Katika hili, Star TV walipotoka

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,976
3,122
Ni majuzi 2 ulifanyika mkutano wa CHADEMA katika viwanja vya sahara jijini mwanza, katika taarifa ya vyombo vya habari ITV ilitoa habari yenye kichawa "CHADEMA NA UMOJA WA WAMACHINGA JIJININI MWANZA WAMPA SIKU 14 WAZIRI MAKUU KUMWONDOA MKURUGENZI WA JIJI HILO BWANA BWANA KABWE KWA KUMTUHUMU KUWA CHANZO CHA MIGOGORO" katika taarifa yao, ITV walimwonyesha mbunge wa nyamagana wenjeakisoma barua kwa niaba ya wamachinga.

Kwa upande mwingine STAR TV, kichwa cha habari kilikuwa "SERKALI YAHIMIZWA KUSIMAMIA RASILIMALI VIZURI KWA MANUFAA YA UMMA" na wakawonyesha viongozi mbalimbali wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutanoa huo.

sikuridhika na kichwa cha habari cha STAR TV, hata kama sio mtaalamu wa uandishi wa habari, kwa sababu moja kubwa kwamba usimamizi bora wa rasilimali za nchi na serikali umezungumzwa sana tena sana, hivyo kuwa na kichwa cha habari cha namna kama ile si kutuletea habari kwa ni habari iliyo kufa tayari, hivyo nikapenda ile ya ITV kwangu ilikuwa ni habari.

Pili, likanijia wazo kuwa STAR TV, inamilikiwa na kada na mwenyekiti wa CCM mkoa bwana Diallo na CCM na wakurugenzi ktka nchi hii huwezi kuwatofautisha hivyo STAR TV wasingependa kutoa habari inayomwangusha mwajiri wao.

Jana ndo nikawagundua jamaa hawa wa STAR TV kuwa wanamlengo wa kisiasa wa upande wa CCM pale walipoleta habari inayoonyesha viongozi wa wamachinga wa mwanza wakimtuhumu Wenje kughushi barua, na kuwachonganisha na serikali na wakamtaka wenje aombe radhi ndani ya siku 14, na hapo STAR TV wakalazimika kuonyesha kipande cha ile habari ambacho kinamuonyesha wenye akisoma barua ya wamachinga.

Hata hao wamachinga kama ile barua si ya kweli lakini kwa yeyote anayeishi mwanza mwenye kutumia akili yake vizuri anafahamu jinsi mkurugenzi huyu anavyolalamikiwa na wanachi kama mtu mwenye kiburi cha madaraka, fisadi (reje mgogoro wake na mwananchi mmoja wa luchelele kwa madai kuwa kavamia kiwanja chake), soko la mwaloni, ni mtu mwenye kutaka kuibeba CCM muda wote na mengine mengi, hivyo kwangu nikisikia watu hawamtaki sitashangaa kwani hapa mwanza yamekuwa yakiongelewa kwa muda mrefu sna.

Binafsi ningependa kuwaasa/kuwaomba STAR Tv, kwangu kimekuwa ni kituo changu cha kwanza cha habari kwa muda mrefu, then Channel 10, ITV, na mwisho TBCCM, hivyo wasiharibu sifa nzuri waliojijengea kwa jamii kwa kukubari kutumika.
 
mbona hata wewe unatumika kisiasa"? watu wengine bana hata kufikili nako kazi kuuuuubwa!
 
Mapenzi yakizidi inakua ujinga! Yaani wafanye vile unapenda wewe?
 
usiishie juu juu sema ni kivipi natumika kisiasa? vinginevyo kaa kimya/pita tu
 
Hii star Tv tangia Dialo awe Mwenyekiti wa CCM mkoa, wamebadilika sana, ni tofauti na mwanzo kabla hajaawa, Mimi nashauri Viongozi wa CHADEMA wafikilie kuanzisha TV na Redia Mapema sana, tuko tiyali kuchanga hata sent tano ilimuradi iwe hivyo,

Hizi TV mbili Stare TV na TBC kwa sasa sio kabisa, kidogo imebakia ITV na Chanel Ten,
 
Aibu aombe msamaha ndani siku14 vinginevyo hatua kali zichukuliwe kwa wenje wamezoea sana kugushi nyaraka sasa amepatikana viongozi wa machinga msimuonee huruma swaga mahakamani kitaeleweka tu hawa watu ni waongo sana jamani duh.....
 
Ndio maana kile kipindi cha YAHAYA M cha jumapili asbuhi wamekigeuza geuza na hakina tena mada za siasa kwani waliona ccm wanazidi kuabika.star tv sasa inakuwa kama tbcccm
 
Wenje hakurupuki hata siku moja,waliotumwa Star tccm ndo waombe msamaha kwa wamachinga. Nani asiejua ubabe wa Willy Mboneo Kebwa? Anaebishb aende Luchelele aongee na wtz masikini waliodhurumiwa wakafanyiwa usanii wa kusainishwa mikataba feki uloandikwa kwa kiingereza! Jamani anaemtetea huyv bwana sina uhakika km ni mtz halisi! Anakampuni ya uwakili na kijana wake mwanasheria kwa sasa kahamishiwa Dar ni balaa tupu!
 
