Katibu wa uhamasishaji na chipukizi UVCCM taifa, Victoria Mwanziva akutana na wahamasishaji UVCCM ngazi ya tawi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,858
930
KATIBU WA UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI UVCCM TAIFA CDE. VICTORIA MWANZIVA AKUTANA NA WAHAMASISHAJI UVCCM NGAZI YA TAWI

27.03.2022 - Dar-Es-Salaam

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Cde. Victoria Mwanziva ashiriki Darasa la itikadi Tawi la UVCCM Msakuzi Mashariki - Kata ya Mbezi - Wilaya ya Ubungo - Mkoa wa Dar - Es - Salaam.

Cde. Victoria Mwanziva amewafunda vijana wa Hamasa katika darasa la Itikadi lilioandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Msakuzi; akiwasihi kujidhatiti ya kwamba hamasa ya kukipigania Chama huanzia ngazi ya Tawi; kwani huko ndiko kwenye wanachama wengi.

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Cde. Victoria Mwanziva amewasihi Vijana wote wa UVCCM; Kuendelea kutembea kifua mbele kusemea mambo mazuri na makubwa yanayofanywa na Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa taifa letu la Tanzania.

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Cde. Victoria Mwanziva aliambatana na Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Mkoa wa Dar - Es - Salaam Cde. Eng Ally Ummiy - na Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mbezi Mary Biita katika tukio lililoandaliwa na Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Msakuzi Mashariki Cde Noel Kapinga ambaye alikuwepo na viongozi wa Tawi na Kata wa Chama na Jumuiya.

VIJANA JEURI YA CHAMA

IMG-20220328-WA0004.jpg


IMG-20220328-WA0009.jpg


IMG-20220328-WA0007.jpg


IMG-20220328-WA0008.jpg
 
Nchi ina vijana wapenda siasa alafu mnataka kuwafikaa wazungu aiseee

Dada kapata msaada wa kusoma nchi za nje kachindwa kutengeneza fursa kwenye mambo mbalimbali.

Nonsense kabisa.
 
Nchi ina vijana wapenda siasa alafu mnataka kuwafikaa wazungu aiseee

Dada kapata msaada wa kusoma nchi za nje kachindwa kutengeneza fursa kwenye mambo mbalimbali.

Nonsense kabisa.
Badala ya kulea ndoa yake kutwa anatafuta uteuzi
 
Nilipokuwa chuo huu unafiki wa kujiunga UVCCM ulinishinda
Watu walikuwa wanazipigania kadi eti watapewa ajira leo hii tupo nao kitaa tunakula vumbi
 
Back
Top Bottom