Katibu Mwenezi Chadema jimbo la Malinyi mkoani Morogoro Bw.Lucas Lihambalimu, kavamiwa na kupigwa risasi usiku

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
20,104
2,000
Tunafuatilia taarifa mbaya kuhusu K/Mwenezi wa @ChademaTz, Jimbo la Malinyi, Morogoro, Ndg Lucas Lihambalimu aliyevamiwa nyumbani kwake, kupigwa risasi na kufariki hapohapo majira ya saa nane usiku. Eneo hilo la Bonde la Kilombero pia aliuawa Diwani Lwena kwa kukatwa mapanga.

===

Katibu Mwenezi wa Chadema jimbo la Malinyi Bw.Lucas Lihambalimu amevamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo, ambapo amepigwa risasi kichwani na kufariki papo hapo. Mwenyekiti wa BAWACHA wilayani humo Imelda Malley amethibitisha kutokea kwa kifo hicho. Polisi wamesema wanafanya uchunguzi kubaini wahusika waliotekeleza unyama huo.

Hii ni mara ya pili kwa Bw.Lihambalimu kuvamiwa na kushambuliwa. Mara ya kwanza ni mwaka 2013 wakati wa uchaguzi mdogo Kata ya Minepa, ambapo vijana wa CCM (Greenguard) walivamia ofisi ya Chadema kata ya Minepa na kumjeruhi kwa mapanga Lihalimbu na aliyekua M/Kiti wa CHADEMA Jimbo la Ulanga Magharibi Mohamed Kibamu. Vijana hao wa CCM walikamatwa na kuwekwa mahabusu lakini baadae waliachiwa.!

=========
UPDATES
=========

Watatu mbaroni mauaji kiongozi wa Chadema

Mwananchi

Morogoro. Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya katibu mwenezi wa Chadema Wilaya ya Malinyi, Lucas Lihambalimu (42).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Juni 14, 2019 Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Wilbroad Mutafugwa amesema tukio hilo la mauaji limetokea Juni 13, 2019 saa 8 usiku katika kijiji cha Munga tarafa ya Mtimbira wilayani Malinyi.

Amesema uchunguzi uliofanywa imebainika chanzo cha mauaji ni mgogoro wa mashamba.

Mutafungwa amesema kada huyo alikuwa na wake wawili Anastazia Sandi (42) na Zaituni Matandiko (42).

Amesema siku ya tukio katibu huyo alikuwa amelala na mkewe mdogo, alisikia vishindo vya watu wakitembea nje ya nyumba yao.

“Alimwamsha mkewe na kumwambia kuwa kuna watu wapo nje ya nyumba, alichungulia kupitia uwazi uliopo kati ya paa na ukuta, na alifanikiwa kuwaona watu watatu na kumtambua mmoja."

“Aliwaona hao watu wakielekea upande mwingine wa nyumba yao na alienda kuchungulia tena ndipo aliposikia mlipuko wa bunduki na kumueleza mkewe kuwa wamempiga na kurudi kitandani akiwa anavuja damu kichwani,” amesema.

Amesema shambulio hilo wananchi walienda kutoa taarifa kituo cha polisi, askari walifika eneo la tukio na kukuta kipande kidogo cha chuma chenye umbo la duara kinachotumika katika bunduki zilizotengenezwa kienyeji.

Amesema walianza msako kutokana na tukio hilo polisi kwa kushirikiana na wananchi na kuwakamata watu watatu.

Mutafungwa amesema mwili wa katibu huyo ulifanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika jana Alhamisi Juni 13, 2019.
 

Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
751
1,000
Tunafuatilia taarifa mbaya kuhusu K/Mwenezi wa @ChademaTz, Jimbo la Malinyi, Morogoro, Ndg Lucas Lihambalimu aliyevamiwa nyumbani kwake, kupigwa risasi na kufariki hapohapo majira ya saa nane usiku. Eneo hilo la Bonde la Kilombero pia aliuawa Diwani Lwena kwa kukatwa mapanga.
Innaalillahi wainnah ilayhi rajiun
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
20,104
2,000
hili ni tatizo ambalo chadema inabidi wajitafakari kuwa na viongozi majambazi au wenye visasi na watu huwezi kuvamiwa na kuuwawa bila sababu atakuwa alikuwa jambazi au mzurumaji wenzake wamemuwahisha ku rest in pc hapo hakuna siasa msijesema ccm kama mmoja alivyo commet hapoa juu nyambafffff
Kama ni Chadema wangapi walishahukumiwa au polisi wanaiogopa Chadema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom