Katika Katiba: Wabunge wote mlikosea! Rais Tafakari Kabla Hujatia Saini Muswada Huo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katika Katiba: Wabunge wote mlikosea! Rais Tafakari Kabla Hujatia Saini Muswada Huo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sikonge, Nov 22, 2011.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nini maoni yako kuhusu hili kosa la wabunge wetu WOTE? Naungana na wanaosema hili kosa, lazima Rais wetu alisahihishe kwa kutokuweka sahihi iwe au bila mbwembwe hii katiba. Swala lianze upya kwa faida ya Watanzania wote.

   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Samahani kwa ujumbe wa hapo juu....

  Baada ya kusikiliza hotuba ya Tundu Lisu, anasikika kabisa akitaja Kifungu cha 86 (3) (b) na kulitaka BUNGE likatae mjadala kusomwa mara ya pili.

  Pia mwisho ni kweli alikosea na kusema ".......Muheshimiwa Spika, naomba kuwakilisha." Ila baada ya sekundi chache, alirudia ujumbe wake na kusema "...... naomba kutowa hoja muheshimiwa spika."

  Spika akaja na kicheko chake na kusema TL ametumia kifungu cha 86 (6) na anasema ".... Muheshimiwa TL anawasilisha hotuba maoni ya kambi ya upinzani kwa kanuni ya 86 (6). Hiyo haitowi hoja ni maoni yake na ...... hayo ni maoni ya kambi ya upinzani."

  Ukifuatilia zaidi, unasikia sasa sauti ya John Mnyika akisema wazi kabisa "HOJA KUAHIRISHA BUNGE." Hoja ya kuahirisha Bunge imeandikwa kwenye kifungu hicho cha 86 (3) (b) na inaweza kutolewa na mbunge yeyote. Maadamu wabunge wote hawawezi kusema pamoja, kuna uwezekano wa wenye hoja hiyo wakachelewa, kama Mnyika.

  Kwa sababu hiyo, naondoa maneno yangu hapo juu kuwa Wabunge wote walaumiwe. Lawama hizo zisiende kwa hawa wacheche ambao walitamka waziwazi hayo maneno/kifungu cha 86 (3) (b) au kuwa na msimamo wa kutaka kushinikiza kifungu hicho kitumike. Tafadhali kama unaweza basi sikiliza hii video hadi kwenye dakika 1:50 tu. Ukitaka kumsikiliza Anna Kilango anavyokula matapishi yake, waweza kumsikiliza zaidi.......  Ukisiki
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kama unataka kusikiliza zaidi ndoa ya CCM na CUF basi sikiliza hii hituba.

  Wazenji wakiona hii, watajua kama kweli ni sisi Watanganyika tumewapa hizo shida au ni jamaa wao wa CUF ndiyo wanataka Zanzibar iendelee kutawaliwa na Tanganyika. Na maadamu CCM kila mke ni Neema, basi wanapeta.

  Msikiliza uozo anaoboronga hapa chini..................

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...