Katika hili UDSM wako sahihi?

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Toka juzi wanafunzi wa UDSM wanaoishi Mabibo Hostel wamegoma kupanda shato wakishinikiza nauli ishuke toka sh. 300 had sh 250. Hawa wanataka nauli ipungue pasipo kufikiri kwanini zimepanda. Mi nadhani ingekuwa busara na uzalendo kama wangeandamana kushinikiza kodi zipunguzwe kwenye mafuta maana siyo wao tu wanaoumia na hizi nauli.:israel:
 
Wajinga hao! Mi jana nilikuwa na pindi saa 3 nikaamka ki-afsa saa mbili unusu, he! Nafika nje sioni gari wala watu, ikabidi nile SP mpaka Ubungo, kutokana na muda ikabidi nichukue gari mpaka utawala... Afu wanaojifanya wanaharakati ndo wale wanaopanda gari siku za test tu, afu wanajifanya wana uchungu! Aaaaaaaaagh!
 
Hiki ndo kizazi chetu ambacho kinadhani kugomea mambo ndiyo maisha. Waache wagome, finally watapakia.
 
Hiki ndo kizazi chetu ambacho kinadhani kugomea mambo ndiyo maisha. Waache wagome, finally watapakia.

Akili zao fupi, imagine mtu anaitisha mgomo eti anataka bei ya chipsi kwenye cafe ishuke mpaka 700. Hajiulizi bei ya viazi, mafuta, cost za kumlipa mfanyikazi ni ngapi, yeye anataka bei ishuke tu! Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha TAIFA, lakini kwa hili hapana, THE BIG NO!
 
Back
Top Bottom