Katibu Mkuu wa UN: Nimeshtushwa na hatua ya Ethiopia kuwatimua maafisa wetu

jollyman91

Member
Sep 21, 2021
69
29
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa sana na kitendo cha serikali ya Ethiopia kuwafukuza maafisa wa umoja huo wanaohudumu nchini humo.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake mjini New York, Guterres amesema, "nimeshtushwa na habari kwamba serikali ya Ethiopia imetangaza maafisa saba wa Umoja wa Mataifa, pamoja na maafisa wakuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, ni watu wasiokubalika au kutakikana nchini humo".

Katibu Mkuu wa UN amesisitiza kwamba shughuli zote za kibinadamu za umoja huo zinaongozwa na kanuni za ubinadamu, kutopendelea na uhuru.

Guterres aidha amesema, ana imani kamili na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walioko nchini Ethiopia na kwamba umoja huo umejizatiti kuwasaidia watu wa Ethiopia, ambao wanategemea msaada wa kibinadamu.

4by03b65d8c7a51uwwz_800C450.jpg
Utoaji huduma za UN kwa watu wa Tigray, Ethiopia
Ameongezea kwa kusema: "tunajadiliana na serikali ya Ethiopia kwa matarajio kwamba wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliotimuliwa wataruhusiwa kuendelela na kazi yao muhimu."

Nchini Ethiopia, Umoja wa Mataifa unatoa msaada wa kuokoa maisha, ikiwa ni pamoja na chakula, dawa, maji na vifaa vya usafi kwa watu wanaohitajia sana msaada huo.

Kwa mujibu wa duru za habari , maafisa hao wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu nchini Ethiopia walipewa masaa 72 kuanzia jana Alkhamisi wawe wameshaondoka nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imesema, maafisa hao wa UN, wakiwemo wa Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu OCHA na wa Shirika la Kuhudumia Watoto UNICEF wametakiwa waondoke kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.../
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom