Katika awamu hii chini ya Rais mpya Malawi, Magufuli atumie fursa hii kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania

Hapana, kwa kuwa kwa maoni yako Kikwete angeweza kumtuma waziri wa vijana na utamaduni kwenda kujifunza masuala ya uchumi.

Na hivi kwa akili yako, Kikwete angetaka kumtuma waziri kujifunza masuala ya uchumi, angemtuma nchi ya Rwanda, ambako pia alikuwa na mgogoro na Kagame? Unaona Rwanda ndio ilikuwa nchi ya kuifundisha Tanzania masuala ya uchumi wakati huo?
Social and economic issues lazima awe waziri wa fedha?
 
Pumbavu wewe, lini Mwandosya alitatua mgogoro wa Rwanda na Tanzania?

Tanzania ilipeleka majeshi yake Drc na waasi wa M23 waliokuwa wanadhaminiwa na Rwanda walifurushwa.

Unatoa mifano ha kipuuzi, koplo wa siasa ndio nini?
Kuna watu wengine wanaropokaropoka kama Mwandosya ni ndugu yako nenda kamsalimie lakini sio kutusndikis utopolo
 
Hili tatizo la mpaka kati ya Tanzania na Malawi hadi leo halijatatuliwa. Suala ni kwamba, kuna dalili za mafuta ndani ya Ziwa Nyasa, ambalo Malawi wanaliita Ziwa Malawi. Na suala la uwezekano wa mafuta lilizua upendezi mpya wa ziwa kwa Malawi wakasema kwamba mpaka kati ya Tanzania na Malawi siku zote umekuwa mwisho wa ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania, yaani ziwa lote liko ndani ya Malawi.

Tanzania wakasema hakuna kitu kama hicho. Siku zote mpaka ni mstari wa katikati ya ziwa ili kutenganisha Malawi na Tanzania, na hiki ndicho kinachokubalika kimataifa kunapokuwa na maji makubwa kati ya nchi mbili. Malawi hawakukubaliana na msimamo wa Tanzania, na wakadai wataweka watafiti wa mafuta ndani ya ziwa lao (Nyasa). Tanzania ikawaambia Malawi watafiti hao wakiingia upande wa Tanzania watakiona cha mtema kuni.

Marais wa Malawi waliopita walikuwa na msimamo mkali kuhusu ziwa Nyasa wakidai ziwa lote liko Malawi na hata walitumia jambo hili katika kampeni zao. Sijui msimamo wa huyu raisi mpya wa Malawi ukoje. Mgogoro huu ulikuwa usuluhishwe na SADC na Thabo Mbeki na Joachim Chisano walipewa jukumu la kuutatua. Sijui ripoti yao iliishia wapi, au kama waliweza kumaliza kazi yao.

Huko nyuma niliwahi kupendekeza humu JF kwamba jambo kubwa linalofanya kuwe na mgogoro wa mpaka ni mafuta ndani ya ziwa Nyasa. Nikapendekeza kwamba, kwa nini Tanzania wasikubaliane na Malawi kwamba mafuta yote yatakayopatikana ndani ya ziwa Nyasa uwe mradi wa pamoja kati ya Tanzania kwa kugawana 50:50? Sijui kama kuna walionisikiliza.

Sasa basi, kwa kuwa tuna Rais mpya Malawi, ambae ameonyesha ukaribu na Magufuli, ushauri wangu kwa Magufuli ni kutumia fursa hii kumaliza hili suala la mpaka wetu na Malawi. Nachela tusipolimaliza sasa huko mbele linaweza kuja kuzaa vita kati ya Tanzania na Malawi.

Mambo ya vita yamepitwa na wakati. Wanajeshi siku hizi hawapigani wanajenga madaraja na kujenga nyumba nk. Rais Magufuli hebu ongea na Rais wa Malawi tumalize jambo hili na kuanza kutumia hayo mafuta kujenga SGR, Stiegler Gorge, flyovers, lami hadi vijijini, nk, tuifanye Tanzania kama Ulaya!

Angalia pia;

  1. Nafurahi Kuona Mediators Wanafikiria Kama Nilivyoshauri Humu JF Kuhusu Mgogoro wa Malawi Tanzania
  2. Suluhisho la mgogoro na Malawi ni hili; sio suala la ziwa wala mpaka
zipigwe kwanza mshindi achimbe mafuta
 
Ingekuwa enzi zile ningekuambia unauliza jibu, maana nadhani angalau una akili ya kutosha kujua waziri wa fedha Tanzania ndio anashughulikia mambo ya uchumi pia!😛
Huna lolote hoja zako unaziibua kwa hisia tu, na ufahamu mdogo kujifanya unajua.
 
Huna lolote hoja zako unaziibua kwa hisia tu, na ufahamu mdogo kujifanya unajua.
Njoo unikosoe, kuna thread nyingine nimeanzisha

 
Back
Top Bottom