Katibu wa CCM agoma kuomba radhi maaskofu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu wa CCM agoma kuomba radhi maaskofu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 12, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KATIBU wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, amesema anaheshimu maoni ya aliyekuwa Makamu Mwenyeki wa CCM, John Malecela, lakini anaamini alichokisema kuhusu maaskofu kuvua majoho kama wanataka kuingilia siasa ni sahihi.

  Akizungumza jijini hapa jana, Chatanda alisema kauli aliyotoa kuhusu maaskofu kuwa wavue majoho na kuingia siasa, kutokana na kutoa kauli ya kutomtambua Meya wa Arusha, Gaudence Lyimo, inabaki imesimama haina makosa.

  Chatanda alisema kabla ya maaskofu kutoa maoni yao, walipaswa kuwaita viongozi wa vyama vya siasa na kujua ukweli badala ya kutoa maamuzi yao.

  "Namheshimu sana mzee Malecela, lakini yale ni maoni yake... mimi nilichokizungumza kinabki kimesimama," alisema Chatanda.
  Hata hivyo, Chatanda alilaumu vyombo vya habari kwa kulikuza suala la kuwataka maaskofu kuvua majoho, hali ya kuwa alizungumza mengi kuhusiana na mgogoro wa Arusha.

  “Niliwaita kutoa tamko la Kamati ya Siasa ya Mkoa, tulipongeza polisi kwa kudhibiti maandamano na pia kuelezea hasara ambayo tumeipata CCM na kutoa pole kwa wafiwa," alisema Chatanda.

  Wakati huohuo, Waandishi wa habari mkoani Arusha, wamelalamikia lugha za kejeli na dharau kwa baadhi ya wanahabari mkoani hapa, ambazo zimekuwa zikitolewa na Chatanda.

  Chatanda anadaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo ambazo zilisababisha mauaji ya watu watatu na kujeruhi zaidi ya 29, baada ya kuruhusiwa kupiga kura ya kumchagua meya wa Arusha, ilhali amepata ubunge wa viti maalum kupitia Mkoa wa Tanga.

  Kutokana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, kumruhusu kupiga kura, madiwani wa Chadema walisusa kikao na kuondoka, huku uchaguzi huo ukiendelea.
   
 2. s

  shemu Member

  #2
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 15
  'Asiye funzwa na Mamaye hufunzwa na ulimwengu' Huu siyo utamaduni wa watanzania, tena mwanamke!!!!! Kama ameoelewa hongera lakini kama bado mmmmm!!!!!!!!!
   
Loading...