Katibu wa Bakwata Arusha afungwa kwa jela siku tatu tu

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Happy Lazaro, Arusha

KATIBU wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) aliyetauliwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa bin Shaaban Simba, Abdulkareem Jonjo, amehukumiwa kifungo cha siku tatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kukaidi amri halali ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha.

Akimsomea shtaka hilo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Devota Msoffe, alisema mtuhumiwa huyo alifanya kosa hilo Aprili mwaka huu, alifanya uchanguzi wa viongozi wa Baraza Wilaya ya Karatu na Arusha uliokuwa umezuiwa na mahakama hiyo.
Alisema mtuhumiwa huyo aliendesha uchanguzi wa viongozi wa Bakwata uliokuwa umezuiwa kutokana na upande mwingine wa viongozi wa baraza ulikuwa tayari umefanya uchaguzi.

Msofe alisema kutokana na migongano ya makundi mawili ya Bakwata; moja la waumini wa dini mkoani Arusha na lingine linalodaiwa kutambuliwa na Mufti Simba, mahakama ilimtaka Jonjo kutoendesha uchanguzi wa aina yoyote, amri ambayo alikaidi kutekeleza.

Kutokana na kuendesha uchaguzi huo unaodaiwa batili, waumini wa dini hiyo walikwenda mahakamani kupinga na kuomba mahakama kutoutambua kwa sababu, tayari waumini walishafanya uchaguzi wao ngazi zote.

Wakili wa walalamikaji, John Materu, aliomba mahakama kutotambua uchaguzi huo na viongozi hao kwa sababu, chaguzi hizo za viongozi zilifanyika kwa mujibu wa katiba ya Bakwata.

Mtuhumiwa huyo aliomba muda zaidi ili awalisiliane na Mufti Simba, kupata wakili wa kumtetea, baada ya wakili wa awali kujitoa, ombi lililopingwa na Wakili Materu kwa madai kuwa, tayari utetezi umefanyika na inasubiriwa hukumu.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Msoffe alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani, hivyo mahakama inatoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine wanaokaidi amri za mahakama.

Jonjo bado anakabiliwa na kesi nyingine ya kudaiwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Sekondari ya Bondeni, ilinayomilikiwa na Bakwata Mkoa wa Arusha kwa kuteua wajumbe kinyume na kanuni na taratibu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
 
Back
Top Bottom