Katika maisha tunahitaji kichwa chenye ubongo na akili zenye maarifa

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Feb 27, 2021
484
541
Kumbuka Katika maisha kuna mtu huwezi kumkwepa. Anaitwa chakubimbi. Chakubimbi ni mtu mwenye mdomo mkubwa, akili ndogo.

Sikiliza! Mara nyingi huwa kuna ukweli ndani ya neno natania na kuna siri nzito ndani ya neno sijui na kuna maumivu makali ndani ya neno niko sawa alisema muhenga wa kale sana!

Katika maisha tunahitaji kichwa chenye ubongo na akili zenye maarifa. Kuwa na akili ni jambo moja, jinsi unavyozitumia ni jambo jingine! Sasa ukitaka heshima kwa gharama ya juu utalipwa dharau kwa bei ya chini! Dunia inaongozwa na watu wenye akili na kuharibiwa na watu wenye nguvu!

Wahenga wakale waliwahi kusema sio muhimu kusema kila unalolijua, la muhimu zaidi ni kujua kila unalosema. Hili nalosema nalijua! Sehemu yenye utajiri mwingi duniani sio kwenye migodi ya dhahabu bali ni makaburini. Kule kuna watu walikufa na mawazo yao akilini bila ya kuyatekeleza. Walikuwa wanasubiri muda muafaka wa kuanza. Wakafa bila kuanza.

TUSIWE KAMA HAO

PGO Nakeraaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom