika jamii. Nakushukuru sana dada Joyce.

Nikirudi sasa katika kile nilichodhamiria kukiandika, leo nataka kuzungumzia mapenzi na pesa na kuonesha ni namna gani vitu hivi viwili havina uhusiano wa moja kwa moja. Ni mada inayoeleza uhalisia wa maisha ya kimapenzi ya huko mtaani ambako imekuwa ni kitu cha kawaida kumsikia mtu akisema, amemuacha au ameachwa na mpenzi wake kwasababu ya pesa.

Katika sehemu za mjini na hata baadhi ya vijiji kuna wale mabinti ambao tunawaita wasanii, yaani wao hawajui kupenda, ukiwa na pesa ni wako ukiishiwa na mapenzi yanakwenda likizo. Si kitu cha ajabu pia kumsikia msichana akitamba mbele za wenzake kwa kusema kuwa, ana buzi lake ambalo analichuna ile mbaya.

Hilo halipo kwa wanawake tu, wapo wanaume pia ambao nao hupenda wanawake wanaotokea kwenye familia bora au mijimama yenye uwezo kipesa ‘Mashugamami’. Unaweza kumsikia mwanaume akisema, “Aah! Yule mwanamke kanizimikia ile mbaya, kadata na mapigo yangu kiasi kwamba kila ninachotaka ananipa, anajua asiponitimizia nitamtosa.

Huo ndio uhalisia wa mapenzi ya sasa. Wengi wanaingia katika uhusiano na watu ambao wanaamini kwa namna moja ama nyingine watanufaika. Tunachotakiwa kujiuliza ni kwamba, hivi mapenzi na pesa wapi na wapi? Kuna uhusiano gani wa moja kwa moja kati ya vitu hivi viwili? Ni kweli kwamba bila pesa mapenzi hamna? Mbona mababu zetu walikuwa wakipendana kwa dhati lakini kitu pesa hakikuwepo? Ndo tuseme ukiwa huna pesa hustahili kupendwa? Tunaenda wapi jamani! Mapenzi ya kweli yale ya kutoka moyoni yamekwenda wapi?

Yaani inafika wakati mwanaume akimtongoza mwanamke hata kama uwezo wake kipesa uko chini lakini atajifanyisha kwamba mambo yake ni supa ili tu alazimishe kupendwa. Kimsingi mapenzi ya kweli hayaangalii mtu ana pesa kiasi gani au ni mzuri wa vipi. Mapenzi ya kweli yanatoka moyoni lakini cha kushangaza sasa siku hizi yamekuwa adimu sana.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, mapenzi ya dhati hayana uhusiano wowote na pesa, ukiona mpenzi wako anaweka pesa mbele na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha.

Sipingi suala la wapenzi kusaidiana, mtu wako akiwa na shida akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna mueleze kwamba huna kisha muangalie jinsi gani mnaweza kusaidiana katika kutatua tatizo linalomkabili.
Itakuwa sio busara kama utakuwa na tatizo linalohitaji pesa ili kulitatua lakini ukaona kwamba ukimweleza mpenzi wako ataona umempendea pesa zake na kwamba unamchuna.

Asikudanyanye mtu, wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana na hili ni kwa pande zote mbili. Kinachokera ni mmoja kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta mtu mwenyewe anahitaji pesa kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi ameomba atumiwe vocha, hajakaa vizuri amepiga mzinga wa pesa. Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka?

Sasa basi, yawezekana wewe unayesoma makala haya umetokea kuingia katika uhusiano na mtu ambaye unampenda sana lakini tatizo anahusudu sana pesa. Mwisho wa siku mtu kama huyu hafai kuwa naye lakini kabla hujamuacha, unaweza kwanza kujaribu kutumia njia zifuatazo ili kukabiliana naye, ikishindikana sasa utakuwa huna budi kumtosa.

Kwanza, kama huna pesa wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana pesa au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi.

Pili, jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake anafanya kazi. Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna pesa zinavyokuwa hazitoshi na akaweza kubana matumizi.

Tatu, kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa pesa kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa wewe unazo.

Unachotakiwa kufanya mapema ni kudhibiti matumizi yako hata kama pesa zinakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati, usijidai mambo supa kumbe ni kapuku tu.

Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi ya siku hizi yamejaa usanii wa hali ya juu, unaweza kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mtu akakuonesha kwamba anakupenda kwa dhati na kamwe hawezi kukusaliti lakini kumbe katika uhalisia hamna kitu.Yaani ni full kujifanyisha.

