Wadau nachukua nafasi hii kuwatakia heri ya Pasaka.
Kama mnavyojua jumatano iliyopita tarehe 31/03/2021 wakati wa kumwapisha makamu wa Rais, mh Rais alitangaza baraza jipya la mawaziri, lakini mimi sina uhakika kama alikuwa sahihi.
Hoja yangu ni kwamba je ni halali kutangaza baraza jipya la mawaziri bila kuteua kwanza waziri mkuu?
Na je waziri mkuu anakuwaje halali wakati alikula kiapo kwa Rais tofauti na huyu wa sasa?
Na ni kwa nini mawaziri anaowaongoza ni mawaziri walioapishwa na Rais tofauti na aliyemwapisha?
Mbona yeye kama Rais alikula kiapo kwanza kabla ya kuwa Rais halafu awe na waziri mkuu ambaye hajala kiapo mbele yake?
Tafadhari wajuvi wa mambo tusaidieni tafsiri halali ya kisheria na kikatiba. Ni hayo tu wadau wa jf.