Katibu Mkuu Wizara ya Afya ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mchana vya malezi ya watoto (Day Care) kurekebisha kasoro kabla havijafungiwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,384
2,000
Serikali imetoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya malezi vya watoto na (Day Care), kurekebisha kasoro ili watoto hao walelewe katika mazingira sahihi na kwa kujibu wa Sheria.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dk. John Jingu, alitoa agizo hilo jijini Arusha baada ya kutembelea baadhi ya vituo na kubaini kutozingatia masharti ya utoaji wa huduma kwa watoto kama ilivyoainishwa kwenye sheria na miongozo.

“Eneo hili (kwenye kituo kimojawapo), halikidhi vigezo na mazingira ya kuwa kituo cha malezi ya watoto mchana, kwa hiyo nawapa wiki mbili mrekebishe upungufu wote, mtafute eneo jingine, maofisa ustawi waje kufanya ukaguzi baada ya siku 14, kama hamjakidhi tutakifunga," alisema Dk. Jingu.

IPPMEDIA
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Serikali ya Tanzania huwa inanishangaza hapo tu, sasa unatoa onyo la nini kwa watu waliovunja Sheria ? Kwa nini wasifunge kwanza na kupiga faini halafu ndio waliopigwa faini wajirekebishe kama wakiweza?

Mnatoa maonyo ya nini? Watu wanakufa na kulemazwa kila siku kwa ungese wenu wa kutoa maonyo, madereva wanachinja watu barabarani mnatoa onyo tunaanza kukagua leseni, watoto wanafundishwa na walimu wasio na vigezo mnatoa onyo mnaanza kukagua vyeti feki, watu wanalishwa nyama za ng'ombe wenye ugonjwa mnatoa inyo mnaanza kukagua, kuna hospitali, maduka ya dawa feki nchi nzima mnatoa onyo kila siku onyo WTF, fanyeni kazi acheni kutuzingua kila siku mnatoa onyo onyo onyo.

Low IQ people !
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,341

Mnatoa maonyo ya nini ? Watu wanakufa na kulemazwa kila siku kwa ungese wenu wa kutoa maonyo, madereva wanachinja watu barabarani mnatoa onyo tunaanza kukagua leseni, watoto wanafundishwa na walimu wasio na vigezo mnatoa onyo mnaanza kukagua vyeti feki, watu wanalishwa nyama za ng'ombe wenye ugonjwa mnatoa inyo mnaanza kukagua, kuna hospitali, maduka ya dawa feki nchi nzima mnatoa onyo kila siku onyo WTF, fanyeni kazi acheni kutuzingua kila siku mnatoa onyo onyo onyo.

Low IQ people !
Wewe ndo mwenye zero IQ. Nitafurahi ukibadili jina hilo unaliaibisha
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
8,928
2,000
Hizo siku14 zisiishie Arusha tuu, hilo liwe zoezi endelevu kwa nchi nzima.

Halafu hata kama vituo vinakua sawa wizara ya afya irudi nyuma na kuangalia faida na hasara za hivi vituo. Watoe miongozo itakayozingatia malezi na afya za akili kwa watoto

Wazazi wa siku hizi nao kuna wakati unaweza kujiuliza kama huwa wanazaa kama fasheni au wanazaa wakijua kwamba wana wajibu wa kuwalea watoto wanaowazaa

Hivi unapomuamsha mtoto wa miaka2 alfajiri hajamaliza kulala na kumfungashia diapers na kumkabidhi mtu usiyejua adeal nae kwa masaa8 hadi 12 unajiskiaje? Hata kama unaenda kutafuta pesa hizo pesa zina thamani ya huyu mtoto kweli??

Kulea sio kumuajiri au kumlipa mtu pesa ukulele watoto wako jamani. Kama hujaweza kulea mtoto afike umri wa kwenda shule heri usubiri hadi uwe tayari
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Wewe ndo mwenye zero IQ. Nitafurahi ukibadili jina hilo unaliaibisha

Hao Serikali ndio wana low IQ, sasa mtu kaenda kusajili kituo cha kulea watoto, kapewa fomu kajaza, kapewa masharti kayasoma na kuyaelewa karuhusiwa kafungua kituo, anashindwa kufwata masharti unaanza kumpa onyo ajirekebishe?

Kwa nini Serikali isiwachukulie hatua badala ya kuwapa onyo kwani wanajua nini wafanye siyo watoto wadogo hao wenye hivyo vituo, unakwenda hospitali daktari ana fyeti feki anapewa onyo ajirekebishe ni ujinga gani huo ?
 
Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
5,261
2,000
Hili la vituo vya afya kukosa dawa muhimu wametoa siku ngapi?
Dada joy alipoingia madarakani badala ya kushughulika na vitu vinavyomhusu, yeye alikua anahabgaika na private schools.
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,341
2,000
Hao Serikali ndio wana low IQ, sasa mtu kaenda kusajili kituo cha kulea watoto, kapewa fomu kajaza, kapewa masharti kayasoma na kuyaelewa karuhusiwa kafungua kituo, anashindwa kufwata masharti unaanza kumpa onyo ajirekebishe ? Kwa nini Serikali isiwachukulie hatua badala ya kuwapa onyo kwani wanajua nini wafanye siyo watoto wadogo hao wenye hivyo vituo, unakwenda hospitali daktari ana fyeti feki anapewa onyo ajirekebishe ni ujinga gani huo ?
Ntakujibu baadaye. Hujui kwamba kuwachukulia hatua ni pamoja na kuwatahadharisha wajirekebishe? Au "kuchukua hatua" unaelewaje? Tuanzie hapo. Isijekuwa unaongea misamiati ya Alfu Lela Ulela
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Ntakujibu baadaye. Hujui kwamba kuwachukulia hatua ni pamoja na kuwatahadharisha wajirekebishe? Au "kuchukua hatua" unaelewaje? Tuanzie hapo. Isijekuwa unaongea misamiati ya Alfu Lela Ulela

Kwangu mimi hakuna haja ya kumtangazia mtu anayevunja sheria kwa makusudi kwamba siku fulani tutaanza kukuchulia hatua, wanapaswa kuvamia bila ya taarifa na kuchukuwa hatua kwani hao wamiliki wa hivyo vituo wanajua wanachopaswa kufanya lkn hawafanyi kwa makusudi hivyo mkiwatangazia watarekebisha sawa mpaka hiyo siku mtakuja kukagua mkiondoka wanarudia yale yale mpaka mje mwatangazie tena na kuwa wanajirekebisha tena mkiondoka wanaendele ni michezo, sasa Seriklai haipaswi kufanya kazi hivyo matatizo hayawezi kupungua kama tunabembelezana hivyo, wao Serikali wafanye kazi bila matangazo wavamie hivyo vituo muda wowote na kukagua atakayekutwa hatimizi vigezo achukuliwe hatua hapo ndivyo nidhamu inavyojengwa na nchi kuanza kusonga mbele, ...
 
Umewnza vizuri: "Kwangu mimi…" Serikali haiko kuadhibu, bali kuongoza na kusimamia na kufundisha. Don't generalize things.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Umewnza vizuri: "Kwangu mimi…" Serikali haiko kuadhibu, bali kuongoza na kusimamia na kufundisha. Don't generalize things.

Na ndio maana matatizo hayaishi na ni yale yale kila siku, bila ya adhabu binadamu haendi, hata Kanisa linaadhibu isitoshe ni gharama pia kwa Serikali hiyo hiyo kurudia mambo na kudili na matatizo yale yale kila siku, kama wananchi wakiweza kujisimamia inaipunguzia Serikali gharama na kuwekeza kwenye mambo mengine sasa hii ya kukagua kila siku mtakagua hiyo siku mliowatangazia, mkiondoka wanarudia tena kwa maana wanajua mtawatangazia tena lkn msisahau hawa watu wanadili na watoto ambao wanaweza kudhurika kwa kuwa kwenye mazingira ambayo hayastahili, ...
 
Aina ya adhabu unayopendekeza siyo motivation fanisi ya behavioral change. Sijajua ahule ulisomeaga wapi!? Tahadhari ni njia ya kuhimiza personal voluntary responsibility na accountability. The government doesnot exist to punish but to lead.
 
Ndiyo hivyo kama hawajui lini mnakuja kuwakagua hawawezi kuzembea watakuwa tayari muda wote lkn kama mnawatangazia hakuna watakachobadilisha ukiondoa hiyo siku mnayokuja, I mean mwizi kaiba halafu unamtangzia wiki ijayo nakuja kukagua chumba atakuwa ni mwizi mjinga kama hataondoa alichoiba kwenye hicho chumba.

Kumbuka kwamba hapa hamdili na watoto bali ni watu wazima ambao wanajua nini cha kufanya lkn wameamua kwa makusudi kutokufanya inavyopaswa sasa mnawatangazia na kuwabembeleza wa nini ?
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
12,372
2,000
Hizo siku14 zisiishie Arusha tuu, hilo liwe zoezi endelevu kwa nchi nzima.

Halafu hata kama vituo vinakua sawa wizara ya afya irudi nyuma na kuangalia faida na hasara za hivi vituo. Watoe miongozo itakayozingatia malezi na afya za akili kwa watoto

Wazazi wa siku hizi nao kuna wakati unaweza kujiuliza kama huwa wanazaa kama fasheni au wanazaa wakijua kwamba wana wajibu wa kuwalea watoto wanaowazaa

Hivi unapomuamsha mtoto wa miaka2 alfajiri hajamaliza kulala na kumfungashia diapers na kumkabidhi mtu usiyejua adeal nae kwa masaa8 hadi 12 unajiskiaje? Hata kama unaenda kutafuta pesa hizo pesa zina thamani ya huyu mtoto kweli??

Kulea sio kumuajiri au kumlipa mtu pesa ukulele watoto wako jamani. Kama hujaweza kulea mtoto afike umri wa kwenda shule heri usubiri hadi uwe tayari
Kumbe kuna siku unaandika mambo ya maana?
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,341
2,000
Ndiyo hivyo kama hawajui lini mnakuja kuwakagua hawawezi kuzembea watakuwa tayari muda wote lkn kama mnawatangazia hakuna watakachobadilisha ukiondoa hiyo siku mnayokuja, I mean mwizi kaiba halafu unamtangzia wiki ijayo nakuja kukagua chumba atakuwa ni mwizi mjinga kama hataondoa alichoiba kwenye hicho chumba.

Kumbuka kwamba hapa hamdili na watoto bali ni watu wazima ambao wanajua nini cha kufanya lkn wameamua kwa makusudi kutokufanya inavyopaswa sasa mnawatangazia na kuwabembeleza wa nini ?
Your views are too extreme. Halafu unawalinganisha na mwizi, really??? The government wants its people to self-govern themselves na wala siyo kuishi kwa hofu ya kuadhibiwa. Kurudia makosa ndiyo mbaya, otherwise "usi-jenero-rahisi" mambo.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Your views are too extreme. Halafu unawalinganisha na mwizi, really??? The government wants its people to self-govern themselves na wala siyo kuishi kwa hofu ya kuadhibiwa. Kurudia makosa ndiyo mbaya, otherwise "usi-jenero-rahisi" mambo.

Ndiyo ni sawa na wezi tena zaidi ya wezi kwa maana ni watu wazima wanadili na maisha ya watoto, na wameamua kwa makusudi kutokufwata sheria za nchi, labda nikuulize ni nani atafidia damage ambayo watoto wataipata kwa kuwa kwenye mazingira mabovu yaliowekwa na watu kwa makusudi kabisa ? Nani atalipia hiyo gharama ? Na mpaka lini hali hii itaendelea mpaka mje muone kwamba labda ninyi ni sehemu ya tatizo ? I mean ni watu wangapi wanakufa kwa uzembe kila barabarani kwa makosa ambayo yangeweza kuzuilika kama tu kungekuwa na adhabu kali kwa wanaokiuka sheria zetu na siyo kuwatangazia na kuwaambia wajitayarishe kwa kuwa siku mnakuja kuwakagua?
 
Usidhani hata wakikatwa shingo inaredeem tatizo, OK? We want to build, not to destroy. Kuna makosa genuine. Kuna kujisahau. Kuna uzembe wa wazi. But tahadhari na maonyo is at the very heart of the permanent solution. We change people's behavior effectively by helping them know where they lacck and how they should improve by giving another chance. This is common sense! Huhitaji kuwa rocket scientist ama Albert Eistein ili kujua hii fomula rahisi.
 
Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,644
2,000
Serikali ya Tanzania huwa inanishangaza hapo tu, sasa unatoa onyo la nini kwa watu waliovunja Sheria ? Kwa nini wasifunge kwanza na kupiga faini halafu ndio waliopigwa faini wajirekebishe kama wakiweza?

Mnatoa maonyo ya nini? Watu wanakufa na kulemazwa kila siku kwa ungese wenu wa kutoa maonyo, madereva wanachinja watu barabarani mnatoa onyo tunaanza kukagua leseni, watoto wanafundishwa na walimu wasio na vigezo mnatoa onyo mnaanza kukagua vyeti feki, watu wanalishwa nyama za ng'ombe wenye ugonjwa mnatoa inyo mnaanza kukagua, kuna hospitali, maduka ya dawa feki nchi nzima mnatoa onyo kila siku onyo WTF, fanyeni kazi acheni kutuzingua kila siku mnatoa onyo onyo onyo.

Low IQ people !

Katili sana wewe mwanamke.
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,341
2,000
Katili sana wewe mwanamke.
Siyo kosa lake; she is among wale elfu ishirini na ushee waliokuwa na fake academic certificate na pia mwenzie alitumbuliwa kwa upiga-dili kule bandarini. Sasa unaelewa kwa nini anataka wengine wabamizwe kama yeye.
 
ammoshi

JF-Expert Member
Jun 14, 2013
534
500
Kama mnataka standard zote siku ya kwanza....Lea mwenyewe dada wala usihangaike. Kama unashjndwa then kosoa kwa staha. Unakuta mtu analalama ila kutunza hawezi, kulipa ada pia hawezi sasa usaidiweje?. Japo siungi mkono watu kutokuweka Mazingira stahiki kwa watoto.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom