Katika kuelekea kujivua gamba hali ya hewa ndani ya CCM SI SHWARI

Kuna tetesi nilizipata jana kuwa hali si nzuri sana kati ya mwenyeki ti na sekretarit ya ccm . Habari hizo ambazo bado ni tetesi zinasema kuwa inaonekana mwenyekiti anampango wa kuwatosa wanasekretariet hao na kuweka watu wake ambao anauhakika hata akiondoka atakiacha chama katika hali nzuri. Na amekuwa akiwatumia baadhi ya wajumbe wa nec katika mpango wake huo bila kuwashirikisha sekretariet hali iliyopeleke Wanasekretariet hao hasa makamba wakimlaumu mwenyekiti kuwa amekuwa anapelekewa umbea na watu kuwa sekretariet imechoka na inapaswa toswe yote. Wakati mwenyekiti akijua jinsi sekretarit hiyo ilivyofanya kazi ya ziada kuhakisha ushindi wa chama chao.

Hata hivyo habari zinasema baadhi ya wanasekretariet hasa makamba na chiligati wanaona upepo huo huenda ukawakumba hivyo nayenyewe wamejipanga kuhakikisha wataweka waridhi wanaowataka wao ndiyo waitiongoza sekretariet hiyo.
Huyo mwnyekiti wa CCM anaweza yote kila mtu anajua alivyoingia kwa njia ya umafia kwa mtandao aliokuwa ameutandaza ndani ya chama na serikalini kama atafanikiwa heri yake lakini asipotengeneza mchoro wake vizuri inaweza kula kwake CCM ikasambaratika ndani ya mikono yake ,majeruhi ni wengi na kwa vile wanajua mbinu zake nadhani anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom