katibu mkuu WEMA zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

katibu mkuu WEMA zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngisi, Sep 2, 2009.

 1. N

  Ngisi Member

  #1
  Sep 2, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU -ZANZIBAR

  naamini wewe ni mmoja ya watendaji wazuri katika wizara ya Elimu Zanzibar ambae licha ya kuwa na uchungu na Elimu lkn ni mmoja ya unaofatilia kwa karibu mfumo wa Elimu Zanzibar na Tanzania,ni mfumo uiobadika katika vyuo vya Serekali na taasisi zinazojitegemea, ni mfumo ambao umewaaptia vijana wengi kuendelea na masomo ngazi mbali mbali
  Hivi karibuni baadhi ya wanafunzi ambapowanaosoma ualimu katika Chuo Cha kiislam kiliopo Mazizini wamesimamishwa masomo huku tayari wakiwa wamefanay mitihani yao na kufaulu (mwaka wa 1)ni kasoro ambayo wewe kama katibu mkuu kuchukua hatua za haraka ili kuwarudisha vijana a waendelee na masomo vyenginevyo kasoro hiyoinaweza kusababisha kuwakosesha masomo vijana ambao wanasifa za kusoma chuoni hapo kwa mujibu wa Mfumo wa Elmu wa Tanzania ulivyo kwa sasa. Lakini pia tayari vijana hao wamesoma hapo Mwaka Mzima na kufaului vizuri mitihni yao ya mwaka wa 1, kitendo cha kuwafukuza kutokana na kukosa C3 ni jambo ambalo limepitwa na wakati au niseme haliwatendei haki vijana hao hasa ukizingatia Vyuo vyote nchini sasa mfumo umbeabadilka.

  kwa mfano vijana wasio na sifa za kujiunga moja kwa moja Chuo Kikuu Dsm , Tunguu universities, Chukwani universities au DIT (Engineer) kwanza husoma Pree Course miezi 3 au mwaka mmoja na baadae hukubalika kujiunga na chuo hicho pindi akifaulu mitihani ya chuo hicho na sio kurudia mitihani ya taifa. Lkn pia vyuo kama chuo cha fedha ZIFA, Chuo kikuu cha ta ifa ambapo wewe pengine ni mmoja ya mwanakamati (SUZA), IFM, MZUMBE nk wanafunzi wasio na sifa za kujiunga na degree moja kwa moja huanzia Cerificate(cheti) ya chuo husika ambao wengi wa wanafunzi hao humaliza Form 4 na husoma hapo kwa muda wa mwaka 1 na baadae hujiunga na Degree au AD diploma. ni mfumo hata Serekali zetu SMZ na SMT wameuridhia. lkn pia NECTA na NACTE wameukubali na ni mfumo uanwapa vijana wengi wa tz kuingia vyuoni na humaliza wakiwa na elimu ya juu.kama utaangalia zaidi, utagundua zaid 13% ya wahitimu wa Elimu ya juu Tanzania ni walimaliza F4 without c3, wakajiunga na kozi ya chuo husika na baadae kuhitimu kwa mafano SUZA na ZIFA ni mfumo ambao vijana wengi wanautumia kufanikisha malengo yao ya kupata Elimu zaid.
  Kutumiliwa kwa wanafunzi katika chuo Muslim kwa kisingizio cha c3 hakiwatendei haki vijana hao wenye hamu ya kujiendeleza na ambao kwakweli katika mfumo huu uliopo Tanzania. jee kwanini vijana hao walimaliza Ulimu ngazi ya Cheti hapo wasikubaliwe kujiunga na Ngazi ya Diploma wakati cheti hicho kinatambulika na wizara na pia walifaulu vizuri? Jee kunatafauti gani kati ya mfumo wa muslim na vyuo vyengine vya tz au hata Zanzibar kama SUZA ambayo pia inatoa walimu?lakini pia Zifa ambayo inatoa wahasibu ambao ni muhimili wa taifa sawa na ualimu lakini wakikubali kuanzia cheti (f4 bila c3) na sasa wameajiriwa? kutofanya vizuri kwa wanafunzi wa f4 au sio kasoro ya walimu bali kutokana kuongezeka mashule na huku pengine wizara kushusha marks kwa wahitiniwa ili mashule yetu mapya yapate vijana jambo huingiza vijana mashulemni wenye uwezo mdogo kielimu .
  kwa hivyo nadhani wizara iangalie tena mfumo huu wa c3 katiak chuo cha kiislam, Lakni pia mfumo wa muslim umebadilkia hamna tena ngazi Chet isipokua kuna Diploma. nadhani Suza, cHWAKA wanaingia wakiwa f4 na wakifaulu huingia degree. matumaini yangu swala hili litakuwa moja ya ajenda yako kulipatia ufumbuzi wakati huu vijana wakihaha kupata elimu.


   
Loading...