Katika hili Madaktari hamtutendei haki wa-Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katika hili Madaktari hamtutendei haki wa-Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by brainiac89, Mar 8, 2012.

 1. brainiac89

  brainiac89 Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nayasema haya nikiwa na uchungu na masikitiko makubwa kwa hiki ambacho madaktari wanachoendelea kututendea waTanzania! kuna machache wacha niyaseme ili moyo wangu utulie!
  1. kama sikosei mgomo wa madaktari wa mwaka 2004, madaktari walikua wanadai ongezeko la mishahara, ambapo kwa kipindi hicho mshahara wa daktari anayeanza kazi ulikua ni mkubwa zaidi ya mshahara wa mwalimu aliyemaliza madaraja yote ya ualimu (nikimaanisha mwalimu aliyeitumikia serikali zaidi ya miaka 35).
  2. daktari anayeanza kazi sasa analipwa 950,000 wakati mwalimu mwenye 'degree' anayeanza kazi analipwa si zaidi ya 500,000.
  3. tukumbuke katika kada za utumishi wa serikali ni madaktari pekee ndio wanaruhusiwa kutumia utaalamu wao nje ya ofisi zao mf. kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri katika ofisi tofauti (najua kunawatakao uliza kuhusu walimu kufundisha tuisheni na kufanya katika shule binafsi, lakini kiukweli ni kwamba walimu hao wanakiuka mkataba wa kazi wa mwajiri wao 'serikali').
  4. tukumbuke pia madaktari ndio watumishi pekee walioruhusiwa kulipwa au kupewa chochote kutoka kwa mtu waliyemuhudumia kwa issue kama consultancy na isihesabike kama rushwa, ndio maana unakuta kuna kibao kimeandikwa KUMUONA DAKTARI NI TSH.****. wakati kwenye kada nyingine hilo ni jambo lenye utata na inahesabika moja kwa moja kama ni rushwa! (ushawahi kuona mwanafunzi kamuuliza swali mwalimu halafu mwalimu akadai pesa???)
  5. Pia tusisahau kwamba madaktari 'Medical Doctors' ndio taaluma pekee ambayo wanaposoma katika chuo kama Muhimbili wanapewa ada na matumizi mengine for free lakini taaluma nyingine wanalipa hiyo mikopo pindi watakapoanza kazi!
  mimi nadhani imefika kipindi madaktari wasifanye vitu kwa utashi wao na kusahau kuwa ni Mungu tu ndiye aliyewapa utaalamu huo na kuwawezesha wafike hapo! tumrudie Mwenye enzi ili atutakase katika hili! kugoma kwenu madaktari mnasababisha vifo vya watu ambao hawana hatia, watu ambao wanategemea vipawa vyenu mlivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu ili muwahudumie wagonjwa. hebu jaribuni kuangalia mnapotupeleka, hivi kweli katika hili Mungu atabariki kazi za mikono yenu???? KWELI KATIKA HILI MADAKTARI HAMTUTENDEI HAKI WATANZANIA!
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Ama Kweli rushwa hupofusha (na kumpa mtu upumbavu -if I may add)! Yaani wee, are you seriously suggesting consultation fee inalipwa kwa doctor personally? Kama unaamini hivyo basi your mental age iko sawa na ya mtoto wa miaka 5. Kwa hiyo tuseme mtu akilipa nauli inakuwa mali ya kondakta? Badala ya kulaumu matokeo kwa nini usilaumu chanzo? Watanzania tunaoteseka kwa maisha magumu yanayosababishwa na CLOWNS waliopo serikalini tunamfahamu na tunamlaumu aliesababisha haya yote na si MADAKTARI. NI SERIKALI hii lege lege, inayoendeshwa kila holela na kishikaji.
   
 3. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye kulipiwa ada naomba uspecify kwamba sio wote waliosoma katika vyuo vya uma...wengine tumepiga private,wengine nje ya nchi na tumelipa kutoka mifukoni mwetu
   
 4. brainiac89

  brainiac89 Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na ndio maana nikasema wanaposoma katika chuo kama Muhimbili nikimaanisha chuo cha umma!
   
 5. brainiac89

  brainiac89 Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi kuna sehemu nyingine katika serikali unalipia huduma ya kushauriwa ni jinsi gani umalize tatizo lako?? hebu fikiri kwa mapana kidogo ndugu!
   
