Katibu wa CCM Mkoa wa Rukwa au Mkewe

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia Katibu Mwenezi wa CCM wa Mkoa, Patrick Maufi (48), kwa tuhuma za kumwua mkewe, Tuli Mwakibinga (38) kwa kipigo kutokana na kilichoelezwa
kuwa ni wivu wa mapenzi.

Taarifa za Polisi Mkoa wa Rukwa, zilisema jana kuwa Tuli ambaye ni Mhudumu wa Afya
katika hospitali ya mkoa mjini hapa alifariki dunia jana asubuhi katika chumba cha
wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), hospitalini hapo.

Habari zilidai kuwa Tuli alifikishwa hospitalini hapo kutoka Hospitali Teule ya Manispaa ya Dk. Atman, kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kupigwa na kuumizwa vibaya sehemu mbalimbali hata kichwani.

Inadaiwa kuwa kabla ya kupigwa, juzi saa nne usiku, Maufi alipata taarifa kwamba mkewe yuko baa mjini hapa na alimfuata na kumpeleka nyumbani eneo la Kristu Mfalme.

Kwa mujibu wa madai hayo, wakiwa nyumbani, walianza mzozo na alimtuhumu kuwa na uhusiano na mwanamume mwingine, wakapigana.

Majirani walioshuhudia ambao hawakuwa tayari kutajwa gazetini, walieleza kuwa walimchukua mwanamke huyo na kumkimbiza Hospitali ya Dk. Atman ili apate matibabu, lakini hali ilikuwa mbaya zaidi.

Ilipofika saa 2.30 jana asubuhi Tuli alipelekwa hospitali ya rufaa mjini hapa, akiwa amepoteza fahamu na kulazwa ICU lakini alifariki dunia muda mfupi baadaye.

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk. Sadun Kabuma, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa baada ya uchunguzi wa kitabibu, ilibainika kuwa alivuja damu nyingi kwenye ubongo na shingo ilivunjika.

“Inawezekana kuwa muuaji alikuwa akibamiza kichwa cha marehemu ukutani kwa nguvu
hali iliyosababisha kuvuja kwa damu nyingi kwenye ubongo.

“Hata hivi ninavyozungumza nawe, baada ya saa kadhaa kupita, mwili bado unavuja damu puani,” alisema Dk. Kabuma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage, alithibitisha kukamatwa kwa Maufi na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

My take: huyu angelikuwa na katibu wa chadema lazima angeshamalizwa na polisi wa ccm. kwakuwa ni wa magamba basi mtasikia mara aliua bila kukusudia, au marehemu alianguka akafa, hata postmoterm itachakachuliwa.
 
Huyu katibu namfahamu vzr ni binamu yangu kabisa.Amewahi kuwa mkufunzi Ifunda_Iringa, mkewe wa ndoa amefariki mwaka huu kama miez 4/5 ilopita kwa kile kilichosemekana ni bp baada ya kumgundua mumewe ana hawala nje ambaye ndo huyo marhemu wa sasa.
 
Huyu katibu namfahamu vzr ni binamu yangu kabisa.Amewahi kuwa mkufunzi Ifunda_Iringa, mkewe wa ndoa amefariki mwaka huu kama miez 4/5 ilopita kwa kile kilichosemekana ni bp baada ya kumgundua mumewe ana hawala nje ambaye ndo huyo marhemu wa sasa.

Mke kampa lana tayari, nimewai kupata stori za lana ya mke kama hii mara mbili hii ya tatu sasa, nadhani kwa wale walioowa wanaweza kupata funzo hapa. Maana yeye aliuwa mke kwa umalaya wake na sasa huyo malaya wake naye kafungua kazi kama kawa kamuuwa kama alivyosema mtoa habari wanaweza kumtoa maana hao nilikuwa nafahamu kesi zao walitoka ila jamaa kawa kama kichaa fulani baa masaa 24/7 na kula haipandi
 
JAMANI MWAKA HUU MUNGU AMEAMUA KUWAUMBUA WANA CCM KILA UCHAO!!!

Huyu Katibu wa CCM kwanza alianza kwa kumgasi mama watoto wake hadi akafa kwa taarifa za Ma-EVENTS zisizoisha mitaani.

Haya basi badala hata ya kutulia na ki-awara chake alichokivuta ndani hata kabla ya ARUBAINNE za marehemu hazijatimia; leo hii afikie mahala pa kumchinja kama kuku hicho KIDUMU chake hivi hivi???

Kumbe hivi sakata zoooote kwa wengi wao viongozi wetu hawa wa CCM kuendekeza UFISADI kila kona ya nchi mambo tu ya kuendekeza NGONO UZEMBE?????????
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom