Katibu mkuu wa uvccm taifa ahutubia manyoni, ashindwa kuwavutia vijana

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,322
Habari za uhakika kutoka manyoni zinatonya kuwa katibu mkuu wa umoja wa vijana wa ccm (uvccm) ndugu shigela amefanya mkutano wa hadhara eneo la majengo mjini manyoni, mkutano huo umehudhuriwa na wananchi wachache sana, kwa uhakika hawakufika mia moja (100) kwa kukadiria hawakuvuka hamsini (50)

Akiwahutubia wananchi hao kiduchu, amedai kuwa eti chadema kule arumeru mashariki waliahidi majukwaani, watafanya mauaji, na sasa wanatekeleza, akirejea mauaji ya vijana kule arumeru pamoja na mwenyekiti wa chadema usa river, amewaambia wasikilizaji hao kiduchu kuwa eti chadema ni chama cha kikanda, kikabila na kinakumbatia udini!!!!!

hapo awali aliahidi kutoa kadi kwa wanachama wapya mia moja na ushee, muda wa kutoa kadi ulipowadia walitokea wananchi wanne (4) tu, jambo lililomsuta machoni kwa uongo.

pitapita ya shushu mtaifa iliwakuta wananchi mara baada ya mkutano kuisha majira ya saa tisa na ushee wakilalamikia maneno ya shigela kuwa ni ya uchochezi, wakikazia ufahamu wao walihoji, Profesor Abdalah Safari na usomi wake angewezaje kujiunga na chadema kama mfumo wao na sera zao ni za kidini? hata hivyo vijana miongoni mwao wameahidi kumjibu kwa vitendo pindi chadema wakifanya mkutano wao mjini hapo.

My take:
ccm wanadhani hii ni karata muhimu kwao kuwaogofya wananchi. ndio maana jumuiya zao zote zina haha nchi nzima kujaribu karata hii. Mwisho wa kubweka kwao naamini wataishauri cc ya chama chao kwa usahihi ya kuwa hawakubalikiiiiiii.

msiulize sorce, kwani si busara muulizapo kwa uzi huu.
KAMA VIPI NAPE AJE KUKANUSHA!!!!!!
 
Wananchi wanataka kuona reli inafanya kazi, ccm badala ya kuisimamia serikali kuelekea kwenye hiyo neema, wao wanahangaika na chadema, hawatapona, wataangamia hakika!!!!!!
 
We shigella wewe, uvuvuzela na singo ya nassary haiwezi kuibadilisha ccm ikawa malaika wa nuru. Ccm imechafuka haitakatiki tena! Kama unaipenda sana, basi iandalie sanda na mahali pa kuizikia 2015. Sis mbeya hatudanganyiki na ccm, hata Pinda akiwasha koroboi yenu mbeya.
 
Bravo Manyoni!
2015 Chiligati na Lwanji pwaaaa!
Wananchi wa sasa ni waelewa. Wanaelewa kwamba kauli ya Nassari ilikuwa ni kuteleza kwa ulimi tu hali iliyotokana na msisimko wa kisiasa. CCM ni lazima wakumbuke kwamba Nassari ni binadamu na wala si malaika. Kosa lake haliwezi kufananishwa na kauli iliyotolewa na mmoja wa viongozi wao kule Mwanza (Jina silikumbuki) kwamba kama polisi wasipochukua hatua, basi wao watawaingiza vijana wao mitaani kuwapiga chadema. CCM haioni Madhambi yake mengi ambayo yameshajaa kipimo na kifuatacho kwao ni hukumu tu, bila kusahau kauli zao hatarishi kama hiyo niliyoitolea mfano.
 
Ni Watu Wachache sana Wanaopenda CCM. Vijana webgi wengi wanaoipigia Debe CCM wamegundua kwamba Ukiwa Rafiki wa Kaka yake Mwanaasha basi UDC nje nje. Ni Njaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hivi ina maana CCM hawana kitu kingine cha kuwaambia wananchi? Kama Nassari hakuongea huko Arusha CCM wangesema nini?
 
Acha nicheke kidhungu tu. kwi kwi kwi.
.
"MADARAKA HUMBADILISHA MTU, YAPATE KWANZA NDIPO TUJUE ULIVYO".
 
ccm zama zao zimeisha.hapa Manyoni 2010 kama chadema wangemsimamisha mgombea makini hakika angepita mfano manyoni magh waliiba kura.
 
Huu uzushi wa Katibu wa UVCCM haujanishtua hata kidogo.
Ningeshtuka sana ikiwa angekuwa ameongea masuala ya maana.

Yaani kiongozi wa kitaifa anajikinahi na kutangaza atawapa kadi wanachama wapya zaidi ya mia, unafika muda haya piteni mchukue kadi wanatokea wanne i.e moja, mbili, tatu, nne halafu mmhh, mi ningetimkia chadema baada tu ya kushuka jukwaani.
 
tuko pa1 wakaz wnzngu wa mnyoni ecko sana. Hakuna kulala mpaka 2015 2takapokua chadema tunachukua nchi. Pplz ......... Malizia bas we gamba!
 
Sasa kama ccm kila sehemu inakataliwa/kukimbiwa, ajila za kina Nape zitakuwaje? Duu!!! Itabidi vuvuzela nape akaimbe taarabu....
 
Back
Top Bottom