Uchaguzi 2020 Katibu wa CCM Wilaya Kyela anadaiwa kumwaga dawa ukumbini muda huu

Kabinti ka ludilo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
409
461
Wakuu, habari nyeti kutoka kwenye ukumbi mkubwa zaidi jijini kyela zinadai Lukas Mwanyanda katibu wa CCM wilaya, ameonekana akimwaga madawa ukumbi utakaotumika kwa uchaguzi kesho.

Vyanzo viwili nyeti vinakiri kushuhudia tukio hilo ambalo limefanyika wazi dakika chache zilizopita.

"Tulimuona alianzia kumwaga eneo la viti vya wagombea , meza kuu na baadae kwa wajumbe, sisi watatu tumemuona" alieleza mnyetishaji huyo ambaye anajilaumu kupoteza nafasi ya kumpa kichapo katibu huyo.

Chanzo hiki kimejaribu kumsaka Dr Kimati katibu mkongwe kutaka kujua mwenendo wa mmwagaji dawa huyu ambaye Ni mtumishi wake lakini hakupatikana. Lukas Mwanyanda kama anavyojiita anafahamika kutembea na kirungu chenye mashanga mashanga na kuvaa mapete ya rangi rangi kama alama yake ya kisiasa.

Nimefika ukumbini hapo muda huu na kukuta ukumbi mzima umezungukwa na mashushu wa Kila mgombea na pikipiki.

Katibu huyu anadaiwa kuwa mtiifu kwa mbunge anae maliza muda wake Daktari msomi Harrison mwakyembe.
KESHO

Kesho Ni mtifuano mkali Sana Kati ya Mafahari watatu, Mbunge Dr mwakyembe, Mwenyekiti wa Chama Ndugu Kinanas na Mwanasiasa Machachari mdomoni Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri Dr Hunter Mwakifuna.

N.B

Wewe kigogo unae karibia kuleta dawa nyingine tunazo habari zako, Tumesikia mmeapa wajumbe wajutie kuingia ukumbini humu,

Lakini je vitendo vya ushirikina vitawapa mafanikio??

Tukutane Kesho...
 
Kawaida yao, watoto wameanza kubakwa na matukio ya ajabu ajabu. Ninaamuru nguvu yoyote anayoipandikiza isifanye kazi. Na kila ovu analowakusudia watu wasio na hatiia limrudie yeye katika Jina la Yesu Kristo.

Kusema ukwlei kabisa mtu pekee mwenye kustahili na anayewapa pumziko Watanzania ni Mheshimiwa rais tu. Wengine hawa wote wanatembelea jasho lake na ki ukwlei hawafai kitu. Tuombe Mungu atupe watu sahihi watakaofanya kazi na Rais wetu na siyo hawa mehepe.
 
Sagoma hiki in kipindi chao cha mavuno. Uchaguzi ukiisha wanaoshinda wanaenda sasa kutoa shukrani makanisani.
 
Kawaida yao, watoto wameanza kubakwa na matukio ya ajabu ajabu. Ninaamuru nguvu yoyote anayoipandikiza isifanye kazi. Na kila ovu analowakusudia watu wasio na hatiia limrudie yeye katika Jina la Yesu Kristo.

Kusema ukwlei kabisa mtu pekee mwenye kustahili na anayewapa pumziko Watanzania ni Mheshimiwa rais tu. Wengine hawa wote wanatembelea jasho lake na ki ukwlei hawafai kitu. Tuombe Mungu atupe watu sahihi watakaofanya kazi na Rais wetu na siyo hawa mehepe.

Yeye mwenyewe huyo rais wako ni kidogo kwenye hayo mambo? Yeye pia bila hayo madaraka atajikuta kwenye wakati mgumu sana kwenye ushindani wa kweli.
 
Lakini si alituambia yeye ni msomi anayejielewa na ana madegree kibao

Madegree wapi boss, hayo madegree huwa yanasingiziwa tu. Watu wana nguvu zao za asili, na hizo ndio degree zao za kweli.
 
Back
Top Bottom