Katika kipindi cha likizo ya COVID 19 Wanafunzi 101 Shinyanga wapata mimba

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
126
250
"Katika kipindi cha likizo ya COVID 19 Wanafunzi 101 Shinyanga wapata mimba"

WANAFUNZI 101 mkoani Shinyanga wamepata ujauzito katika kipindi cha mwezi mmoja, kuanzia Machi hadi Aprili Mwaka huu.

Wanafunzi hao wamepata ujauzito huo katika kipindi cha likizo ya kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na kirusi cha Corona.

Pamoja na ujauzito huo, pia katika kipindi hicho ndoa za utotoni 16 zimeripotiwa katika dawati la jinsia la Polisi mkoani humo.

Mkurugenzi wa shirika la kutetea Haki za wanawake na watoto la KIVULINI Yassin Ally amesema pamoja na mimba hizo mkoa huo una kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni nchini kwa kuwa na asilimia 59 ikifuatiwa Tabora yenye 58.

Ally ametoa kauli hiyo, wakati alipoenda kutoa msaada wa matenki 16 yenye ujazo wa lita 1000 kwa ajili ya kuyatumia kunawa mikono wanafunzi kwenye shule za msingi na Sekondari za Halmashauri mbili za Shinyanga vijijini na Kishapu.

"Kwa mjibu wa taarifa za dawati la jinsia, Machi - Aprili wanafunzi 101 wameripotiwa kupata ujauzito, ambapo halmashauri ya Shinyanga ina wanafunzi 26, Kishapu 25, Manispaa Shinyanga 20 Msalala 17 na Kahama 16.

"Hizi takwimu za mwezi zinaonesha kabisa kuna changamoto na huenda tukipima baada ya shule kufunguliwa idadi hii inaweza kuongezeka," amesema Yassin.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba, amesema Serikali wilayani humo itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobanika kuwapa ujauzito wanafunzi.

Amesema kuwa, pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria lakini watahakikisha wanapewa adhabu kwanza ya kufanya shughuli za kijamii kabla ya kupandishwa kortini.

Sanjari na hayo, mkurugenzi huyo amewataka walimu wa shule za msingi na Sekondari kuhakikisha wanaongeza juhudi za ufunndishaji ili kuongeza ufaulu hususani kwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajiwa kuhitmu mwaka huu.

Mwalimu mkuu shule ya msingi ya Iselamagazi, amesema wamejiwekea mikakati inayohusu watoto wa kike kukutana na walimu wa kike kufahamu changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuangalia mienendo yao.

"Tumeanzisha chumba maalumu kinachohusu mtoto wa kike hususani ni pale wanapotoka katika siku yake ambapo walimu wamekuwa wakiwashauri.

Mwanafunzi wa darasa saba katika shule ya msingi Iselemagazi, Kulwa Lameck, amesema tamaa inachangia wanafunzi kupata mimba, pamoja na wanafunzi kuendekeza makundi ya kihuni mtaani na yale ya shuleni.

Kulwa amewashauri wanafunzi kusoma kwa bidii kwani ndio njiia ambayi itawafikisha katika mafanikio pamoja na kuachana na makundi ya kihuni.

IMG20200701112055.jpg

Mwisho
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,662
2,000

Kulwa amewashauri wanafunzi kusoma kwa bidii kwani ndio njiia ambayi itawafikisha katika mafanikio pamoja na kuachana na makundi ya kihuni.Mwisho
Hawakupewa semina kuwa siyo likizo ya honeymoon, matokeo ndiyo hayo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom