Katika demokrasia chama cha siasa huwa tegemezi, hakimiliki mali, rasilimali au madeni.

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,527
46,055
Mfumo wa demokrasia unaojumuisha ushindani wa vyama vingi tunaoupigia chapuo katika nchi yetu asili yake hasa ni magharibi.

Katika demokrasia halisi vyama vya siasa huwa ni vyombo vinavyokuwa tegemezi kabisa kupitia hisani au ufadhili wa wanachama wake, wapenzi au "interest groups" kama vyama vya wafanyakazi n.k

Hapa Tanzania CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani kimekuwa kinatupiwa shutuma, vijembe na kejeli sana kuhusu kukosa vitega uchumi vyake binafsi vya kuingiza mapato katika chama. CDM wako sahihi kutegemea michango ya wanachama na siku wakijiingiza kufanya biashara za kudumu ndio itakuwa wamekizika chama chao kutoka kuwa chama kinachoongozwa kwa maoni ya wananchi na kitapoteza imani kwa watu wengi.

Kwa nini ni tatizo kubwa kwa chama cha siasa kuwa na mali, rasilimali na vitega uchumi vyake binafsi?

Sababu ya kwanza; Hakitasikiliza maoni ya walio wengi kwa sababu kinajua kitapata tu fedha na rasilimali za kujiendesha kupitia biashara zake na vitega uchumi vya kudumu.

Sababu ya pili; Kitakuwa kinavutia watu wengi ambao hawana interests na siasa au itakidi ya chama ila wana shida ya kupata mshahara tu kama kazi nyingine. Matokeo yake ni kuwa na vilaza wasiojua kujenga hoja bali wanapigania kubaki madarakani hata kwa nguvu na udhalimu mkubwa siku zote.

Sababu ya Tatu; Kuhamahama vyama kusikoongozwa na itikadi au sera. Hii sio afya kwa demokrasia kukomaa.

Vyama vya siasa katika demokrasia komavu za magharibi huwa vinajiendashaje ?

Katika nchi kama Uingereza au Marekani vyama vya siasa huwa vinaendeshwa kwa michango ya watu tu, wanachama na wasio wanachama wanaovutiwa na sera katika kipindi husika. Kupata mchango mkubwa kupitia wanachama wengi waliochangia kidogo kidogo hutumika kama kiashiria cha kukubalika kwa mgombea katika uchaguzi.

Consertives, Labour Party, Democrats na Republicans hawana rasilimali zozote, vitega uchumi wala biashara za kudumu za kuingiza mapato katika vyama.
Wanategemea michango ya wanachama wakati wa uchaguzi kuendesha vyama vyao. Vyama vya kikomunisti kama cha China, Cuba na Korea Kaskazini ndivyo humiliki mali na kuwa na vitega uchumi vyake binafsi.

Demokrasia ina tamudini zake, tujifunze na tuendane nazo kama tunadai sisi ni wanademokrasia.
 
Uchambuzi murua, ipo siku Watanzania wataamua Mali zote za CCM ilizizipata kwa mlango wa nyuma kuzirejesha kwa umma.
 
1648885745250.png
 
Nimekusoma vizuri ila umeniacha njia panda. Kwangu chama kuwa na uwezo wa kujiendesha ni moja kati ya silaha kuu itakayokifanya kitimize majukumu yake ya kisiasa vizuri na kwa wakati.

Hapa ndipo hutakiwa chama kiwe na vyanzo vyake vya mapato, vijue namna vitakavyokusanya fedha zitakazokiwezesha kugharamia shughuli mbalimbali kama kusafirisha wagombea wakati wa uchaguzi, kulipa mishahara, na mahitaji mengine.

Sasa unaposema chama cha siasa kinatakiwa kiwe tegemezi maana yake unataka chama kife kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake, wafanyakazi wakose mishahara, na mengine, hii kwangu sio sifa, ni kuua chama.

Chama kushindwa kujitegemea ndio mwanzo wa wanachama wake kuanza kununuliwa kama karanga mtaani, na hili linadhoofisha harakati za ukombozi kwasababu hao wanaonunuliwa huko waendako mara nyingi huenda kuwekwa mfukoni hawasemi chochote.
 
Uwezo wa kujiendesha wa chama unatakiwa utokane na michango ya wanachama wake. Kama chama hakiwezi kupata michango ya kujiendesha kutoka kwa wanachama kinatakiwa kife.

Hakuna chama kinaweza kufanya siasa na biashara kwa pamoja na bado kikaendelea kuwa chama makini.

Ukiondoa mwenyekiti Taifa, Makamu na Katibu Taifa na viongozi wengine wachache sana ngazi ya taifa Chama hakitakiwi kiwe na wafanyakazi wa kudumu kama serikali, kampuni au Ngo, wengi wa viongozi wa chama wanatakiwa wawe watu wenye shughuli zao binafsi na kazi yao katika chama iwe ni ya kujitolea hivyo suala la mishahara halitakiwi liwe issue.
Nimekusoma vizuri ila umeniacha njia panda. Kwangu chama kuwa na uwezo wa kujiendesha ni moja kati ya silaha kuu itakayokifanya kitimize majukumu yake ya kisiasa vizuri na kwa wakati.

Hapa ndipo hutakiwa chama kiwe na vyanzo vyake vya mapato, vijue namna vitakavyokusanya fedha zitakazokiwezesha kugharamia shughuli mbalimbali kama kusafirisha wagombea wakati wa uchaguzi, kulipa mishahara, na mahitaji mengine.

Sasa unaposema chama cha siasa kinatakiwa kiwe tegemezi maana yake unataka chama kife kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake, wafanyakazi wakose mishahara, na mengine, hii kwangu sio sifa, ni kuua chama.

Chama kushindwa kujitegemea ndio mwanzo wa wanachama wake kuanza kununuliwa kama karanga mtaani, na hili linadhoofisha harakati za ukombozi kwasababu hao wanaonunuliwa huko waendako mara nyingi huenda kuwekwa mfukoni hawasemi chochote.
 
Vyama vya kikomunisti kama cha China, Cuba na Korea Kaskazini ndivyo humiliki mali na kuwa na vitega uchumi vyake binafsi.
"Humiliki mali na kuwa na vitega uchumi vyake binafsi" Kama vipi hivyo ?
 
Back
Top Bottom