Katika hili naungana na Antony Mtaka

MMASSY

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
261
250
Nimetazama clip inayozunguka katika mitandao ya kijamii kuhusiana na umuhimu wa makambi ya kitaaluma kwa wanafunzi kwa ajili ya kujiandaa na mithnani ya kitaifa.

Wapo watu ambao wanananga kauli hii na kuona kuwa mkuu huyu wa mkoa amewananga wanasiasa wenzake,sisi tuliopata bahati ya kusoma sehemu yalikofanyika anayozungumzia RC Mtaka tunawashauri watu wa Dodoma wamsikilze Rc wao kwa sababau zifuatazo;

Mosi, mkoa wa Dodoma ni mmoja wa mikoa ambayo ipo chini sana kielimu na inahitaji juhudi zisizo za kawaida sana kuivusha kutoka hapo ilipo. Ni mkoa ambao elimu imekuwa haipewi sana kipaumbele na kwa bahati mbaya suala la elimu ni kama lilikuwa limetekelezwa, au limeachiwa wanasiasa ambao hawana agenda ya maana sana kwenye suala hili

Ukisikiliza wanasiasa wengi wa mkoa wa Dodoma elimu haijawahi kuwa kipaumbele kwao pamoja na kuwa makao makuu ya nchi na sasa makao ya serikali lakini suala la elimu lilibaki kuwa nyuma sana.Juhudi za serikali kuanzia ya Mkapa na Kikwete kuifanya Dodoma mji wa kielimu kwa kuanzisha taasisi za elimu kubwa kama UDOM bado haikutosha sana kuwaamsha viongozi wa mkoa wa Dodoma. Mungu alimwongoza Rais Samia Suluhu Hassan (SSH) kuteua viongozi kama Rc Mtaka pengine wanaweza kuufanya mkoa huu uamke na kuwa kati ya mikoa bora sana katika Nyanja ya elimu japo tayari ameshaanza kukutana na vigingi

Nasema hivyo kwa kuwa najua fika kuwa Rc Mtaka aliteuliwa kuwa Rc Simiyu kipindi ambacho Simiyu ikiwa hoi bin taaban katika suala la elimu na kwa muda mfupi sana tumeona kwa macho na tumesikia namna ambavyo alipambana kuupandisha hadhi mkoa huo hadi kuwa moja ya mikoa inayoongoza katika matokeo ya ngazi mbalimbali. Hivyo Rc kusema wazi kuwa haitaji ushauri wa mwanasiasa yeyote ni kwamba anajua fika wapo wanasiasa ambao wataingilia mchakato huu usifanikiwe.

Pili,tukiangalia mikoa ambayo imekuwa na juhudi za dhati za kuinua elimu tangia kpindi cha nyuma ni kwamba aidha waliamua kuweka siasa pembeni na wakafanyia kazi maoni na ushauri wa kitaalamu ama waliamua kuungana na wanasiasa waliokuwa na maono ya kuendeleza elimu na baadaye wakafanikiwa. Ukiangalia mikoa kama Kilimanjaro ambayo imekuwa na rekodi nzuri sana katika suala la elimu,haibebwi tu na historia, mkoa huo unabebwa na juhudi za wananchi na viongozi waliojitambua mapema na kuweka nguvu katika suala la elimu.Ni mkoa ambao shule zake zote za msingi na sekondari kuna kanuni kuwa lazima watoto wapate mlo wa mchana shuleni.Hapa hakuna longolongo za diwani,mbunge sijui waziri.

Miaka yote tuliyosoma sisi ulikuwa unapeleka debe la mahindi shuleni,sado ya maharage,mafuta ya kupikia na chumvi mara moja kwa mwaka na asiyefanya hivyo kulikuwa na msaragambo wa kumbambua mzazi. Hapa hakuna ngonjera kuwa eti inatolewa elimu bure na serikali wala cha kauli ya waziri.Miaka yote kanuni hii imetekelezwa na wanafunzi wamefaulu vizuri sana.Wengine shule ilikuwa na mashamba ambayo tunaenda kulima na kuvuna magunia ya mahindi na maharage ya kutosha kiasi cha kuwapunguzia mzigo wazazi.

Huko tulijifunza ujasiriamali na hadi leo tunaishi mjini lakini lazima ukute tunaotesha hata mboga kwenye mifuko ya cement na maisha yanaenda.Hizi swaga anazolalamikia Rc Mtaka zilishaisha tangia enzi za ukoloni mkoani Kilimanjaro.Mkoa wa Kilimanjaro mtoto akishaingia shuleni asubuhi kurudi nyumbani ni saa kumi na moja ama saa moja kwa wale wa madarasa ya mitihani.

Swaga za sijui mtoto arudi nyumbani kula mchana hazipo kabisa sababau kwanza huko nyumbani atamkuta nani? Watu wako busy kama sisimizi wanatafuta maisha. Kukutana familia ni jioni sana na kuachana ni mapema alfajiri. Wanasiasa kuona watoto wanazagaa mithani eti wameenda kula kwa o ni credit ya kuombea tena kura wakati mwingine na ahadi hewa.

Tatu, Upo ugonjwa wa kutegemea serikali kwa kila kitu, na ugonjwa huu unaitafuta mikoa mingi ikiwemo Dodoma anayoiongoza kaka Mtaka.Kwa mikoa kama Kilimanjaro, tangia enzi za ukoloni hadi sasa hakuna wakati ambao wananchi waliamini kuwa serikali inaweza kuwasomeshea watoto bure tu na ikawajengea madarasa na kuwalisha.Serikali ilifanya pale ilipoweza na wananchi walijiongeza zaidi na zaidi.

Siku hizi wanasiasa wanaitumia kauli kuwa serikali inatoa elimu bure na wazazi wasitoe michango ya mlinzi,chakula,sijui kuendeleza taaluma.Kinachotokea ni kwamba wakuu wa shule na viongozi wa bodi za shule wanalazimika kusitisha mipango mingi ambayo ingesaidia kuwasaidia wanafunzi waweze kufaulu zaidi.

Ukisoma waraka wa serikali kuhusu elimu bila malipo,hakuna sehemu serikali imesema kuwa itatoa chakula bure,wala kutoa mitihani ya ziada bure,hakuna sehemu ambako kuna ruzuku kwa walimu wanaojitolea kufundisha watoto baada ya muda wa darasani wala kujitolea kufundisha watoto siku za wikiendi.

Watu wa Dodoma msidanganywe na wanasiasa. Msikilizeni mkuu wenu wa mkoa. Sisi wengine tunamtamani aje kuwa Rc huku kwetu tupige hatua kubwa zaidi. Hao wanasiasa wanaowadanganya msichangie makambi ya elimu ndio hao hao watakuja kuwaomba kura kwa kiki za kuwasaidia vijana wanaozagaa mtaani kwa kukosa chakula shuleni na kufeli mitihani yao. Na kama anavyowaambia kiongozi wenu,hao wanasiasa watoto wao hawako huko,wanasoma shule bora kabisa na wanafundishwa masomo ya ziada hadi nyumbani wakati mwingine hadi usiku.

Nne, mikoa kama Kilimanjro ajenda yao sasa sio shule za kata tena wala sio watoto wakae kwenye makambi ama wasikae,wala sio issue ya madawati tena,ajenda yao sasa ni ujenzi wa mabweni katika shule za kutwa. Hili limeanza kitambo zaidi.Wanafunzi wote wa madarasa ya mitihani kuanzia January kila mwaka hukaa bweni. Zipo juhudi za kuhakikisha mabweni yanajengwa kila shule ya kata lakini sasa wameanza na madarasa ya mitihani. Hawajasubiria mwanafunzi abakwe ili kujenga mabweni. Hapa hata angetokea waziri gani akaimba mchana kutwa, ajenda hii haitasistishwa kwa kuwa hakuianzisha yeye. Sana sana akijitokeza mwanasaisa wa kuungana na wananchi katika kutekeleza ajenda kama hizi ndio hukubalika zaidi. Usishangae ni kwanini wabunge wengi wa mkoa wa kilimanjato hawana uhakika wa kuvuka vipindi viwili.Hawa jamaa wakogi serious sana na mambo yao ya maendeleo.