 6. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri madaktari kuhusu huu mgomo wangefikiria upya jamani kuliko kutuua tusio na hatia!Kama ishu ni kutomkubali Dr Mponda na Dr Nkya mimi nadhani kuwazomea na kukataa kuwasikiliza wanapokutana nao kwenye mikutano au majadiliano mbalimbali ilikuwa inatosha kuonyesha hisia zao kwao kuliko kutuua wananchi tusio na hatia!Haki ya mungu itafikia kipindi madaktari watakuwa wanapigwa mawe na raia kwa maamuzi yao haya yasiyokuwa na utu!!Hivi chukulia unauguza mgonjwa hospitali mpaka anakufia mikononi bila kuandikiwa hata panadol ukitoka hapo utamuangaliaje Daktari aliyekuwa kwenye mgomo akagoma kukutibia ndugu yako?
   
 7. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,825
  Trophy Points: 280
  Mungu ndiye atakaye wahukumu. Watu wafe kwa vile hawamtaki wziri. Haiingii kichwani!!!. Naweza nikaelewa kama wanadai mishahara, posho etc ingawa nayo sio sahihi sana maana na kada nyingine zisizo za udaktari nao wana haki ya kuishi.
   
 8. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Pitia upya (kuanzia mwanzo mwa mgomo ule wa mwanzo - zipo threads nyingi tu hapa ukumbini) utajua kiini cha mgomo huu (kama kweli hujui that is - and I doubt it). Naamini upo kazini, which means wewe na wenzako mnafanya juhudi kupotosha ukweli. I can assure you kuwa kama lengo ndio hilo basi you are about ten years too late! Mbinu mnazotumia ni za kizamani na haziwezi kuwa effective zama hizi na kizazi cha sasa!
   
 9. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Zipo, nakutajia chache. BRELA, TIC, Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, niendelee?
   
 10. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Unajitahidi kujenga hoja za UONGO kiasi mtu hasipokuwa makini anaweza kukuamini...hongera kwa hilo. Acha tu tuaninshe ukweli wa baadhi ya uliyodanganya hapo:

  2. Ni ukweli kuwa kada hazilipwi sawa kwa kiwango kimoja cha elimu kama mshahara wa kuanzia. Na hata benefit zinatofautiana..hilo lipo kisheria. Mshahara wa kuandia wa mwalimu mwenye degree, si sawa na mshahara wa kuanzia wa daktari mwenye degree, na si sawa na mshahara wa kuanzia wa mwanasheria, mchumi, mhasibu etc..Kila fani ina jukumu la kuamua thamani yake, na maDakatari hawawezi kuamulia fani nyingine thamani yao, kama mwalimu ameridhika na 500,000 na hadai zaidi, wakati kuna taasisi za serikali mtu mwenye diploma tu analipwa mamilioni...hiyo ni shauri yao! Hata muda wa kusomea degree ya udakatari na ile ya ualimu ni tofauti sana, na kuna sababu ya kufanya iwe tofauti. Daktari akidai anachodhani ni thamani yake, we usipodai ukakalia kubeza juhudi zaker, ni shauri yako!

  3. Huo ni uongo wa mchana kweupee...mfano wa haraka haraka, wanaSheria kutumia utaalamu wao nje ya ofisi. wapo wanasheria wengi wa taasisi za kiserikali wanawakilisha watu binafsi mahakamani. Madaktari si fani pekee inayofanya hili.

  4. Huo ni uongo dhahiri pia...narudia mfano wa wanaSheria ambao nao wanatumia utaalamu wao nje ya ofisi kutoa ushuri wa kisheria pamoja na huduma nyingine (mafano certification ya documents, mihuri etc). Na wanajitangaza, na consultation fee yao wanajipangia wenyewe..madaktari si fani pekee inayofanya hili.

  5. Huo ni uongo wa kipuuzi kabisa...HESLB mwezi uliopita ilitoa list ya wadaiwa sugu...madaktari wapo kweny hiyo list (inapatikana online, itafute kwa faida yako). Mimi nalipa deni langu tangu mwaka 2009, na uthibitisho mwengine ni kuwa iliandikwa mpaka kwenye magazeti watoto wa rais JK nao ni wadaiwa sugu (Ridhiwani na Salama), Salama Kikwete ni daktari amesoma Muhimbili na anadaiwa. Kwa hiyo madaktari wanakopeshwa na wanalipa/wanapaswa walipe deni lao HESLB kama wadaiwa waliosoma fani nyingine.

  Kama unataka kuweka hoja..tumia facts kufanya hoja yako iwe na mashiko, na sio kulazimisha ionekane na mashiko kwa kubandika uongo hapa!
   
 11. E

  Edo JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ndugu zangu hakuna anayepinga ninyi Madokta mna madai yenu ya msingi, lakini kweli kwa wingi wenu na usomi wenu(kiapo mmeweka pembeni) hamuwezi kutafuta mbinu nyingine za kupambana na serikali mpaka mtumie human shield? Hata katika vita taratibu za kimataifa zinakataza kutumia kinga ya binadamu! Tuoneeni huruma jamani, fikirieni silaha nyingine katika vita hii yenu na serikali- you are top brains! Chondechonde hebu fikirieni tena approaach nyingine iliyo salama kwetu sisi ndugu zenu tusioweza kwenda appolo na kwingineko.
   
 12. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nafikiri sasa umefika wakati Serikali kufikiria kuongeza subsidy/ruzuku kwenye HOspitali binafsi ili waweze saidia wananchi wengine wa kipato cha chini na kuachana na Hospital za Serikali. Serikali ibake na Hospital kubwa kwa akili ya Research na Development of capacities kwani hata Madaktari wakiwa hawako kwenye migomo huduma pia haziridhishi. najua wengi hapa mtapinga kwa sababu mnazozijua wenyewe.
  Mfumo wetu wa kunttayarisha Daktari toka la kwanza mpaka kwenye iternship kwa sasa sio mzuri. Migomo inaanza toka masomo yanaanza. Jana wengine wameenda na kushinda nje Wizarani kudai pesa za chakula hakuna chuoni sasa huyo mtu atakuwa daktari wa aina gani mpaka amalize kozi atakuwa amepata misukosuko mingapi na akili yake towards Government itakuwa vipi?
  Swala hili ni kubwa kuliko linavyochukuliwa kishabikishabiki. Hii iahitaji mjadala mpana wa kitaifa Serikali peke yake hawataweza kusolve. Kinachihitajiak ni suluhisho la muda mrefu.
  Mimi naamini kabisa leo hii wakitimiziwa madai yao kama mfumo utabaki huu haitapita mwaka mwingine bila ya kuwa na mgogoro mwingine.
  Ushauri wangu: Madaktari rudini kazini saidieni Ndugu zenu na huku Sisi Wanachi tukitafuta njia ya kuweka mjadala wa kitaifa juu ya swala hili.
   
 13. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Nyie ndio vibaraka, nenda nawe ukasome ulipiwe ada kama unadhani ni rahisi kusomea udaktari. Umekurupuka na kujiunga JF ufanikiwe kufanya ukibaraka siyo? Hao madaktari uwasemao ndio wametendewa haki ipi?
   
 14. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,304
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  I'm not a Doctor but I think I also shouldn't be pessimistic on their strategy, katika kudai haki na kuondoa ukandamizaji kuna sacrifices fulani, I'm sorry its the poor sickmen to suffer, lakini ukweli nimekukumbuka kwamba most of us died the next second after receiving khanga and tshirts.
   
 15. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kwani mafisadi huwa hawaapi mpaka wasifuate viapo vyao? Au ni madaktari tu ndio wanatakiwa kufuata viapo?
   
 16. brainiac89

  brainiac89 Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo ni rushwa! BRELA unalipia nn?
   
 17. brainiac89

  brainiac89 Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe hilo ndio tatizo lenu?? ugomvi wenu na wanasiasa mnawaua wananchi!!! this is very unfair! jiangalieni kwa upya, kwa kuruhusu roho za wasio na hatia kufa kwa sababu ya mambo yasiyo na msingi kamwe baraka katika kazi ya mikono yenu itakua ndoto
   
 18. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  1. Ndio maana huyu kaitwa Mwalimu na Yule kaitwa Daktari. Kila mtu ana umuhimu wake. Kila mtu anajua thamani yake.
  2. Hizo figure umekopi kwa Pinda? Unajua take home ya sh. 950,000/= ni sh. ngapi? Na kwanza hizo figure za mboga unaziona kwako ni kubwa sana nini? Au unadhani ni dola?
  3. Kwani afisa kilimo hajaruhusiwa na serikali kuwa na shamba lake? Daktari tu ndio nongwa?
  4. Una IQ ya kutosha kuweza kujua walau kaneno consultation fee? Mbona iko kila mahala? Kwa engineer, madaktari na fani nyingine. Kwa madaktari consultation fee ina range kati ya 10,000-20,000 wakati consultation fee kwa wengine ni millions of dollars. Unajua Iddi Simba alisema alikuwa anamdai Robert Kisena consultation fee ya kiasi gani? Wewe unadhani unapoongea na daktari mnakuwa mnapiga story tu? Kama fani yako haina consultation fee basi pole sana.
  5. Porojo porojo hizo zilisababisha ushindwe masomo ya Science. Unaandika porojo kama waandika insha. Nani kakudanganya kuwa madaktari wamesomeshwa bure? Nenda mtandao wa HESLB uangalie wadaiwa toka Muhimbili Chuo na UDSM ambao walikuwa wanasomea udaktari.
   
 19. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Mwanao anapokimbia masomo ya Kemia,Biolojia na Fizikia nawewe ukakenua meno unategemea daktari atatoka wapi?
   
 20. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Maneno hayo...Ngumu kumesa aisee!
   
Loading...