Katika mazingira hayo sasa, wewe ambaye unayajali maisha yako una kila sababu ya kuwa makini sana na kila atakayekuambia kwamba anakupenda. Wapo wanaume ambao wanatokewa na wanawake na kuambiwa wanapendwa lakini ukijaribu kuangalia unakuta kwamba msichana anamwambia mvulana anampenda kwa kuwa ameona kitu flani, ameona jamaa anafanya kazi na mwisho wa mwezi uhakika!

Kwanini nasema hivyo, nataka wewe uliye katika uhusiano usijidanganye na kusema mpenzi wako anakupenda kwa asilimia zote. Yawezekana wala hakupendi kama unavyofikiria bali kuna sababu inayomlazimu akupende. Mchunguze unaweza kubaini ninachokisema.

Kwa leo naomba niishie hapo, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine kali zaidi. Kwa ushauri au maoni kama kawaida wasiliana nami kwa simu namba 0716007373 au baruapepe:zekaima@yahoo.com
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
Nina imani kwamba umzima na mambo yako yanakunyookea huku ukiyafurahia maisha yako ya kimapenzi na yule umpendaye.

Kikubwa ambacho nimekuwa nikisisitiza hasa katika dunia hii ya sasa, ni watu kujitahidi kuwa na mapenzi ya kweli dhidi ya wapenzi wao na kuondokana na tamaa zisizokuwa na msingi.

Nasema hivyo kwasababu, magonjwa ni mengi sana kiasi kwamba kama hutatulia na mpenzi wako mmoja na kuangalia ni jinsi gani mnaweza kuishi maisha yenu kwa furaha, kubaliana na mimi tu kwamba, maisha yako yatakuwa ni mafupi.
Ukimwi uko kila pembe, warembo na mabrazameni unaowaona huko mtaani wote wameathirika ambaye yuko salama ni wewe tu na mpenzi wako. Kwa maana hiyo, tulia na mpenzi wako na ridhika na kile unachokipata kutoka kwake.

Mpenzi msomaji wangu, kuna katabia ambako nimekabaini nimeona nitakuwa sijafanya busara kama nitaamua kukanyamazia. Ni hii tabia ya baadhi ya watu wanapobaini kuwa wapenzi wao wana vijisenti, hubweteka na kujigeuza tegemezi kwao. Hii ipo kwa jinsia zote si wanaume wala wanawake.

Si ajabu leo hii ukamsikia mwanamke akilalamika kuwa, jamaa yake amekuwa akimpiga mzinga kila siku tena wengine wanatumia nguvu. Wapo wanaume ambao wanalishwa, wanavalishwa, wamepangishiwa vyumba na wapenzi wao na hata kupewa fedha za matumizi. Hao wapo hasa sehemu za mijini.

Lakini leo nataka kuwazungumzia wanawake ambao wamegeuka kuwa kero kwa wapenzi wao kutokana na tabia ya kila wakati kuomba wasaidiwe na wapenzi wao bila kujali kwamba hali ya kifedha inaruhusu ama laa.

Sote tunajua kwamba, asilimia kubwa ya wanawake wanawategemea wapenzi wao katika mambo fulani yanayohitaji pesa. Achilia mbali wale ambao wana kazi licha ya kwamba nao kuna wakati wanaomba wasaidiwe. Lakini sana kuna wengine wanaboa bwana katika hili tuseme tu ukweli. Unaweza kusikia msichana akimtumia sms hii mpenzi wake:

“Dear naomba leo ukija uniletee choculate baadaye si utanipeleka steers? Nimekumiss sana” Kabla hujajibu anakuunganishia “samahani nilitaka kusahau naomba unitumie vocha nataka kuwasiliana na mama” Unamaliza kuitikia kwa unyonge anahitimisha “uwahi mpenzi tutoke”

Msichana wa namna hii ndiye ninayetaka kumzungumzia leo katika safu hii. Wapo baadhi ya wanaume hukacha kuonana na wapenzi wao kwa kudanganya kuwa wamesafiri, wako bize na kazi, kumbe hakuna lolote, wanakwepa kupigwa mzinga

Mambo hayo yapo sana, karibu wanaume wengi wanakabiliana nayo, wawe wameoa au wale ambao wana wapenzi tu. Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna baadhi ya wanaume wanapoteza mahaba kwa wake zao kwa sababu ya kubanwa katika suala zima la matumizi. Wengine huamua kutoa talaka au kusitisha uhusiano, si kwa sababu hawapendi bali wamezidiwa na utegemezi wa wale wanaowapenda.
Labda nikupe tu mbinu kadhaa zinazoweza kukusaidia wewe mwanaume ambaye mpenzi wako amezidi kukuchuna.

Wakati mwingine mwambie SINA
Wapo wanaume ambao hawajui kukataa kila wanachoombwa wanatoa, eti wanaona aibu kusema SINA! Akiombwa vocha analeta, kuku, kila kitu, hata kama hana fedha atakopa!

Lakini pamoja na ukarimu huo mazingira yanayojengeka kwa mwanamke ni ya tofauti ambayo yatakufanya siku huna kitu unyimwe penzi au wewe mwenyewe ujifanye umesafiri. Hili halitakiwi hata kama unazo wakati mwingine mwambie huna!

Kuwa muwazi
Inashangaza baadhi ya wanaume huongopea wenzao kwa kuwaambia wana mali hii na ile wakati ni waongo. Ni makosa kufanya hivyo sema ukweli...Itaendelea wiki ijayo, Kwa maoni 0713070116

Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana pesa au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi.

Naye akusaidie wakati mwingine
Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wake zao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mkewe ana kazi yake. Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna pesa zinavyokuwa hazitoshi na akaweza kubana matumizi.

Usifuje pesa
Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa pesa kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa wewe unazo.
Unachotakiwa mapema ni kudhibiti matumizi yako hata kama pesa zinakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.

Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, mapenzi ni kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe ukiwa na tatizo akusaidie. Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kere. Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo upukana na tabia hiyo.
Niishie hapo kwa leo, tuonane tena wiki ijao kwa mada nyingine lakini kwa ushauri zaidi unaweza kunicheki kwenye namba 0713070116 au email:zekaima@yahoo.com
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
Kama wewe ni mmoja wa wadau wa safu hii, utakumbuka wiki iliyopita nilianza kuzungumzia mada hiyo hapo juu. Jinsi ya kuishi na mpenzi anayependa kukuchuna kila mara. Ni mada inayoeleza uhalisia wa maisha ya kimapenzi ya huko mtaani ambapo imekuwa ni kitu cha kawaida kumsikia msichana akitamba mbele za wasichana wenzake kwa kusema “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nitakitosa yaani nakichuna kama sina akili nzuri”

Si hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kutegemea kupewa kila kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo wa kuvipata vitu hivyo kama watajishughulisha.

Unaweza kumsikia mwanaume akisema, “Aaah! Yule demu kazimika ile mbaya na mapigo yangu, kila ninachotaka ananinpa anajua akinizingua namtosa,hadi mshahara wake akipata ananigawia”.

Ninachotaka kusema leo ikiwa ni katika kumalizia mada hiyo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano wowote na pesa, ukiona mpenzi wako anaweka pesa mbele na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha.

Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna mueleze kwamba sina kisha muangalie jinsi gani mnaweza kusaidiana katika kutatua tatizo linalomkabili.

Itakuwa sio busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba ukimweleza mpenzi wako ataona kwamba unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana, na hili ni kwa pande zote mbili.

Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi umemuomba mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija akuletee chipsi mayai, baadaye unataka akupeleke ‘out’, bila kujali kwamba wakati huo mpenzi wako ana fedha au hana. Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka? Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu?

Kimsingi kama nilivyosema wiki iliyopita, ukiwa na mpenzi mwenye tabia ya kutaka kukuomba pesa kila wakati tena katika matumizi mengine ambayo sio ya msingi, mbinu zifuatazo ni muhimu kuzifuata:

Kuwa muwazi
Kama huna pesa wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana pesa au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi.

Wakati mwingine naye akusaidie
Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake. Ifike wakati kwa makusudi,

mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna pesa zinavyokuwa hazitoshi na akaweza kubana matumizi.
Usifuje pesa

Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa pesa kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa wewe unazo.
Unachotakiwa kufanya mapema ni kudhibiti matumizi yako hata kama pesa zinakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.

Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, mapenzi ni kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe ukiwa na tatizo akusaidie. Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero. Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo epukana na tabia hiyo.

