Katibu wa ccm wilaya ya namtumbo akataliwa na afungiwa na viongozi wenzake ofisini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu wa ccm wilaya ya namtumbo akataliwa na afungiwa na viongozi wenzake ofisini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Stephano Mango, Mar 24, 2012.

 1. S

  Stephano Mango Verified User

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na Stephano Mango, Namtumbo
  WAJUMBE wa kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi(CCM) wilayani Namtumbo mkoa wa Ruvuma wamemkataa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Getruda Lupola na kumfungia mlango kwa makufuri zaidi ya mawili ofisi yake kwa madai kuwa hajawahi kuitisha vikao vya kamati hiyo kwa kipindi cha miezi nane.

  Akiongea na waandishi wa habari jana Katibu mwenezi wa chama wa wilaya hiyo Reagan Luambano alisema kuwa licha ya kutoitisha kamati ya siasa kwa kipindi hicho pia kwa kipindi cha miaka mitano ameshindwa kuitisha vikao vya halmashauri kuu ya CCM ya wilaya.

  Alisema kuwa kila mara kamati ya siasa ilikuwa ikimtaka aitishe vikao lakini katibu huyo alikuwa akikataa jambo ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya chama hicho.

  Luambano alidai kuwa januari 29 mwaka huu kamati hiyo ilikutana na Katibu huyo wa chama wa wilaya ambapo walimwuliza kwa nini haitishi vikao halali vya chama lakini aliwajibu kuwa angeitisha februari 20 mwaka huu jambo ambalo halikufanyika.

  "Ilipofikia tarehe hiyo alifunga simu zote za mikononi na tulipomfuata alitueleza kuwa hawezi kuitisha vikao hivyo kwani aliagizwa na CCM makao makuu kupitia kwa Katibu wake wa chama wa mkoa asiitishe vikao hadi kipindi cha uchaguzi mwaka 2015"alisema Luambano.

  Alisema kuwa baada wa wajumbe wa kamati ya siasa kuona mwenendo wa chama sio mzuri machi 16 mwaka huu majira ya mchana walikutana chini ya Mwenyekiti wao wa CCM wa wilaya Edmund Ngonyani kujadili kwa kina mstakabali mzima wa suala hilo na baadaye walifikia uamuzi wa kumkataa Katibu huyo kutofanya shughuli zote za CCM katika wilaya.

  Alisema kuwa Lupola kukataliwa kufanya kazi za chama ni baada ya kamati ya siasa ya wilaya hiyo kugundua kuwa Katibu huyo amekiuka katiba ya chama na kwamba amevunja maadili ya uongozi ndani ya chama hicho.

  Alifafanua kuwa kamati ya siasa inapaswa kukutana kila mwezi mara moja lakini imekuwa tofauti jambo ambalo ni hatari kwa uhai wa chama.

  Alibainisha zaidi kuwa mapato na matumizi ya chama hicho yamekuwa hayasomwi na kwamba katibu huyo amekuwa akikusanya fedha toka kwa wafadhili mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya bila kamati ya siasa kujua.

  Katibu huyo mwenezi alisema kuwa kamati ya siasa inamtuhumu katibu huyo amekuwa akifanya kazi kwa ubabe na dharua kwa viongozi wenzake pamoja na wanachama wakiwemo wazee waasisi wa chama hicho wa wilaya hiyo ambao anadai wamepitwa na wakati.

  Hata hivyo Katibu wa CCM wa wilaya ya Namtumbo alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na tuhuma zinazomkabili alisema kuwa yeye hafahamu lolote na kwamba hana tatizo lolote na baadaye alikataa kuongea zaidi.

  Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma Emmanuel Mteming'ombe zimedai kuwa kamati ya siasa ya mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na mwenyekiti wake wa CCM mkoa Cornelius Msuha tayari imejipanga kwenda wilayani Namtumbo kwa ajili ya kukutana na pande zote mbili zinazovutana ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo.

  MWISHO.   
 2. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ngedere wanakula mahindi
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Chama lenyewe limeshakufa,hakuna pesa ya posho kikao ataitishaje?
   
 4. y

  yplus Senior Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamieni ChaDeMa,Chama cha Wananchi.Chama Chetu,kila MTz anahati miliki nacho.Wabunge wetu sio Miungu watu,wanatusiliza...
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe Malima keshawasili kwenye tukio jimboni kwake kwa kujionea songombingo hilo jipya au bado anashughulikia kesi Morogoro?
   
 6. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hamieni CHADEMA
   
Loading...