Katibu Mkuu Yanga ajiuzulu

Simba na Yanga ni MIJIPU ya soka letu ambayo imekosa mtumbuaji.

Wamejaribu akina Mengi ikashindikana Mo kaja leo na billioni zake waapi!

Itungwe sheria ya kuvifutilia mbali au sheria ya kuvilazimisha viwe makampuni na hisa zake zisajiliwe soko la hisa wenye mpunga wao waje wavinunue.
 
Mimi binafsi sioni tofauti ya makatibu waliopita na huyo aliyeondoka tuwe wakweli kipi kipya? hatuna chanzo chote cha mapato bado tunategemea vigiliwo vya uwanjani, bidhaa zenye nembo ya yanga zinauzwa kama njugu yanga haifaidiki chochote, ukija kwenye usajili aliyeletwa ni je anamzidi aliyevunjiwa mkataba? imefika wakati sasa yanga itafute eneo la uwanja tofauti na pale jangwani, Nimepeleka barua ya kampuni moja inataka kuidhamini yanga imewekwa kapuni, mimi naumia kwa yanga kutokuwa na uwanja sikwakuondoka kwa mtu, mfumo wenyewe mbovu.
 
Kwakhery dr Tborhora
Na moody kabwe

Mimi binafsi sioni tofauti ya makatibu waliopita na huyo aliyeondoka tuwe wakweli kipi kipya? hatuna chanzo chote cha mapato bado tunategemea vigiliwo vya uwanjani, bidhaa zenye nembo ya yanga zinauzwa kama njugu yanga haifaidiki chochote, ukija kwenye usajili aliyeletwa ni je anamzidi aliyevunjiwa mkataba? imefika wakati sasa yanga itafute eneo la uwanja tofauti na pale mimi naumia kwa yanga kutokuwa na uwanja sikwakuondoka kwa mtu, mfumo wenyewe mbovu

Katiba ya Yanga africa ibara ya 48: Mapato

Chanzo cha mapato ya Young Africans Sports Club kitakuwa hasa ni:

1. Kutokana na viingilio.
2. Kutokana na mikataba ya udhamini
3. Kutokana na ada ya uwanachama wa Yanga africa
4. Kutokana mapato yaliyotokana kwa kuuza haki ambazo yanga africa inastahiki na mauzo ya bithaa zenye chapa maalumu;
5. Kutokana na michango ya mwaka ya mwanachama.
6. Kutokana na faini iliyotozwa na vyombo vilivyoidhinishwa;
7. Kutokana na ada zinazotakiwa kulipwa na mapato mengine kwa mujibu wa malengo yanayotekelezwa na yanga africa
8. Kutokana na ruzuku za serekali, TFF na wahisani wengune;
9. Kutokana na mapato yaliyotokana na shughuli za biashara za Yanga africa
10. Kutokana na mapato yaliyotoka na shughuli za biashara za Yanga Africa
11. Kutokana na fedha zinazopatikana kutokana na hisa za klabu kwenye kampuni.
12. Kutokana na fedha zinazotokana na timu kusimamiwa na kampuni kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni na klabu;
13. Kutokana na vyanzo vingine vyovyote halali

Baada ya maelezo hayo na kuooanisha vyanzo vya mapato ninaomba ndugu zangu wanayanga muniambie ni kipi huyu dr Tiborhora kafanya kipya???

Binafsi naigeshimu elimu yake kwakua hatufanani ila elimu yake ameshindwa kuitendea haki ndani ya Yanga kwani amani ya Yanga hajaileta yeye ndiyo maana hata yeye kaja baada ya kukuta ndani ya timu kuna amani kubwa sana
Ambayo kaitengeneza mwenyekiti manji na wanachama kuonesha usikivu kwake

Hivyo bas kama Dr kaona hatendewi haki tunamtakia kila la khery kama watumishi wengine tu wanaohitaji katika katiba yetu kama inavyoeleza katika ibara ya 37 ya katiba yety ya Yanga africa ya mwaka 2008 iliyofanyiwa marekebisho

Nakutakia kila kheri Dr Tiborhora umeiyacha yanga kama ulivyoikuta

Sijaona la zaidi kungana na mashabiki wengine wanaokuona bora kwakua tumefunga simba na mtibwa nyumbani kwake

Nipende kuwaomba ndugu zangu mashabiki wa yanga Yanga ugonjwa wake sio katibu ugonjwa wa yanga ni sisi wenyewe maana tumebebwa na mhemko mkubwa sana wa ushabiki kuliko kuangalia maendeleo ya soka la kilabu yetu

Asanteni by moody kabwe
 
Soka la Association tusemezane ukweli haliwezi kuendana na kasi ya mabadiliko na utandawazi wa siku hizi.

Hilo la Association lilikuwa kipindi kile wazee wetu walipokuwa wakiwa wanapata faragha ya kubadilishana mawazo na kumwondoa mkoloni.

TFF itunge kanuni timu zote za VPL zimilikiwe kwa mtindo wa KAMPUNI hiyo itaondosha kabisa MZIZI WA FITINA.

Vilabu vitakuwa na wamiliki wakubwa haina maana wanachama wataondolewa watakuwa na hisa na na watakuwa na VETO ya kumchagua Mwenyekiti wa timu.
 
Binafsi nimefurahi, adui mwombee njaa. Tayari gogoro linafukuta nyumba ya jirani.
 
Katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha amejiuzulu wadhifa wake ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangua akalie kiti hicho.
Tiboroha ameandika barua ya kujiudhuru kwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kwa sababu alizoziita za “kujikita zaidi katika kazi yake ya uhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam’.
Habari za ndani ya Yanga zinasema kujiuzulu kwa Tiboroha si jambo la kushtukiza kwani kumekuwa na msuguano kwa muda sasa kati ya pande mbalimbali.
Inadaiwa suala la Niyonzima pamoja na usajili wa wachezaji na kutolewa mlangoni kwa baadhi ya makomandoo kulizua vita ya kimaslahi ndani ya klabu hio.
Habari zaidi zinadai, Tiboroha aliamua kung’atuka baada ya kuwepo taarifa za nafasi yake kupewa mkurugenzi wa fedha, Baraka Deusdith kuikaimu yake.
Huyu bwana yupo makini ni bora akaajiriwa Azam FC.
 
Mliokua mnabisha naimani mtakua mmeelewa sasa SAKATA LA NIYONZIMA LAMUONDOA KATIBU YANGA
 
usifikiri kama yanga itayumba ng'ooo.. vipigo vipo palepape.
Yangu macho. Kwa sisi wapenzi wa mpira wa hapa kwetu tunajua, gogoro zamu kwa zamu likitulia kwa wananchi ujue wazalendo hali ngumu. We si shabiki wa Chelse au Mwanitesa united huwez jua soka letu
 
Pluijm aupongeza uongozi wa yanga kwa hatua walizochukua.

Binkleb aupongeza uongozi wa yanga kwa hatua walizochukua.....

Bye bye hakizimana....nenda simba.....

Tiboroha is there to stay
Kauli yako unaionaje na yalitokea Yanga?

Tiboroha aliondoka, Pluijm na Niyonzima mambk safi tu wanapiga kazii
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom