Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Serikali imetoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya malezi vya watoto na (Day Care), kurekebisha kasoro ili watoto hao walelewe katika mazingira sahihi na kwa kujibu wa Sheria.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dk. John Jingu, alitoa agizo hilo jijini Arusha baada ya kutembelea baadhi ya vituo na kubaini kutozingatia masharti ya utoaji wa huduma kwa watoto kama ilivyoainishwa kwenye sheria na miongozo.
“Eneo hili (kwenye kituo kimojawapo), halikidhi vigezo na mazingira ya kuwa kituo cha malezi ya watoto mchana, kwa hiyo nawapa wiki mbili mrekebishe upungufu wote, mtafute eneo jingine, maofisa ustawi waje kufanya ukaguzi baada ya siku 14, kama hamjakidhi tutakifunga," alisema Dk. Jingu.
IPPMEDIA