Katibu wa Mufti Zanzibar (Sheikh Soraga) amwagiwa tindikali

silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,161
1,535
Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema Sheikh Soraga amemwagiwa tindi kali na watu wasiojulikana asubuhi ya leo wakati akiwa katika mazoezi.

hivi sasa inasemekana yuko njiani kuelekea Dar kwa matibabu.

Sheikh Soraga ni pro-government na ni 'critic' mkubwa wa Uamsho. Katika hotuba yake ya Sala ya Iddi, aliiponda sana jumuiya hii. Sasa whether there is causal relationship between the two, ni kazi ya vyombo vya dola kung'amua

-------------------UPDATE-----------------------


Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akipandishwa kwenye Gari ya Wagonjwa kwa lengo la kuwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Wananchi mbalimbali wakishuhudia Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akiwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.


Imewekwa na MAPARA at 10:30 AM
 
Katibu wa muft wa UAMSHO SHEKH FADHIL SORAGA AMEMWAGIWA TINDIKAL NA WATU WASIOJULIKANA ASBUH HII HUKO ZANZBAR NA HALI YAKE NI MBAYA AMESAFIRISHWA KUPELEKWA MUHIMBILI MUDA HUU SOURC FB WALL YA UAMSHO
 
Mwisho wa siku tutawajua perpetrators wote kwa sura zao!
Kama nchi yetu ni Dola kwanini vikundi vya wachache waiendeshe dola nzima?
Akikamatwa mmoja ni kumchinja ndio wataogopa!
 
Katibu wa muft wa UAMSHO SHEKH FADHIL SORAGA AMEMWAGIWA TINDIKAL NA WATU WASIOJULIKANA ASBUH HII HUKO ZANZBAR NA HALI YAKE NI MBAYA AMESAFIRISHWA KUPELEKWA MUHIMBILI MUDA HUU SOURC FB WALL YA UAMSHO
Soraga ni katibu wa mufti wa Zanzibar,hana uhusiano na
Jumuiya ya UAMSHO,
 
Yale yale ya MWL Mkianza kubaguana mtabaguana hadi mwisho.
So now kuna vikundi ndani ya wao, dhambi ya ubaguzi imeanza kuwala hawa.
 
Baada ya kuchoma makanisa wameamia sasa wao kwa wao..

Wazee wa tindikali wameanza!!! Unajua hii dhambi ya chuki waliyoippanda huwa inawasumbua sana. Sasa walichinja yule koplo Said, leo tindikali kwa sheikh!!!! Huu ni mfano hai, angalia kinachotokea Syria, kilichitokea Lebanon, angalia yanayotokea Sudan, Somalia et al. Its better to preach peace rather than cowardness!!! Mbaya sana. Kwa kweli visasi ni vibaya sana, yani mtu ukizoea kuishi kwa visasi haya huwa matokeo yake maana na wale wafuasi wa huyo sheikh nao watamsaka aliyefanya hilo tendo na kumchinja sijui, then itakuwa malipizano tu!! Watu mnaishi kama wanyama bana! Mungu awjaalie hekima na busara sio maliizi.
 
Back
Top Bottom