Rangi za Star TV zilikuwa zimepauka kwa muda mrefu sasa. Subirini muone, baada ya muda mfupi Star TV itakuwa na rangi za kijani kibichi!
 
Wakati ITV na Channel ten wanasonga mbele katika kutoa habari za uhakika na mijadala huru ya kisiasa na kijamii, Star TV na TBC zinakufa taratibu kwa kueneza propaganda chafu za kupotosha umma.

Lakini kwa kuwa watanzania wanauelewa mpana kwa sasa, wanajua mbichi na mbivu, Kwa mwendo huu TBC na Star TV vitakufa taratibu(Natural Death).
 
Ndio maana kile kipindi cha
YAHAYA M cha jumapili asbuhi wamekigeuza geuza na hakina tena mada za
siasa kwani waliona ccm wanazidi kuabika.star tv sasa inakuwa kama
tbcccm

Ni bora ndugu zangu tupitishie habari zetu Tanzania Daima
 
mtoa mada ni mtu binafsi, mwenye mapenzi yake na chama fulani, ndo maana kakerwa na taarifa ya habari ya star tv kwa kuwa imeandaliwa asivyotaka yy. vile vile star tv ni chombo cha habari binafsi yawezekana kinamalengo elekezi ya mmiliki au muandaa taarifa anamapenzi binafsi au alichoaandaa ndiyo ukweli wenyewe, kwangu mimi swali langu ni; alichosema MH WENJE ni kweli alighushi? na ni kweli walioenda studio kutoa malalamiko ni machinga? na kile kilichoandaliwa na kurushwa na itv na kilichoandaliwa na kurushwa na star tv licha ya kutofautiana vichwa vya habari vyote vinawakilisha matatizo yaliyopo au la. matatizo yapo lkn tukiyageuza mitaji ya kisiasa hatutatatua tatizo kamwe.
 
Wakati ITV na Channel ten wanasonga mbele katika kutoa habari za uhakika na mijadala huru ya kisiasa na kijamii, Star TV na TBC zinakufa taratibu kwa kueneza propaganda chafu za kupotosha umma.

Lakini kwa kuwa watanzania wanauelewa mpana kwa sasa, wanajua mbichi na mbivu, Kwa mwendo huu TBC na Star TV vitakufa taratibu(Natural Death).

Suluhisho CHADEMA waanzishe fasta Redio na Tv make hali ya Upotoshaji kwa sasa inatisha, na kwa sasa nimeunganisha star TV kwenye Black rist, Star Tv na TBCCCM huwa sizitazami kabisa, ni bora ninagalie TV ya katuni kuliko hizi TV mbili
 
Ndio maana kile kipindi cha YAHAYA M cha jumapili asbuhi wamekigeuza geuza na hakina tena mada za siasa kwani waliona ccm wanazidi kuabika.star tv sasa inakuwa kama tbcccm


Hawa jamaa wabelekea iliko TBC CCM, na mwisho wa UBAYA ITAKUA NI AIBU KUBWA SANA
 
Ninaweza kuwa sipendi kile mtu anachokisema maana inawezekana sio kile ninacho kiamini, lakini niko tayari kufa kwa kupigania uhuru na haki ya mtu huyo kusema kile anachokiamini na hiyo ndio inaitwa uhuru wa kuongea! Ndugu zangu muda mfupi tu hapa JF watu waliisifia ile hotuba ya AAK aliyoitoa pale Dodoma siku alipokuwa anawaaga CCM wenzie, na sehemu iliyovutia zaidi ( kwa maono yangu) ni pale alipowaasa wanaCCM kuwa waheshimu uhuru wa watu wengine katika kutoa maoni na wawe wavumilivu pale wanaposikia kile wasichopenda kusikia! Dr. kuwa mvumilivu.
 
Makamanda msile lie kama demu aliyebanwa gheto, hebu anzisheni basi hata karedio watu tuskie sumu zenu lakin sio kulalamika daily na kuomba huruma humu kama watoto, hivi maela yote ya M4C mmeshindwa hata kuanzisha kagazeti ka kurasa 1 tu au ndo kusema ubahiri au zile fedha mumempa yule mnafiki Zitto akale xmas uswisi mwezi huu..

Chadema acheni kulilia na kutafuta huruma kama demu.
 
Vyombo vya habari vyote vya serikali na binafsi havitakuwa upande wa chadema kuanzia sasa kuelekea 2015 hata ITV nimekuwa sifurahishwi sana na habari zake kwasasa! La msingi ni tujitegemee kwa kuanzisha hata karedio ketu na kagazeti ketu ka kila siku!
 
kwa hakika startv walishapiga hatua moja mbele lakini kwa mwenendo wa hivi sasa wanaanza kujiporomosha taratiibu..na tatizo hapa ni hivi vyombo vya habari kumilikiwa na wanasiasa.Yahaya ulijitahidi kuipaisha star tv lakiki muda si mrefu utakutana na kilichomkuta Tido mhando.
 
Back
Top Bottom