Katibu wa Bunge: Hali ya afya ya Spika Ndugai inaendelea vizuri, kurejea nchini wakati wowote

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
54a6d715d9dc3cec52bcc7108fa5508e.jpg

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema hali ya afya ya Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyepo nchini India inaendelea vizuri.

Kagaigai amesema leo Februari 14,2018 kuwa Spika Ndugai yupo India kwa ajili ya kuangalia afya yake (check-up) na anatarajiwa kurejea nchini wakati wowote.

Katibu huyo wa Bunge akizungumza na MCL Digital iliyotaka kujua maendeleo ya afya ya Ndugai ambaye pia ni mbunge wa Kongwa amesema, “Tulikwisha kusema kwamba Spika yuko India kwa ajili ya ‘check-up’ na hali yake inaendelea vizuri.”

Alipoulizwa kuwa Spika atakuwa ughaibuni hadi lini, Kagaigai amesema: “Hilo ni kati ya daktari wake na yeye lakini ninachoweza kusema wakati wowote anaweza kurudi nchini.”

Chanzo: Mwananchi

Kulikuwa na taarifa kwamba Spika Ndugai ni mgonjwa na amepelekwa India kwa matibabu zaidi. Soma => Spika wa Bunge la JMT, Job Ndugai ni mgonjwa anatibiwa India.! Tumuombee
 
Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema hali ya afya ya Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyepo nchini India inaendelea vizuri.

Kagaigai amesema leo Februari 14,2018 kuwa Spika Ndugai yupo India kwa ajili ya kuangalia afya yake (check-up) na anatarajiwa kurejea nchini wakati wowote.

Katibu huyo wa Bunge akizungumza na MCL Digital iliyotaka kujua maendeleo ya afya ya Ndugai ambaye pia ni mbunge wa Kongwa amesema, “Tulikwisha kusema kwamba Spika yuko India kwa ajili ya ‘check-up’ na hali yake inaendelea vizuri.”

Alipoulizwa kuwa Spika atakuwa ughaibuni hadi lini, Kagaigai amesema: “Hilo ni kati ya daktari wake na yeye lakini ninachoweza kusema wakati wowote anaweza kurudi nchini.”

mwananchi
 
Apambane na hali take. Jeuri yote ya mwanadamu iko kwenye ugonjwa, ukifika hapo huwezi tens kuendelea maana kifo kinakufuata.

All in all get well soon Ndugai, taifa linakutegemea sana bado hujakamilisha majukumu muhimu bungeni.
 
Mara ya ngapi hii mpendwa wetu amepelekwa India kwa masuala ya afya ? Amuombe msamaha yule aliyemcharaza bakora mambo yaishe. Aliyecharazwa bakora hakushtaki mahakamani alishtaki anakojua yeye.
Aaah wapi wala sio kwa sababu hiyo...huyu spika ana maradhi mengine ya kibinadamu
 
spika anatibiwa kwa pesa zetu na ni miongoni mwa viongozi wa mihimili mikuu ya nchi.Kuna ubaya gani bunge likatoa taarifa rasmi kwamba anaumwa na anatibiwa India?wamebaki tu kusema amekwenda kwa ajili ya check up na anaendelea vizuri lakini hawasemi kwamba anaumwa.Ugonjwa unaweza kuwa siri yake na daktari lkn hakuna ubaya kusema anaumwa na pengine kalazwa huko maana check up gani ya zaidi ya mwezi?
 
Back
Top Bottom