Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro Aachia Ngazi and Soon to Defect to ....

Nipo morogoro hoja yake kubwa anasema amejiona anatumikia chama ambacho kinaendeshwa kikabila zaidi,pia wale ambao wa kabila hilo na waliopo na kabila hilo wanasikilizwa zaidi,amebanwa na mwandishi ataje hilo kabila amesema wandishi wajue tu chadema ipo kikabila zaidi na amewalaumu wandishi wa habari kufumbia macho ukabila wa chadema,anaonekana ana wasi wasi sana!
Hawa wachaga kumbe kabila hatari sana, kumbe mpaka Morogoro wapo wachaga pia?
 
yeye alijua CHADEMA wanatania kutaka kuongoza nchi.mpuuzi kweli huyo hawezi kuhimili kasi ya M4C.!
 
Nahisi kwa kushirikiana na Nape na Nchemba walikuwa wanapanga ule mpango wa kuvuruga mkutano wa CHADEMA hapo Morogoro sasa anaona haya baada ya dili kushtukiwa na Dr. Slaa.
 
Kwani mwenyekiti wa chadema ni nani na Kabila gani nadhani tunaweza tukaanzia hapo
 
Huyo ni unyoya mmoja tu kwa jogoo lenye manyoya milioni kedekede. Nape ataambulia hao vibaraka wake tu lkn sisi wazalendo kama Kasulumbayi tunazidi kujitolea kujenga chama.
daaa jamanii hiyo nnn kinatoke kwa cdm tena au ndio nape na mwigulu wamefanikiwa lengo lao la kubomoa ngome ya chadema
 
Mi nilijua tu hii M4C haiwavurugi CCM na washirika wao tu bali kuna makapi mengine hata ndani ya CDM yameshavurugwa na ndo haya tunayoyaona leo na bado tutandelea kuyashudia
 
Hapa Tanzania tatizo kubwa ni utendaji usio na tija kukubalika na wengi. Tuna utamaduni huu ambao unaligarimu taifa. Ukiangalia sana hasa public sector hakuna kipimo cha utendaji hata kama mwajiriwa ana hadidu rejea za kazi. Hiyo ni style ya CCM na serikali yake. Alidhani CDM wanaafiki hali hii. Kama alikuwa na agenda nyingine ya kuihujimu CDM, ni mjinga sana kwani kwa kufanya hivyo kanaswa mapema. CHADEMA haihitaji uchafu kama huu wajiengue wote wa aina hii kabla hawajaunguzwa na huu moto mkali wa M4C.
 
Quote from DT125
Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, ameachia ngazi!.

Katibu huyo, (jina litafuatia), ameachia ngazi rasmi kwa kuitisha press conference iliyomalizika soon mjini Morogoro!.

Katibu huyo ametoa sababu kuu za kuachia ngazi, ni sintofahamu kati yake na Mwenyekiti wake, Mhe. Susan Kiwanga kuhusiana na lengo la M4C!.

Kwa mujibu wa mtoa habari wangu, Katibu huyo ameanza rasmi ubomoaji wa Chadema kwa aliyoyazungumza
na nimeona sii bora kusema alichosema, bali nitawawekea hapa soon!.
Bila shaka itakuwa anatumiwa na magamba kuivuruga CHADEMA kama ilivyotokea kwa aliyekuwa Mwenyekiti wetu Mgesi mwaka 2005 aliyehamia CCM gafla wakati kampeni za uchaguzi mkuu zilipokuwa zinaendelea.
Magamba wengi walifikiri hatua ile ingekiua kabisa chama, lakini kinyume chake CHADEMA imeimarika kabisa mkoani hapa. Kupambana na CHADEMA ni kupambana na umma kwa hiyo wanaojisumbua kuihujumu CHADEMA popote wataishia kuaibika. A luta continua!!!!
 
Alichofanya huyu Bwana ni kujisalimisha tu na kujenga historia yake. Juzi usiku nafasi aliyokuwa nayo ya Mwenyekiti wa Morogoro vijijini ilijazwa baada ya viongozi wapya wa Kata waliochaguliwa katika Vuguvugu kukutana pale Mount Uluguru hotel na kuchagua Task force ya kukijenga Chama. Kwa hiyo kilichokuwa kinafuata ni nafasi ya Ukatibu aliyokuwa amebakiwa nayo. Pia huyu Bwana tangu Operesheni Sangara imeanza tarehe 08/08/2012 hajashiriki katika kitu chochote

Ila tuthamini hata hicho kidogo alichochangia haitampotea kamwe thawabu yake.
 
Nipo morogoro hoja yake kubwa anasema amejiona anatumikia chama ambacho kinaendeshwa kikabila zaidi,pia wale ambao wa kabila hilo na waliopo na kabila hilo wanasikilizwa zaidi,amebanwa na mwandishi ataje hilo kabila amesema wandishi wajue tu chadema ipo kikabila zaidi na amewalaumu wandishi wa habari kufumbia macho ukabila wa chadema,anaonekana ana wasi wasi sana!

Kwani huyu Katibu ni kabila gani mpe pole sana.
 
Back
Top Bottom