Katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2024/2025, watafuta tozo zote huku wakidai Serikali yao ni sikivu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Hawa watu wanajua uchaguzi bado uko mbali na ndio maana wanafanya yote haya licha ya kelele zote zinazopigwa na msitarajie watabadili chochote katika kipindi hiki(wakibadili, basi ni kidogo sana).

Watachofanya ni kusubiri Bajeti ya kuelekea mwaka wa uchaguzi(Bsjeti ya 2024/2025) ndio watakuja kufuta hizo na kuwaambia serikali yenu sikivu imesikia kilio chenu cha muda mrefu na wabunge hawa wa CCM watagonga meza na kuimba: "CCM,CCM,CCM".

Tukiendelea na hii tume ya uchaguzi ilippo,2025 watarudi tena madarakani na tozo hizi(zote au baadhi) watazirudisha tena na watawaka watanzania kuwa wavumilivi kwani wanajenga nchi na maneno au porojo nyingine za aina hiyo.

Ukweli nii kwamba, utawala wa Mwendazake uliingiza nchi katika miradi mingi na mikubwa kuliko uwezo wa nchi na pasipo kuwa na mikakati wala mipango ya muda mafupi na mirefu ya namna gani wangepata fedha za kukamilisha hiyo miradi na haya ndio matokeo yake japo hawawezi kukiri hadharani.

Jiiulizeni baada ya kuanzisha miradi yote hii, walikuja na vyanzo gain mahususi vya mapato vya kugharamia hiyo miradi wakati Bajeti yenyewe miaka yote haitoshelezi na inategemea mikopo na misaada kutoka kwa nchi wahisani?

Nimekumbuka ya plea bargain,watu kuporwa fedha zao katika mabenki, wenye maduuka ya fedha za kigeni kuporwa fedha zao na mengineyo bila kusahau ya Sabaya na aliowataja mbele ya Pilato kuwa walikuwa wanajua aliyokuwa akiyafanya.

Tuombe uzima tu kufika hiyo 2024 kuelekea 2025.
 
Wanaupiga mwingi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaa , mingine tena kwao jameniiii, kwa sauti ya Uhuru Kenyatta, kimsingi maarifa yao ndio yameishia hapo jiandaeni kwa kodi hadi za kupumua mambo ni mengi sana , wataanza hadi kuingilia kazi za Muumba hawa ni suala la muda tuu na hivi wako peke yao kule kwenye jengo, huku mtaani lieni tu machozi yenu yatakauka na mtaendelea kuwa wanyonge, kwani shing ngapi bana ,wanyonge woyeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Mwanzo sikuelewa Mwigulu aliposema suala la mtu kuhamia Burundi, nilidhani ni issue ya utani ila sasa maana halisi ya tamko lake imeanza kujidhihirisha!
 
Back
Top Bottom