Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,219
- 40,454
Tusiwe wajinga wa kusubiria wajinga watupatie taarifa tunapokuwa na uhakika kuna tatizo.Hivi hili suala la CORONA nalo ni la kisiasa ?!!
Lini tutajifunza kuheshimu taarifa za ofisi za wengine ?!!!
Lini ndg.Mkina amekuwa msemaji wa HOSPITALI?!!! Tena kuzitoa taarifa nzito zenye kuzua taharuki?!!!
Yaani mimi nijikurupukie tu niongelee suala la ndani la kitengo cha wagonjwa mahututi(ICU) pale MUHIMBILI kuhusu "mitungi yao ya gesi na ufanyaji wake kazi" halafu nisionekane kuzua "sintofahamu"?!!!
Magufuli muda mwingi alikuwa akiwadanganya na kuwapotosha watu wengi kwa habari za uwongo, ikiwa ni pamoja na kuwadanganya watu kuwa corona haipo, imetoweka baada ya maombi ya siku 3. Na wajinga wengi waliamini, na madhara yake ikawa ni kwa baadhi ya wenzetu kupoteza wapendwa wao.
Tunataka Taifa la watu wanaoangalia, wanaochambua, wanaodadisi, na wanaoweza kupinga kwa kauli thabiti hata kama huyo aliyesema uwongo ni Rais.
Ifahamike kuwa kwa taarifa ya CAG, zaidi ya 60% ya watumishi wa Serikali, hawanauwezo na weledi unaotakiwa kwa kazi wanazofanya, na wengi ni wenye akili ndogo na wanafiki. Ukiwafuata viongozi kama hao, utaangamia.