Katika kuitafsiri na kuiishi demokrasia kwa vitendo, CCM hakina mpinzani. Vyama vingine vijifunze kutoka CCM ili kujenga demokrasia bora

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,600
Utaratibu, mila, desturi na utamaduni wa wanaCCM na watanzania kukosoa serikali na CCM ni jambo si la kukoma wala kuacha. Katika moja ya mikutano yake, Katibu Mkuu wa CCM amewaasa wanachama wa chama hicho kikongwe Afrika kuwa huru kuikosoa serikali na CCM kwa sababu ni utamaduni uliopo na yeye kama katibu mkuu hana’ mandate’ ya kuutoa utaratibu huo wala chama hakina nia hiyo.

CCM kinajiimarisha kwa kadiri kinavokoselewa na kikiimarika maana yake kitakuwa ni bora Zaidi katika kuisimamia serikali yake. Kutokana na kauli hii, naweza kusema CCM ya sasa ambayo ni imara katika kuisimamia serikali ni zao la kukubali kukosolewa na kufanyia kazi kasoro hizo. Katibu mkuu wa CCM anaposema kukosoa ni utamaduni na desturi ya CCM ana maana ya kwamba CCM imejengwa katika msingi huo na kila mwanaCCM kuanzia kwa mwenyekiti wa CCM taifa anafuata utaratibu huo.

Mengine yanayosemwa nje kwenye vibaraza na vijiwe kuwa CCM ya sasa haikosolewi ni ya kuachana nayo kwa sababu si utamaduni na utaratibu wa CCM na mwenye jukumu la kutukumbusha utaratibu huo ni Katibu mkuu wetu wa CCM na kasema kuwa utaratibu huo ni mzuri, uendelee kufuatwa. Nikiri kusema KM wa CCM na Mwenyekiti wake ni moja ya zao huru la fikra kupitia kukosoa na kukosolewa.

Utaratibu, utamaduni, mila na desturi hii ya CCM kukosoa, kukosolewa na kukosoana ni jambo muhimu katika ukuaji wa demokrasia nchini. Kwa maana hii, nikiri kusema kuwa CCM kwa Tanzania ndicho chama kinachoitafsiri na kuiishi demokrasia kwa vitendo na hakina mpinzani katika hilo. Wale wanaohoji demokrasia ya CCM, wanalijua hili? Pengine hawalijui na wanahitaji kufafanuliwa ili walijue.

Huwezi kujenga taasisi imara na yenye demokrasia kubwa kama CCM ukiwaziba midomo wasikosoe hivyo CCM imetokana na kukosoa, kukosolewa na kukosoana. Demokrasia iliyopo Tanzania ni zao la utaratibu, utamaduni, mila na desturi za CCM katika kukosoa.

CCM ingekuwa hahitaji kukosolewa, ninaamini leo bajeti ya wizara ya mambo ya ndani ingekuwa kubwa kuliko bajeti ya wizara ya ujenzi kwa maana kwamba bajeti ya wizara ya wizara ya mambo ya ndani ingeongezeka ili kujenga magereza mengi kwa ajili ya wakosoaji lakini si hivyo, wizara ya ujenzi ndio kubwa kwa sababu ukosoaji unajenga uchumi.

Kutokana na utamaduni huu wa kukosoa unavyoishi ndani ya CCM na kufanya CCM kuwa ni chama kinachoitafsiri na kuiishi demokrasia kwa vitendo na si mdomoni, upinzani una mengi ya kujifunza kutoka CCM. Upinzani umeonesha ombwe kubwa kwa mtu mwenye fikra mbadala

Hata wapinzani wenyewe wanakuwa huru Zaidi kuikosoa CCM kuliko vyama vyao kwa sababu utaratibu, utamaduni, mila na desturi za kukosoa ndani ya upinzani haujawa wazi kuliko ule wa CCM. CCM inachukulia kukosoa ni fikra mbadala lakini wenzetu wanaamini kukosoa ni usaliti.
 
Kwa hiyo kuwazuia wenye nia ya kugombea urais 2020 kuonyesha nia zao nayo pia ni moja ya mbinu za kutafsiri demokrasia? Mf. Membe anavyoshutumiwa kuwa anataka kumpinga magufuli 2020.
 
Kwa hiyo kuwazuia wenye nia ya kugombea urais 2020 kuonyesha nia zao nayo pia ni moja ya mbinu za kutafsiri demokrasia? Mf. Membe anavyoshutumiwa kuwa anataka kumpinga magufuli 2020.
hakuna yeyote aliyezuiwa kufanya hivyo zaidi ya maneno ya kufukirika tu mtaani. kauli ya CCM inatoka katika sehemu rasmi na vikao rasmi vya kitaifa. hao wanaotoa kauli nje ya utaratibu wa vikao ni maoni yao binafsi si ya chama. katibu mwenezi au katibu mkuu wa CCM wakitoa kauli, hiyo ndio kauli ya chama
 
hakuna yeyote aliyezuiwa kufanya hivyo zaidi ya maneno ya kufukirika tu mtaani. kauli ya CCM inatoka katika sehemu rasmi na vikao rasmi vya kitaifa. hao wanaotoa kauli nje ya utaratibu wa vikao ni maoni yao binafsi si ya chama. katibu mwenezi au katibu mkuu wa CCM wakitoa kauli, hiyo ndio kauli ya chama
Kwahiyo wewe unapingana na Katibu Mkuu pamoja na Rostam Aziz, au hujawahi kusikia katibu mkuu akimtaka membe kufika ofisini kwa ajili ya mahojiano.?
 
Msipozuia watu kumpokea Lissu mnamo tarehe 7 septemba nitayaamini mambo yako.Vinginevyo nitaamini wasemayo wahenga kuwa bila polisi,TISS na jeshi CCM haiwezi kupambana na APPT Maendeleo kwenye uwanda wa demokrasia
 
CCM wawape upinzani access ya dola kama wao na mikutano ya hadhara iwepo waone kama after next 20 years CCM haitakuwepo.Vijana wanaokuja sasa (watoto wetu) wako kisayansi na kiutandawazi Zaidi wakati wazee wa sasa hawabadiliki.Mark my word after 20 years from now CCM isipobadilika hawa vijana wetu ni species nyingine kabisa.CCM msijidanganye aiseee mbadilike muendeshe chama kisayansi na sio kidictetar soon ndani ya CCM kutakuwa na chama cha upinzani mioyoni mwa wanaccm na wala sio ndani ya CCM
 
Ccm ni chama au genge la wahuni ,mafisadi,wezi ,wala rushwa ,wauaji ,wakiukaji haki za binadamu ,wavunja sheria na katiba ,zaidi hapo hakuna .
 
Back
Top Bottom