Katibu wa CHADEMA akataa matokeo ya JK hadharani

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,084
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kutoka kwa katibu wa mkoa wa KINONDONI, KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM, HENRY J KILEWO

Kwa niaba ya chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA, tunapenda kuwashukuru wapiga kura waliyo fanikisha ushindi wa majimbo mawili kati ya matatu ndani ya mkoa wa Kinondoni.

Pili tunapenda kuwapongeza wabunge wetu wa mkoa mh John Mnyika, Halima Mdee, Susan Lyimo kwa kitendo chao cha kuunga chama mkono kutotambua matokeo yaliyo muweka rais Kikwete madarakani.

Kutokana na hilo chama mkoa tunawapongeza wabunge wetu wa chama kwa kudai KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCHANGUZI, kwa kutumia njia sahihi na ujumbe kuwafikia walengwa kwa wakati muafaka, tunawaunga mkono wabunge wote waliyo fanya kitendo hicho cha kihistoria na tupo nyuma yao mpaka kitakapoeleweka.

Tatu tunawomba watanzania wenzetu kuungana na chama katika harakati hizi za ukombozi wa wanyonge, tuwasihi kuachana na uzushi wa wapuuzi wachache wanaozusha propaganda zisizo kuwa na tija katika mabadiliko tunayo yataka watanzania ya katiba mpya.

 
Wapambanaji wote tunawaunga mkono mashujaa wetu waliotoka na maboa kwa sababu moja au nyingine walishindwa kuhudhuria kiako hicho. Chadema ni moja na haigawanyiki
 
hii imekaa njema sana........... hata mimi na familia yangu kutoka huku kijiji cha iponya makalai simtambui Raisi aliyeko madarakani
 
Tupo pamoja mpaka kieleweke. Inashangaza JK anatangaza vipaumbele vyake vyote lakini hakuna kipengele kilichogusia katiba, pamoja nakufahamu tatizo lake kwa miaka mingi.
 
mimi pamoja na wananchi wenzangu kijiweni tunawaunga mkono wabunge wote walioamua ku-walkout,
hii ni kuonesha ujasiri ambao hautaonekana tena hapa Tanzania.
Kwa Chama ni dalili za ukomavu wa kisiasa.
kuna watako pinga na kuna watakaounga mkono-na ndio sisi.
mapambano yaendelee.
tuko nyuma nyao,cha msingi watangaze maandano nchi nzima ili tuanze ushawishi kwa nguvu zote.
 
Hilo liko wazi wasiounga mkono hatua ya wabunge wa chadema ni mkumbwa ally wa daily news, uhuru, mzalendo, na familia za mafisadi wengine wote wera weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeela mwendo mdundo chadema kiongozi wa anga mbowe mpaka kieleweke
 
Back
Top Bottom