Niishie hapo kwa leo, tuonane tena wiki ijayo kwa mada nyingine kali lakini kwa ushauri zaidi unaweza kunicheki kwenye namba 0713070116. Ukiwa unahitaji ushauri unaohitaji tuongee muda mrefu, hakikisha unatumia tigo kisha weka huduma ya extreme,tutaongea bure na utaridhika.
 
B

bwanashamba

Senior Member
Joined
Mar 29, 2010
Messages
193
Likes
0
Points
0
B

bwanashamba

Senior Member
Joined Mar 29, 2010
193 0 0
ntafanyia kazi ndugu course natarajia kuingia choo cha kike
uku nikiona kabisaaa kwa macho yangu.
 
hussein boxer

hussein boxer

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Messages
774
Likes
221
Points
60
Age
34
hussein boxer

hussein boxer

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2013
774 221 60
mimi nilimpima demu wangu ambaye nilitarajia kufunga nae ndoa aliniomba elfu 30 ya kusuka nikamuambia sina mpaka sasa amekata mawasiliana na mimi.
 
jje's

jje's

JF Gold Member
Joined
Sep 3, 2014
Messages
10,009
Likes
13,979
Points
280
jje's

jje's

JF Gold Member
Joined Sep 3, 2014
10,009 13,979 280
mimi nilimpima demu wangu ambaye nilitarajia kufunga nae ndoa aliniomba elfu 30 ya kusuka nikamuambia sina mpaka sasa amekata mawasiliana na mimi.
Sasa kama elfu 30 tu unasema huna utakuwa unaacha kodi ya meza kweli?

ndio maana nawapendaga kina atoto na Miss Chagga. wao husema ukweli bila unafiki.
 
jje's

jje's

JF Gold Member
Joined
Sep 3, 2014
Messages
10,009
Likes
13,979
Points
280
jje's

jje's

JF Gold Member
Joined Sep 3, 2014
10,009 13,979 280
mimi nilimpima demu wangu ambaye nilitarajia kufunga nae ndoa aliniomba elfu 30 ya kusuka nikamuambia sina mpaka sasa amekata mawasiliana na mimi.

nimesahau ku-add something,

vipimo vingine havina mantiki kabisa, inaelekea hata akiomba elfu 10 huwa unabisha tu kwamba sina, akaona ngoja aseme angalau 30 aone labda hujazoea kutoa hela ndogo nayo huna.

Looh akaona shida za nini bora ajiongeze mapema.

Wanaume msiwe wabahili sana kwa wapenzi wenu jamani, mwanamke matunzo.
 
hussein boxer

hussein boxer

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Messages
774
Likes
221
Points
60
Age
34
hussein boxer

hussein boxer

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2013
774 221 60
Sasa kama elfu 30 tu unasema huna utakuwa unaacha kodi ya meza kweli?

ndio maana nawapendaga kina atoto na Miss Chagga. wao husema ukweli bila unafiki.
hiyo 30 ni nyingi sana kwa kusuka hiyo ni kodi ya nyumba ya mwezi mmoja kabisa
 
hussein boxer

hussein boxer

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Messages
774
Likes
221
Points
60
Age
34
hussein boxer

hussein boxer

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2013
774 221 60
nimesahau ku-add something,

vipimo vingine havina mantiki kabisa, inaelekea hata akiomba elfu 10 huwa unabisha tu kwamba sina, akaona ngoja aseme angalau 30 aone labda hujazoea kutoa hela ndogo nayo huna.

Looh akaona shida za nini bora ajiongeze mapema.

Wanaume msiwe wabahili sana kwa wapenzi wenu jamani, mwanamke matunzo.
demu mwenyewe bado sijamgonga huoni nikimpa hiyo hela ni hasara?
 
hussein boxer

hussein boxer

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Messages
774
Likes
221
Points
60
Age
34
hussein boxer

hussein boxer

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2013
774 221 60
Sasa kama elfu 30 tu unasema huna utakuwa unaacha kodi ya meza kweli?

ndio maana nawapendaga kina atoto na Miss Chagga. wao husema ukweli bila unafiki.
kodi ya meza nitaacha atakapokuwa tayari ni waifu.
 
peterchoka

peterchoka

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Messages
7,412
Likes
7,248
Points
280
peterchoka

peterchoka

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2014
7,412 7,248 280
ukifika home ukifungua unakuta mbwa
 

Forum statistics

Threads 1,250,538
Members 481,405
Posts 29,736,930