Katika Hili la Sakata la ESCROW Watanzania Tusiilaumu CCM tujilaumu wenyewe.

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
Nadhani sasa tumeshadhibitisha kuwa watu tuliowapa dhamana walinde rasimalali zetu ndio wamakengeuka na kuwa wezi wa rasilimali zetu. Hakuna shaka lolote kuwa CCM jana imeliweka hili bayana kwa mara nyingine. Watu wamepambana toka juzi kuweka facts mezan hadi kikaeleweka. In fact haikuwa rahisi kufikia hatua ya kuanza kupitisha maazimio.

Mwanzo kabisa, uhuni wa kutaka kuzuia sakata hili ulianzishwa na mahakama kutaka kuzuia mjadala bungeni, watu wakakomaa tukavuka. Uhuni wa Pili ukaja pale Kiti kiliporuhusu wezi kuwasilisha utetezi ulioitwa kauli ya serikali, Hapa wezi walitaka kuuaminisha umma kuwa hawajaiba, hapo pia tukavuka kwa kuwavua nduo had za ndani wezi hawa. Tukaendeea hadi wakati wa Maazimio, Hapa ndipo shetani CCM ilipojiinua na kuonesha dhamira yake ya kweli katika sakata hili.

Watu wengi sana walitoa formulation kwa spika ila hakuzikubali, inaonekana alikuwa anataka fomulesheni inayotoka kwa mwinzi mmoja wapo maana alipotaja mwizi tu ghafla huyu mama akaamuru bunge liipigie kura fomuleshen hiyo na kuzisahau kabisa fomuleshen za awali.

Kwa kilichofanywa na Mbowe ni kitendo ha kishujaa ambacho wazalendo wote walipenda kitokee. Tusinge weza kupitisha adhabu yoyote zaidi pale maana wezi walitamalaki na kuachiwa nafasi ya kujitungia adhabu. Yani Jizi kama Werema bila aibu yoyote jamani linasimama kumkingia kifua mwizi mwenzake wakati kamati imeshapendekeza asimamishwe kupisha uchunguzi ambao ni utaratibu wa kawadida kabisa ktk hatua hii tulofikia. Werema yeye ndo mchunguzi had aseme Maswi hana Kosa? Kwa hili CCM hamtabaki kuendelea kutuibia kiasi hiki.

WAY FORWARD

Kutokana na kilichoshuhudiwa jana na watanzania, Chonde chonde watanzania wenzangu, nendeni mkajiandikishe uchaguzi wa serikali za mitaa. Ili tuonyeshe hisia zetu kupitia kura zetu. Tena inapaswa tumshkuru mungu kwa kuonesha haya siku ya jana kwani leo ndio deadline ya kujiandikisha kwa uchaguzi wa serikali za mitaa. Shime ndugu zangu, lets take actions humu tumeshalalamika sana. Its time to act.

Pia jitahidi kuhamasisha familia yako na watu wengine at least kumi kila mmoja ili akajiandikishe na hatimaye kupiga kura ya kuondoa wezi madarakani. Tafadhari ndugu zangu, dharau iliyooneshwa jana inatokana na uzoefu uliojengwa kipindi kirefu kuwa watanzania ni wasahaulifu na ni wagumu kuchukua hatua. Katika hili tuchukue hatua na inapaswa tusiilaumu CCM kwa uhuni huu bali tujilaumu wenyewe kwa kutokufanya maamuzi kupitia kura zetu.
 
Back
Top Bottom