Katika harakati zake Bwana Yesu ni wapi aliwahi kusababisha mauaji ya wafuasi wake?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,635
218,067
Nimepata kusoma mahali fulani kwamba Yesu Kristo alifundisha neno la Mungu, aliponya wagonjwa na kufufua waliokufa, lakini sijawahi kusoma popote ambapo imeandikwa kwamba aliwahi kusababisha mauaji iwe ya kimbari ama ya watu kadhaa.

Hata hivyo, mimi si mjuzi sana wa mambo ya Biblia na wala sijui sana habari za Yesu. Hivyo basi, ninawaomba wenye ujuzi na uelewa mpana wa habari za Yesu Kristo watusaidie kufafanua.

Naomba kuwasilisha.
 
Kwanza ungejiuliza hivi ni lini alitumia mafuta ya upako

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
Yesu alitumia hadi mate na matope kuponya ingekuwa leo mtu anafanya hivyo watu wangemshambulia hadi basi

Yesu Amponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu

YOH 9:1-7
Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. 2 Wanafunzi wake wakamwuliza, “Bwana, ni nani aliyetenda dhambi ya kusababisha mtu huyu azaliwe kipofu, ni yeye au wazazi wake?”

3 Yesu akawajibu, “Huyu hakuzaliwa kipofu kwa sababu yeye au wazazi wake walitenda dhambi. Jambo hili lilitokea ili nguvu za Mungu zionekane zikifanya kazi katika maisha yake. 4 Yatupasa tutende kazi yake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana kwa maana usiku unakuja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. 5 Wakati nipo ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.”

6 Baada ya kusema haya, akatema mate kwenye udongo aka tengeneza tope kwa mate yake akampaka yule kipofu machoni. 7 Kisha akamwambia, “Nenda kanawe uso katika kijito cha Siloamu.” Neno ‘Siloamu’ maana yake ni ‘aliyetumwa.’ Yule kipofu akaenda akanawa na akarudi akiwa anaona
 
Yesu alitumia hadi mate na matope kuponya

Yesu Amponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu

YOH 9:1-6
Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. 2 Wanafunzi wake wakamwuliza, “Bwana, ni nani aliyet enda dhambi ya kusababisha mtu huyu azaliwe kipofu, ni yeye au wazazi wake?”

3 Yesu akawajibu, “Huyu hakuzaliwa kipofu kwa sababu yeye au wazazi wake walitenda dhambi. Jambo hili lilitokea ili nguvu za Mungu zionekane zikifanya kazi katika maisha yake. 4 Yatupasa tutende kazi yake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana kwa maana usiku unakuja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. 5 Wakati nipo ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.”

6 Baada ya kusema haya, akatema mate kwenye udongo aka tengeneza tope kwa mate yake akampaka yule kipofu machoni. 7 Kisha akamwambia, “Nenda kanawe uso katika kijito cha Siloamu.” Neno ‘Siloamu’ maana yake ni ‘aliyetumwa.’ Yule kipofu akaenda akanawa na akarudi akiwa anaona

Umejibu vyema mkuuu,ila huyu hatuwezi kumwita yesu wa uhongo mana yeye ndo manabii wa uhongo wanatumia jina lake kutuminisha Mafuta yao ya upako kuwa yanamiujiza ya Yesu mponyaji.
 
Mwana wa adamu alikuja kuokoa sio kuua watu!!!Watu walijazana sana kwenye mikutano yake na hakuna rekodi ya mtu hata kuzimia tu!!!Hawa waliopo nhj wauaji tu tena wachumia tumbo!!
 
Yesu alitumia hadi mate na matope kuponya ingekuwa leo mtu anafanya hivyo watu wangemshambulia hadi basi

Yesu Amponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu

YOH 9:1-7
Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. 2 Wanafunzi wake wakamwuliza, “Bwana, ni nani aliyetenda dhambi ya kusababisha mtu huyu azaliwe kipofu, ni yeye au wazazi wake?”

3 Yesu akawajibu, “Huyu hakuzaliwa kipofu kwa sababu yeye au wazazi wake walitenda dhambi. Jambo hili lilitokea ili nguvu za Mungu zionekane zikifanya kazi katika maisha yake. 4 Yatupasa tutende kazi yake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana kwa maana usiku unakuja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. 5 Wakati nipo ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.”

6 Baada ya kusema haya, akatema mate kwenye udongo aka tengeneza tope kwa mate yake akampaka yule kipofu machoni. 7 Kisha akamwambia, “Nenda kanawe uso katika kijito cha Siloamu.” Neno ‘Siloamu’ maana yake ni ‘aliyetumwa.’ Yule kipofu akaenda akanawa na akarudi akiwa anaona
Huyo ni yesu mwenyewe, je hawa wanaojiita manabii ndio yesu mwenyewe, wana nguvu sawa na yesu mwenyewe? Kumbe ndio maana wanatumia hadi JIK

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Nijuavyo Mimi Nabii sikuzote huwa anajua litakalotokea mbeleni sasa cha kushangaza huyu nabii feki alishindwa vipi kujua kitakachotokea mbele?
Sikuzote anajifanya kuwatabiria watu matatizo Yao na maisha Yao ya baadae lakini kujitabiria mwenyewe ameshindwa ndiyo maana wenye akili tunajua Ile ni KAFARA tu
 
Back
Top Bottom