Katibu wa CHADEMA Mbeya anaswa kwa rushwa

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Imeandikwa tarehe 05 Desemba 2012 | Mwandishi wa HabariLeo

KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) James Mpalaza wa Wilaya ya Mbeya Vijijini amenaswa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) akipokea rushwa ya Sh 73,000.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zinasema kuwa, Mpalaza ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Ardhi katika Kata ya Nsalala alidai rushwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Ahadi Ndile kwa lengo la kumpatia hukumu iliyotolewa na Baraza hilo.

Ndile alikuwa kwenye mzozo wa mpaka na Diwani wa Kata ya Ikukwa Viti Maalumu, Monica Degua (CCM) na Baraza hilo lililopo Mbeya vijijini lilimpa ushindi Degua. Ndile alithibitisha kutokea tukio hilo akisema;

"Sikuridhishwa na hukumu ya Baraza, nikaamua kuomba nakala ya hukumu ili nisonge mbele, mwanzo waliniambia nipeleke Sh 10,000 ili niandikiwe taarifa nzuri sana.

"Nilipokwenda na fedha hizo ambazo walidai ni gharama za Baraza, walidai hazitoshi na nitapewa endapo tu nitapeleka Sh 73,000. Sikuona sababu ya kupeleka fedha hizo ndipo nilipowasiliana na Takukuru ambao leo (jana) wamefanya kazi yao," alisema.

Kwa upande wake, Kamanda wa Takukuru mkoani Mbeya, Daniel Mtuka alikiri kumshikilia Mpalaza kwa tuhuma hizo kwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Asia Haruna.

Akizungumzia tukio hilo alisema Novemba 26 mwaka huu ofisi za Takukuru mkoani hapo zilipata taarifa kutoka kwa mlalamikaji aliyefahamika kwa jina la Ahadi Ndile ambaye alikuwa na kesi ya madai namba 26, 2012 ya kugombea mpaka yeye na jirani yake Monica Degula.

Alisema kutokana na mgogoro huo wa mpaka, walipeleka kesi katika Baraza hilo ambapo baada ya uamuzi, Ndile alishindwa na Monica na hakuridhika na uamuzi huo na hivyo kuamua kuomba kupatiwa mwenendo wa shauri pamoja na hukumu.

Mtuka alisema wakati akiomba kupatiwa hukumu hiyo ndipo alipotakiwa kuhonga Sh 73,000 kwa Mpalaza ambaye ni Katibu wa Baraza hilo ikiwa ni pamoja na Sh 10,000 kwa ajili ya gharama ya kesi.

Hata hivyo Mtuka alisema migogoro ya ardhi imekuwa kero katika eneo hilo na kwamba Takukuru ina majalada mengi yatokanayo na malalamiko kutoka kwa wananchi wakitakiwa kutoa rushwa na kudhulumiwa haki zao.

Alisema bado wanahojiana na Ndile pamoja na Mwenyekiti lakini aliyepokea fedha hizo ni Mpalaza.
 
hehehe hii movie hii ya kudondoka na kusambaratika cdm itakwisha mapaema kuliko nivodhani , pass d` popcorn please :popcorn:...
 
hicho chanzo cha habari kinaifanya habari yote iwe takataka...mnajitahidi sana lakini tutawang'oa tu madarakani.
 
hehehe hii movie hii ya kudondoka na kusambaratika cdm itakwisha mapaema kuliko nivodhani , pass d` popcorn please :popcorn:...


Hivi Takukuru walikamat ngapi wakati wa uchaguzi wa ssm.kuna watu wanasangilia kama mazuzu,rushwa ya uswizi kinachoshindikana ni nini kukamata au mkulu yumo
 
78,000/= mmezishikia bango kichizi, (lakini kama ni kweli )na kwa mambo ya EPA< RICHMOND, TUSKER au NDOVU... na uchafu mwingine mwingi tu mngekuwa mnajituma hivi. Maisha bora kwa kila mtanzania yangewezekana, lakini mnashindwa kutoa boiliti kwenye macho yenu kwa kuona kibanzi ndani ya macho ya wengi, nchi hii ina laana kubwa tu, sema hatujajitambua
 
Mwenyekiti wa Baraza Asia Haruna mbona yeye chama chake hakitajwi?!

TAKUKURU well done, RUSHWA ni kansa ktk nchi hii, lakini msiishie kwenye hivyo vi-rushwa vya 73,000/- tunataka pia rushwa kubwa kama zile za USWISS nazo mzishughulikie bila kujali kama nchi itayumba.

BTW, natafuta ile habari ya Mwakyembe na RUSHWA ya TPA na TRA jana siione!
 
Kumbe gazeti lenyewe Habari Leo hapo hakuna kitu ni uhuni tuu wa gazeti,tuleteeni fedha zetu mlizokwiba na kuzipeleka Uswisi,mwambieni Kina..na arudishe wanyama wetu ambao hizo fedha ndizo wanazotumia kuhonga wapinzani.
 
Njaa mbaya katibu wa Chadema Mbeya 73,000 imemtoa imani.
 
Vigogo nchi hii HAWALI RUSHWA KABISA maana kila siku wanaokamatwa na TAKUKURU ni katibu kata,nesi Mwananyamala,mtoza ushuru stand ya Ubungo na wengineo wenzangu na mm!

Kabilioni kake na ushee Andrew Chenge huko visiwani kametulia tulii;wala hakaguswi!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom