Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mchembe: Tusichelewe kwenda katika Vituo vya Afya kupata matibabu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
871
1,000
Na WAMJW- ARUSHA

KATIBU MKUU Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchembe ametoa wito kwa wananchi kuwahi kwenda kupata matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya kuliko kujitibia nyumbani jambo linaloweza kuhatarisha maisha ya mtu kwa kiasi kikubwa.

Prof. Mchembe ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya, katika Hospitali ya Selian (Arusha Lutheran Medical Centre) na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru) ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi kukagua hali ya utoaji huduma za afya nchini

"Nitoe wito kwa wananchi pale inapotokea matatizo ya kuumwa ni vizuri kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuonwa kuliko kusema kwamba unajitibia nyumbani jambo ambalo ni hatari kwa afya yako, hospitali zimejengwa kwa ajili ya kutoa huduma." amesema Prof. Mchembe.

Prof. Mchembe aliendelea kutoa rai kwa wananchi kujitahidi kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kufahamu hali zao na kuweza kuanza matibabu mapema endapo itagundulika kuwa na tatizo la kiafya.

Aidha, amesisitiza kuwa, sio kila tatizo ambalo analipata mgonjwa katika mfumo wa hewa ni Corona, huku akiweka wazi kuwa wengi wana matatizo ya moyo, matatizo ya kisukari na matatizo ya figo ambayo kwa kiasi kikubwa yanapelekea shida katika upumuaji.

"Tujitahidi sana kupima Afya zetu, kwasababu kuna wagonjwa wengi walio hospitali wana matatizo ya moyo, na kisukari na matatizo ya figo, sio matatizo yote yanahusishwa na Corona, mengine yanahitaji matibabu." Amesema Prof. Mchembe.

Akijibu swali kuhusu taarifa za uzushi juu ya kujaa kwa wagonjwa katika hospitali hizo Prof. Mchembe amesema kuwa, ni vizuri kwa wanasiasa kujiridhisha kwa kutembelea katika maeneo ya kutolea huduma za afya kabla ya kutoa kauli zao ambazo hazina ukweli wowote, huku akisisitiza vitanda vipo wazi na hospitali hizo zinaendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (Serian) Dkt. Paul Kisanga amesema kuwa, shida ya wagonjwa kuchelewa kwenda kupata matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya, ni jambo linaloweza kupelekea kupoteza maisha kwa mgonjwa.

"Tatizo kubwa ambalo tunalipata katika hospitali sasahivi ni watu kuja wakiwa wamechelewa, sio tu kwa matatizo ya kifua, hata matatizo ya upasuaji, sasahivi pia tunapata shida ya watu kuwa na tabia ya kujitibu nyumbani hata wanapokuwa na matatizo mengine kama kisukari na moyo," amesema.

Aliendelea kwa kutoa rai kwa wananchi, kuwahi kwenda kupata matibabu ili wataalamu wapate nafasi ya kuwarudisha katika mzunguko wa kawaida wa afya zao na kuendelea na ujenzi wa Taifa, huku akisisitiza kuwahi kupata huduma kutasaidia kupunguza gharama kwa mtu binafsi, hospitali na Taifa kwa ujumla.

Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru), Dkt. Alex Ernest amesema kuwa, Hospitali ya Mount Meru imejipanga vizuri kutoa huduma bora kulingana na miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya.
IMG-20210212-WA0067.jpg
IMG-20210212-WA0065.jpg
IMG-20210212-WA0064.jpg
IMG-20210212-WA0063.jpg
IMG-20210212-WA0062.jpg
IMG-20210212-WA0059.jpg

IMG-20210212-WA0061.jpg
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,120
2,000
Hiyu nimemwona ni mjinga asiye na faida, pale anapokazania kuonesha hakuna tatizo la corona.

Wagonjwa wengi wanaoamini wanaugua corona wanaamua kuugulia nyumbani kutokana na maelekezo yao potofu kuwa corona inatibiwa kwa nyungu.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
81,837
2,000
Hiyu nimemwona ni mjinga asiye na faida, pale anapokazania kuonesha hakuna tatizo la corona.

