Katika kumu enzi nyerere umejifunza nini?

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,615
Ni rahisi sana watu kupanga siku za maadhimisho ya mwalimu Nyerere na hata kubishana ni siku gani iliyo bora zaidi. Ni rahisi pia kupitia hotuba za mwalimu ukazisoma na kumbua mazuri mabaya na usia kama kioo cha utabiri na matukio mengi yanayotuhusu kama jamii, lakini haitakuwa na maana yoyote ikiwa hujajifunza lolote kutokana na uongozi wake na ukatumia mafundisho yake kuwa msingi wa mtazamo msimamo na mwelekeo wa Tanzania uitakayo..

Binafsi yangu yapo mengi sana nilojifunza, pamoja na kwamba watu wameandika vitabu, wengine hata kumuiga sauti ktk mazungumzo yao, na wengi zaidi kutumia mifano yake ktk simulizi za hoja zao ili zipate mshiko..Lakini kubwa zaidi ambalo mimi nalikubali kwa mwalimu ni ujumbe wake unaohusu zaidi Utajiri wa roho...ile HADHI ya kuwa huru na mwenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kuthamini UTU bila kushawishika na mataifa au utajiri wa mtu, bila kujali rangi, kabila au jinsia.. Waswahili husema - Maskini Jeuri, lakini tafsiri haswa ya fikra na mtazamo wa mwalimu ilikuwa na malengo ya wananchi kuwa na ROHO ya KITAJIRI japokuwa ni MASKINI wa mali.

Nimesoma vitabu vingi vya mwalimu na mara nyingi nimekuwa nikijiuliza ujasiri ule kaupata wapi? ni shule gani ilomfundisha maswala mazito yenye uzalendo ambao sii rahisi kwa viongozi wengine kuufuata hali kazi waliyokabidhiwa na wananchi ni ile ile, mamlaka ni yale yale lakini wameshindwa hata kujiwekea legacy ambayo itawakumbuka kwa mafundisho ama matendo yao. Africa nzima tuna viongozi wachache sana wa mfano wa mwalimu na wote ambao wanakubalika leo, ni wale waliojenga Utaifa wakaweza kuzitajirisha nyoyo za wananchi kwa kuwapa imani ya thamani ya UTU wao. Namkumbuka Abdi Nassar wa Misri, Kwame Nkurumah wa Ghana na SekoToure wa Guinea ambao kamwe hawatasahaulika kwa misingi walioiacha ktk ujenzi wa imani zetu..

Leo hii, Tanzania yetu imejaa watu na viongozi ambao hawana kabisa Utajiri wa roho, maamuzi na matendo yao ni ya kitumwa zaidi ya wakati tuliotawaliwa. Tumezidi kutokomea ktk lindi la umaskini wa roho kiasi kwamba juhudi zote za mwalimu na waasisi wengine wa Uhuru wa mwafrika katika ujenzi na utambulisho wa UTU wetu zimepotea kwa kasi kubwa sana na hivi sasa tumerudi ktk Utumwa na umaskini wa roho kiasi kwamba adui mkubwa wa mwafrika ni mwafrika mwenzake, ni jirani yako ni rafiki yako na pengine hata ndugu yako!.

Na athari za umaskini wa roho unajitokeza wazi - roho mbaya, watu wamekuwa wabinafsi, Uzalendo ni utamaduni uliopitwa na wakati, kati ya watu 10 wanane hawaaminiani, na hakuna mtu anataka kuaminiwa isipokuwa kuogopwa. Tumeipoteza FAITH kwa sababu hatujui tunakwenda wapi, hatuna dira ya kitaifa wala haihitajiki. Umaskini wa roho umeondoa trust, hope and Belief ya UTU wa Mtanzania kiasi kwamba tumechukua utajiri wa Mali kuwa kigezo cha Tanzania mpya...Na hakika UFISADI ni matunda ya umaskini wa roho kwa sababu hakuna mtu hatari sana kama maskini wa roho anapokabidhiwa mamlaka ya kushika mali..Maskini wa roho huongozwa na vitu vitatu Ignorance, greed and selfishness.
Ni bora ukutane na Tajiri maskini wa roho, kuliko kukutana na maskini wa mali na roho...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom