Henry Kilewo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2010
- 899
- 1,084
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwa niaba ya chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA, tunapenda kuwashukuru wapiga kura waliyo fanikisha ushindi wa majimbo mawili kati ya matatu ndani ya mkoa wa Kinondoni.
Pili tunapenda kuwapongeza wabunge wetu wa mkoa mh John Mnyika, Halima Mdee, Susan Lyimo kwa kitendo chao cha kuunga chama mkono kutotambua matokeo yaliyo muweka rais Kikwete madarakani.
Kutokana na hilo chama mkoa tunawapongeza wabunge wetu wa chama kwa kudai KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCHANGUZI, kwa kutumia njia sahihi na ujumbe kuwafikia walengwa kwa wakati muafaka, tunawaunga mkono wabunge wote waliyo fanya kitendo hicho cha kihistoria na tupo nyuma yao mpaka kitakapoeleweka.
Tatu tunawomba watanzania wenzetu kuungana na chama katika harakati hizi za ukombozi wa wanyonge, tuwasihi kuachana na uzushi wa wapuuzi wachache wanaozusha propaganda zisizo kuwa na tija katika mabadiliko tunayo yataka watanzania ya katiba mpya.