SoC01 Katika jamii zetu kitu kinachotupa hofu ya kuendelea ni kuogopa mabadiliko

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Kama tujuavyo kila kitu kina sababu ya kuumbwa je? haudhani kwamba wewe ni sababu bora na ndio maana unaishi hadi kufikia hivi sasa, hebu jaribu kufikiria kitu.

Katika jamii zetu kitu kinachotupa hofu ya kuendelea ni kuogopa mabadiliko yanayoweza kutukabili Kwa kuogopa kujaribu tukidhani tutapata hasara zinazoweza kujitokeza mbele yetu.

Hivyo tunapaswa kuwa na imani uvumilivu na nia ya kufanya vitu zaidi na zaidi pasipo kukata tamaa Kwa kuwa hakuna kufanikiwa pasipokuwa na uvumilivu. Hivyo cha msingi unayo afya njema basi ujue unayo nafasi ya kushinda changamoto za maisha na kuyafikia maendeleo yako na pengine ukasaidia ndugu na jamaa.

Japokuwa wewe unapotaka kufika mbali usisubiri usaidiwe kwanza kiukweli ni kwamba utapoteza muda wako bure kwakuwa yule ategemeae cha ndugu hufa angali masikini, Hata kwenye vitabu vitakatifu imeandikwa kwamba umeumbwa kuwa kichwa wala si mkia hivyo wewe ni nyota unaetegemewa ung'are mahali penye kiza kinene ili wengine japo waione njia.

Kama tunavyojua umasikini ni sawa na usingizi mzito ambao kama hutokua na akili ya kuamka basi utakuta wenzako wamepiga hatua na kukuacha mbali. kimantiki ni kwamba tunapaswa kuzichukulia changamoto katika jamii na kuzibadilisha kuwa fursa, Inawezekana kuwa mtaani kwako kuna changamoto ambazo pia ni fursa hata pengine ukaziona lakini shida ikawa kwenye kuzianzisha au hata kukabiriana na hizo changamoto.

Hivyo changamoto zipo ila pia tuzione kwa jicho la tatu kwamba ni kwa namna gani zitatunufaisha. Kwa hakika sio wote tunaotokea kwenye maisha zenye kipato kizuri cha fedha.. Ila mtaji bora na thamani yako ni akili yako fikra zako na jitihada zenye kuvumilia kila hali bila kuchoka, endapo tukifanya hivyo kwa hakika mafanikio yapo mbele yetu.

Hivyo tutaweza kujijengea uchumi wetu kwa maendeleo yetu na maendeleo ya taifa letu.
nawaombeni tusiwe watu wa kukata tamaa tuendelee kujaribu kwa kuwa hakuna muujiza kwenye maisha ambao utakuja bila kufanywa kwa mikono yetu wenyewe.

Asante kwa kupitia makala hii hakika itakusaidia mahali fulani.
 
Back
Top Bottom