DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,122
Ni majuzi 2 ulifanyika mkutano wa CHADEMA katika viwanja vya sahara jijini mwanza, katika taarifa ya vyombo vya habari ITV ilitoa habari yenye kichawa "CHADEMA NA UMOJA WA WAMACHINGA JIJININI MWANZA WAMPA SIKU 14 WAZIRI MAKUU KUMWONDOA MKURUGENZI WA JIJI HILO BWANA BWANA KABWE KWA KUMTUHUMU KUWA CHANZO CHA MIGOGORO" katika taarifa yao, ITV walimwonyesha mbunge wa nyamagana wenjeakisoma barua kwa niaba ya wamachinga.
Kwa upande mwingine STAR TV, kichwa cha habari kilikuwa "SERKALI YAHIMIZWA KUSIMAMIA RASILIMALI VIZURI KWA MANUFAA YA UMMA" na wakawonyesha viongozi mbalimbali wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutanoa huo.
sikuridhika na kichwa cha habari cha STAR TV, hata kama sio mtaalamu wa uandishi wa habari, kwa sababu moja kubwa kwamba usimamizi bora wa rasilimali za nchi na serikali umezungumzwa sana tena sana, hivyo kuwa na kichwa cha habari cha namna kama ile si kutuletea habari kwa ni habari iliyo kufa tayari, hivyo nikapenda ile ya ITV kwangu ilikuwa ni habari.
Pili, likanijia wazo kuwa STAR TV, inamilikiwa na kada na mwenyekiti wa CCM mkoa bwana Diallo na CCM na wakurugenzi ktka nchi hii huwezi kuwatofautisha hivyo STAR TV wasingependa kutoa habari inayomwangusha mwajiri wao.
Jana ndo nikawagundua jamaa hawa wa STAR TV kuwa wanamlengo wa kisiasa wa upande wa CCM pale walipoleta habari inayoonyesha viongozi wa wamachinga wa mwanza wakimtuhumu Wenje kughushi barua, na kuwachonganisha na serikali na wakamtaka wenje aombe radhi ndani ya siku 14, na hapo STAR TV wakalazimika kuonyesha kipande cha ile habari ambacho kinamuonyesha wenye akisoma barua ya wamachinga.
Hata hao wamachinga kama ile barua si ya kweli lakini kwa yeyote anayeishi mwanza mwenye kutumia akili yake vizuri anafahamu jinsi mkurugenzi huyu anavyolalamikiwa na wanachi kama mtu mwenye kiburi cha madaraka, fisadi (reje mgogoro wake na mwananchi mmoja wa luchelele kwa madai kuwa kavamia kiwanja chake), soko la mwaloni, ni mtu mwenye kutaka kuibeba CCM muda wote na mengine mengi, hivyo kwangu nikisikia watu hawamtaki sitashangaa kwani hapa mwanza yamekuwa yakiongelewa kwa muda mrefu sna.
Binafsi ningependa kuwaasa/kuwaomba STAR Tv, kwangu kimekuwa ni kituo changu cha kwanza cha habari kwa muda mrefu, then Channel 10, ITV, na mwisho TBCCM, hivyo wasiharibu sifa nzuri waliojijengea kwa jamii kwa kukubari kutumika.