Lakini zaidi ninachoamini mimi,mkuu wenu wa mkoa anavyoongea ni kama vile ana mtoto anasoma shule ya kata hapo Makulu ama Jamatini lakini hapana. Kwa mshahara wake anao uwezo wa kuwasomesha watoto wake shule za maana kabisa lakini bado kajitoa kuwaeleza ukweli wa namna bora ya kuwaisaidia watoto wenu.

Yeye kama Rc anaweza kunyamaza na bado akalipwa mshahara,tena akinyamaza ndio atakuwa sehemu sahihi zaidi sababu hatakwaruzana na wanasiasa. Pili,anaweza kuwaacha maendeleo ya wanenu yakaendelea kuwa mabaya na akaamua kujipaisha kisiasa kwa kuwaadhibu walimu ama wasimamizi wa elimu mkoa hadi wilayani na nyie mkampigia makofi vilevile

Anachowaambia ni sahihi mno. Amekuwa Dc wa Hai na hadi leo wananchi wanakumbuka juhudi zake kwenye suala zima la elimu na mambo mengine. Alikuwa Rc Simiyu akasimamia elimu kindakindaki na hadi leo wanamlilia. Katika suala la elimu tambueni kuwa mnalo jukumu la kumsikiliza jiongozi wenu.

Mikoa kama Kilimanjro suala la serikali kwenye elimu siku zote limekuwa kusimamia mtaala ufuatwe katika ufundishaji lakini mbinu sijui mikakati ya wanafunzi wafaullu vipi hilo siku zote limebaki mikononi mwa wananchi na serikali zao za mitaa.

Aksanteni

Jerome Ernest Mmassy

Arusha
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,430
2,000
Tatizo Mtaka ameonesha kama alikuwa na chuki binafsi na Ndalichako, hata kama ana point, lakini kitendo cha kurudia mara mbili huyo anasomesha watoto wake international school ni ushamba.

Mpaka anavua barakoa eti labda hamniskii, naamini hata yeye Mtaka watoto wake watakuwa wanasoma huko huko, namuona zaidi kama mtu alietaka sifa za kisiasa kwa lile tamko lake, au akienda bar jioni apongezwe, lakini alichofanya ni upuuzi.

Ndalichako angeandika barua ya ku-resign ningemuelewa sana, huu ujinga utaendelea kutokea kwa viongozi wengine waandamizi na kwasababu mamlaka ya uteuzi ni mpole hakuna watakachofanywa.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,283
2,000
Kaomba radhi ila hatujamsamehe
Hata msipo msamehe, nini kitakacho mtokea? Kwa sasa mnapigwa tu za uso, huku mkiwa hamna cha kufanya. Yule mungu wenu aliye watia ujinga, hayupo!

Antony Dialo nae kampiga mungu wenu za uso, na yeye mliishia tu kumtishia nyau! Ccm ilisharudi kwa wenyewe. Mkishindwa kuvumilia haya maumivu, hameni nchi au mfuatene tu mungu wenu huko aliko.

No way out!
 

tamsana

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
963
1,000
Hoja anayo ila ameshindwa kutafuta mlango wa kuitolea. Angeitisha kikao cha ndani cha watendaji wake awape hayo maelekezo.
Naamini maelekezo yake yangetekelezwa viruri tu bila kutengeneza taharuki ya kugomea maelekeo ya kiongozi yeyote.

Kwa hiyo na yeye akitoa maelekezo ambayo sio mazuri kwenye ngazi ya kijiji, Mwenyekiti wa kijiji ampinge hadharani kama yeye alivyofanya kwa Waziri?

Ninachoamini ni kuwa kiongozi mzuri ni yule anayejua kufukia mashimo bila chuki kwa wengine hata kama wanakosea.

Kwa ujumla anayo hoja nzuri yenye mashiko ila ameshindwa kuiwasilisha na kuifanyia kazi kama kiongozi mkomavu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom