Ni wahalifu ndio wamefanya hayo mauaji.Tunafuatilia taarifa mbaya kuhusu K/Mwenezi wa @ChademaTz, Jimbo la Malinyi, Morogoro, Ndg Lucas Lihambalimu aliyevamiwa nyumbani kwake, kupigwa risasi na kufariki hapohapo majira ya saa nane usiku. Eneo hilo la Bonde la Kilombero pia aliuawa Diwani Lwena kwa kukatwa mapanga.
===
Katibu Mwenezi wa Chadema jimbo la Malinyi Bw.Lucas Lihambalimu amevamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo, ambapo amepigwa risasi kichwani na kufariki papo hapo. Mwenyekiti wa BAWACHA wilayani humo Imelda Malley amethibitisha kutokea kwa kifo hicho. Polisi wamesema wanafanya uchunguzi kubaini wahusika waliotekeleza unyama huo.
Hii ni mara ya pili kwa Bw.Lihambalimu kuvamiwa na kushambuliwa. Mara ya kwanza ni mwaka 2013 wakati wa uchaguzi mdogo Kata ya Minepa, ambapo vijana wa CCM (Greenguard) walivamia ofisi ya Chadema kata ya Minepa na kumjeruhi kwa mapanga Lihalimbu na aliyekua M/Kiti wa CHADEMA Jimbo la Ulanga Magharibi Mohamed Kibamu. Vijana hao wa CCM walikamatwa na kuwekwa mahabusu lakini baadae waliachiwa.!