MtuHabari
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 321
- 1,019
Nimejaribu kuangalia mwenendo wa nchi kwa sasa baada ya uchaguzi mkuu uliohujumiwa wa 2020.
Kikubwa ambacho kama nchi tutakuja kukijutia na "kitengo" watajua kuwa hawajui ni kwa kuingilia mchakato wa wananchi kupata wabunge wao na kitengo kuwapangia wabunge wawe kina nani.
Kama walitaka kupanga uongozi wangebaki na nafasi hiyo ya Rais pekee na kuacha vichwa viwezavyo kukosoa Serikali, kukemea wizi na kufichua maovu bila woga na kwa akili kubwa vibaki kuwepo bungeni kupunguza hata ile nyongo ya wananchi. Lakini sasa kwa miaka mitano ijayo tutashuhudia chuki kubwa sana baina ya Wananchi na Serikali yao maana hata kwenye machungu wabunge waliopo WATASIFIA SERIKALI KINAFIKI.
Nini kifanyike maana hata baada ya uchaguzi kuvurugwa hakuna aendaye mahakamani kupinga kwani hata imani na Mahakama nayo imepotea?