Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,781
- 898
KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA AZINDUA VIJANA JOGGING CLUB ALIYOIANZISHA MKOANI DODOMA.
31.07.2021
Katibu mkuu wa Uvccm Taifa Ndugu Kenani Kihongosi amezindua rasmi VIJANA JOGGING CLUB MKOANI DODOMA.
Amelekeza Mikoa yote kuwa na Vikundi Vya JOGGING VYA VIJANA lengo ikiwa kulinda afya pamoja na kudumisha Umoja na mshikamano katika Nchi yetu Pia kuepula maradhi mbali mbali.
Katibu mkuu amewasisitiza vijana na wananchi waliojitokeza katika mazoezi kuzidi kuunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais shupavu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mapambano dhidi ya UVIKO 19 pamoja na *shughuli za maendeleo.
Katibu mkuu amesema serikali Inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imedhamiria kufanya *mapinduzi makubwa ya kiuchumi na inaendelea kuleta maendeleo makubwa ambayo yatawagusa vijana na wananchi kwa ujumla hivyo lazima vijana washiriki katika kufanya kazi, Kulinda Amani pamoja na kukuza uchumi wa Taifa
Katika uzinduzi huo katibu Mkuu aliambatana na Mbunge wa jimbo la dodoma Mheshimiwa Anthony Mavunde, Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Ndugu Pili August in,Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Dodoma Ndugu Billy Chidabwa,Mwenyekiti wa uvccm wilaya ya Dodoma mjini Kasote Jumanne pamoja na Hassan Kadoke pamoja na wajumbe wa baraza mkoa wa dodoma.
Mwisho, amewataka wananchi kulinda amani pamoja na kuheshimu viongozi katika maeneo yao kwani uzalendo wa kweli ni kulinda Taifa lako.
#AmaniYetuMaishaYetu
#KaziIendelee
#MtumishiWaWote