katika kulinda ufisadi;Rais Kikwete apiga mkwara mabalozi uchaguzi 2010

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Rais Kikwete apiga mkwara mabalozi uchaguzi 2010





Raisi Jakaya Kikwete ambaye amewaonya mabalozi kutothubutu kujihusisha na chama chochote cha siasa wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwakani

Ramadhan Semtawa

RAIS Jakaya Kikwete jana alitumia hafla ya kukaribisha mwaka 2010 kwa kuwaonya mabalozi kutothubutu kujihusisha na chama chochote cha siasa wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.


Katika hafla ya kawaida ya kusherehekea Mwaka Mpya na mabalozi kutoka nchi mbalimbali, Rais Kikwete alisema kitendo chochote cha mabalozi hao kushabikia chama chochote kitashughulikiwa vema na serikali yake.


"Tunawashukuru sana nyote ambao mmekuwa mkisaidia mchakato wa programu za uchaguzi chini ya Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)," rais alianza kurusha kombora hilo.


Kitu ambacho Tanzania isingependa kuona, alisema Rais Kikwete, ni miongoni mwa mabalozi kugeuka kuwa wanachama wa vyama fulani kwa kuvishabikia na kulazimisha kuchagulia Watanzania mtu au chama fulani.


"Tafadhali jizuieni kufanya hivyo," alionya rais.


"Mkifanya hivyo mtakuwa mmevuka hatua ya mamlaka yenu na hiyo itakuwa ni ukiukaji wa maadili ya kazi za kidiplomasia."


Kikwete, ambaye anatarajiwa kugombea urais kwa kipindi kingine cha miaka mitano kupitia CCM, alisisitiza kwamba licha ya heshima kubwa kwa wanadiplomasia hao lakini kitendo hicho kitashughulikiwa kwa nguvu.


Ni kwa nadra sana mabalozi huingilia siasa za ndani na hasa kwenye uchaguzi, lakini iwapo misingi ya kidemokrasia inakiukwa kwenye uchaguzi au uendeshaji nchi, mabalozi hutoa taarifa kwa nchi zao ambazo huamua kuiweka serikali kwenye hali ngumu kifedha, hasa nchi wahisani ambazo huamua kuzuia fedha zao wanazoahidi kwenye bajeti ya nchi husika.


Mkuu huyo wa nchi aliongeza kwamba serikali imepanga kuhakikisha uchaguzi huo wa Oktoba unakuwa huru na haki ukitawaliwa na amani na utulivu.


Kwa mujibu wa rais, hakuna mtu atakosa haki yake ya kupiga kura au kupigiwa kura na kusisitiza kwamba hata uchaguzi wa serikali za mitaa wa Oktoba mwaka jana ulikuwa huru na haki.


Kuhusu athari za mvua zinazoendelea kunyesha, rais alisema uharibifu wa miundombinu, na hasa madaraja unahitaji Sh6.7 bilioni ambazo serikali inategemea kuzinyofoa kwenye fedha zilizotengwa kwa wizara mbalimbali.


Balozi Juma Mpango, akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa mabalozi nchini, alisema wamekuwa wakiridhishwa kuona Tanzania imekuwa nchi ya amani na utulivu na utekelezaji mzuri wa mwafaka visiwani Zanzibar kati ya CUF na CCM.


Mpango, ambaye ni kiongozi wa mabalozi nchini, alisema nchi hizo zimekuwa zikifuatilia kwa karibu mazungumzo kati ya katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na Rais Aman Abeid Karume, hivyo wataendelea kuunga mkono juhudi hizo.


Kwa mujibu wa mpango, mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini pia wanaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuimarisha utawala bora na kupambana na rushwa.


Jana Rais Kikwete aliwaalika mabalozi wote wanaowakilisha nchi zao nchini kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2010, hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
 
we mwongo!
yaani ile taarifa ya habari ya jana anakaribisha mabalozi kwa nia njema wewe unakuja na SINGLE YAKO?....

ACHA USANII MZEE!..
 
Back
Top Bottom