Wagonjwa wengi wanaoamini wanaugua corona wanaamua kuugulia nyumbani kutokana na maelekezo yao potofu kuwa corona inatibiwa kwa nyungu.
Huyu ni miongoni mwa viongozi duni kabisa nchini Tanzania
 
Wizara ya Afya Tanzania

Verified Member
Oct 1, 2020
34
125
Badala mseme hali ilivyo mnazunguka zunguka tu unafiki huu
Lugha ya kiungwana ni mhimili katika uzalendo. Huwezi kuambiwa hii ni Corona wakati mtu ana matatizo ya figo, high pertension, athma, sickle cell, upungufu wa damu mwilini, HIV n.k ambayo pia yanaleteleza shida hiyo.

Ila vile hatufiki hospital kwa wakati hayo nayo yanakua chronic na matokeo yake hali ikishakua tete ndo tunajitokeza kuokoa maisha wakati tuko kwenye koma...ni mbaya.

Tusienezeane taharuki mpaka watu wanaacha kuhudhuria klinik zao za kila siku kwa uoga. Nawasihi tuendelee kufuata maelekezo ya wizara na wataalamu wetu wa afya
 
Wizara ya Afya Tanzania

Verified Member
Oct 1, 2020
34
125
Hiyu nimemwona ni mjinga asiye na faida, pale anapokazania kuonesha hakuna tatizo la corona.

Wagonjwa wengi wanaoamini wanaugua corona wanaamua kuugulia nyumbani kutokana na maelekezo yao potofu kuwa corona inatibiwa kwa nyungu.
Hamatan,
Hakuna aliyeelekeza watu kuugulia nyumbani. Na ingekua hivyo hata tusingesema tuonapo dalili tuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa huduma za haraka kabla ya mwili kuchoka kabisa na kushindwa kuhimili mikiki ya matatizo haya. Aidha, cha msingi ni kufuata maelekezo ya Wizara na wataalamu wa afya.
 
binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
4,374

Wakuu kumbe mpo hadi huku, basi mwambieni yule mama Gwajima aache komedi zake.
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,920
2,000
Gharama ni zilezile za awali, nazo hatuzimudu? Ukipewa gharama tofauti mtafute aseme why unapewa gharama tofauti, namba zao si wametoa public?!
Gharama ni zilezile lakini watu hawana uwezo wa pesa. Waliokuwa wanamudu zamani sasa hivi hawazimudu. Na wale waliokuwa wanakopa ili wazimudu sasa hivi hamna wa kuwakopesha. Watu wengi kupata 5000 ni mtihani.

Amandla...
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,920
2,000
Hamatan,
Hakuna aliyeelekeza watu kuugulia nyumbani. Na ingekua hivyo hata tusingesema tuonapo dalili tuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa huduma za haraka kabla ya mwili kuchoka kabisa na kushindwa kuhimili mikiki ya matatizo haya. Aidha, cha msingi ni kufuata maelekezo ya Wizara na wataalamu wa afya.
Mnachanganya watu. Mara nyungu na maparachichi ndio mpango mzima, mara dawa za Nimr halafu sasa wakimbilie hospitali!

Amandla...
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,920
2,000
Lugha ya kiungwana ni mhimili katika uzalendo. Huwezi kuambiwa hii ni Corona wakati mtu ana matatizo ya figo, high pertension, athma, sickle cell, upungufu wa damu mwilini, HIV n.k ambayo pia yanaleteleza shida hiyo. Ila vile hatufiki hospital kwa wakati hayo nayo yanakua chronic na matokeo yake hali ikishakua tete ndo tunajitokeza kuokoa maisha wakati tuko kwenye koma...ni mbaya. Tusienezeane taharuki mpaka watu wanaacha kuhudhuria klinik zao za kila siku kwa uoga. Nawasihi tuendelee kufuata maelekezo ya wizara na wataalamu wetu wa afya
Tumewasikia.

Amandla...
 
Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
8,568
2,000
Gharama ni zilezile za awali, nazo hatuzimudu? Ukipewa gharama tofauti mtafute aseme why unapewa gharama tofauti, namba zao si wametoa public?!
Wizara ya Afya katika hili la covid19, imeshindwa kuweka basics za Public Health.
Hadi Waziri anakazania nyungu badala ya elimu ya kujikinga.
Leo wananchi kwenye daladala hawavai barakoa na wanasongamana.
Tutawategemea wanasiasa katika hili?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom